Lenie
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 17,229
- 50,144
NakaziaTafuta pesa kaka,
Kujiamini kutakuja automatic,
Sitanii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NakaziaTafuta pesa kaka,
Kujiamini kutakuja automatic,
Sitanii
Asante,Nakazia
Pole kwa hiyo changamoto. Ni tatizo, lakini si tatizo kubwa saaana. Hapana. "Linatibika". Hata Mimi nilishawahi kuwa na changamoto kama hiyo, na watu wengine wengi, lakini kwa sasa si tatizo tena.yaani kiujumli hili tatizo la kutojiamini limenianza toka nikiwa mtoto mpaka kufikia sasa japo nahisi limepungua kidogo labda kutokana na kukutana na watu wa tofauti tofauti kila wakati
kwa mfano kuna kitu nimewahi buni nikapeleka shuleni veta nikaambiwa nikitolee maelezo nilishindwa kabisa kila nikijitahidi mikono inatetemeka tu,
Ushauri mzuri sana huu. Akiufanyia kazi. Tatizo lake litaisha kabisa.Pole kwa hiyo changamoto. Ni tatizo, lakini si tatizo kubwa saaana. Hapana. "Linatibika". Hata Mimi nilishawahi kuwa na changamoto kama hiyo, na watu wengine wengi, lakini kwa sasa si tatizo tena...
Mkuu hawa watu wanapatikana wapi,Hii ni social phobia, onana na watu wanaoshugulika watakusaidia
yaani kiujumli hili tatizo la kutojiamini limenianza toka nikiwa mtoto mpaka kufikia sasa japo nahisi limepungua kidogo labda kutokana na kukutana na watu wa tofauti tofauti kila wakati
kwa mfano kuna kitu nimewahi buni nikapeleka shuleni veta nikaambiwa nikitolee maelezo nilishindwa kabisa kila nikijitahidi mikono inatetemeka tu,
Hospital kubwaMkuu hawa watu wanapatikana wapi,
Tafuta bangi mbichi changanya kwenye mboga yoyote ya majani ichemke vzr kula na ugali Baada ya wiki Moja utaona Kila mtu kama sisiminzi na hapo ndo kujiamini kutaanzayaani kiujumli hili tatizo la kutojiamini limenianza toka nikiwa mtoto mpaka kufikia sasa japo nahisi limepungua kidogo labda kutokana na kukutana na watu wa tofauti tofauti kila wakati
kwa mfano kuna kitu nimewahi buni nikapeleka shuleni veta nikaambiwa nikitolee maelezo nilishindwa kabisa kila nikijitahidi mikono inatetemeka tu,
yaani kiujumli hili tatizo la kutojiamini limenianza toka nikiwa mtoto mpaka kufikia sasa japo nahisi limepungua kidogo labda kutokana na kukutana na watu wa tofauti tofauti kila wakati
kwa mfano kuna kitu nimewahi buni nikapeleka shuleni veta nikaambiwa nikitolee maelezo nilishindwa kabisa kila nikijitahidi mikono inatetemeka tu,
Ni kweli, achukue k vant ndogo lakini anywe robo, akimaliza atafute Pk ili akate halufuPiga k-vant ndogo utakuja nishukuru.
yes! wanafunzi wa udakitari wanaitumia hii dawa sana wakiwa wanafanya presentetionsku nyingine ukiwa na presentations tumia propanol
Pole kwa hiyo changamoto. Ni tatizo, lakini si tatizo kubwa saaana. Hapana. "Linatibika". Hata Mimi nilishawahi kuwa na changamoto kama hiyo, na watu wengine wengi, lakini kwa sasa si tatizo tena.
Kwa nchi zingine kama Marekani, kuna mpaka vyuo vinavyotoa mafunzo yanayowasaidia watu kuwa na ujasiri wa kuzungumza mbele ya hadhara kwa ufasaha. Warren Buffett alishapitia kwenye hiyo Course, nafikiri na Barack Obama pia.
Mojawapo ya hivyo "Vyuo" ni DALE CARNEGIE TRAINING. Sijui kama taasisi kama hizo zinapatikana huku kwetu Tz.
Kwa kuwa inawezekana usipate "course" ya kukusaidia kuondokana na hiyo adha, nakushauri ufanye yafuatayo:
1. FANYA HICHO UNACHOKIOGOPA
Unaogopa kuongea mbele za watu? Dawa yake siyo kukwepa bali ni kuikabili kwa kufanyia hicho hicho ambacho unakihofia. Hiyo ni kanuni ya Kisaikolojia: FANYA UNACHOKIOGOPA NA HOFU ITATOWEKA.
Kama mtu, kwa mfano, anaogopa kupanda basi, anashauriwa apande basi mara nyingi na hatimaye hofu itayeyuka. Kama anaogopa kupanda ndege, anapaswa kupanda mara nyingi na hatimaye hofu itageuka kuwa shauku.
Hofu ni tabia, kadhalika na ujasiri. Moja ni kinyume ya mwenzake. Na zote hizo, hofu na ujasiri, ni tabia za kujifunza. Ndiyo kusema, ama ulijifunza, au ulifundishwa kuwa na hofu. Na kwa sababu hiyo basi, unaweza kujifunza kinyume chake, na hofu ikaondoka bila kuaga.
Kwa kawaida, inaweza kumchukua mtu siku 21 kujiumbia tabia mpya. Anachopaswa kifanya ni kulifanya jambo hilo kila siku, na hatimaye hilo tendo litatengenezewa faili lake kwenye ubongo wa huyo mtu. Inapifikia hapo, mtu hatahitaji tena kujitutumua kufanya, badala yake atakuwa " mtumwa" wa hiyo tabia mpya. Kama ni tabia nzuri, itakuwa heri kwake. Kuwa na ujasiri wa kuongea mbele za watu ni tabia nzuri.
Kwa hiyo unachopaswa kufanya ni kutafuta fursa ya kuongea mbele za watu kila siku, hata kama ni watu wachache tu. Usipoweza kuipata hiyo fursa kila siku, jitahidi alau iwe mara tatu au hata mbili kwa wiki. Cha msingi, wiki isiishe bila kuongea mbele ya watu, hata kama ni kundi la watu watano tu. Wanasema, "repeatations is the mother of learning"
Nikupe angalizo pia kuwa mwanzoni hutaona ni rahisi, wala hutajihisi kutaka kufanya hilo. Lakini ujue hapo ndipo panapomtofautisha "mwanaume" na "mvulana'. "Mwanaume" atatenda, siyo kile anachojisikia kufanya, bali anachopaswa kufanya bila kujali kama anajisikia au hajisikii. Atafanya, hata kama hapendi kufanya, atafanya tu. Hana uchaguzi mwingine zaidi ya kufanya, hata kama itamlazimu kufanya huku akitokwa na machozi, atafanya kwa sababu kanuni inamtaka afanye.
Anapofanikiwa kufanya anachopaswa kufanya hata kama hapendi kufanya, itampelekea afikie hatua ya kufanya kile anachopenda kukifanya kwa wakati anaoutaka kukifanya.
Unaweza ukauliza, "sitachekwa?" Hilo nitalijibu katika pointi namba tatu.
2. HATA KAMA UNAONGEA MBELE YA WATU MILIONI MOJA, CHUKULIA KAMA UNAZUNGUMZA NA MTU MMOJA, TENA WA KAWIDA SANA
Mtu mmoja alishawahi kusema, "the only person who is smarter than anybody is everybody". Kwa tafsiri isiyo rasmi, anamaanisha MTU PEKEE MWENYE AKILI KULIKO MTU YEYOTE NI KILA MTU. Huo ndiyo mtazamo unaopaswa kuwa nao. Hata kama ni mwanafunzi wa darasa la tatu, na hadhira yako inawajumuisha maprofesa wa Chuo kikuu na wakuu wa nchi, wachukulie kwamba hao wote ni wanafunzi wako, na unachokiwasilisha kwao ndicho pekee kilicho sahihi hivyo ni lazima wakusikilize. Hicho siyo kiburi, ni ujasiri.
Na kama watu unaoongea nao ni wengi, usiongee kama mtu anayehutubia maelfu ya watu. Kwenye ufahamu wako jenga taswira kuwa UNAZUNGUMZA na mtu mmoja.
Unaponyanyuka kwenda kuanza kuzungumza, epuka kuwaangalia watu wote wanaokutazama. Badala yake, unapoanza, elekeza macho yako kwa mtu mmoja unayemwona ni wa kawaida kwako, na uchukulie kuwa huyo ndiye unayezungumza naye. Sekunde chache baada ya kuanza kuongea, ukiona umeshaupata "utulivu" wa ndani, unaweza ukaangaza macho maeneo yote, lakini kwa utulivu na kwa kujiamini.
Unapoongea pia usisimame sehemu moja kama gogo. Kama utaratibu wa mahali husika haukubani, unaweza ukatembea kidogo pande zote, lakini si kama anayefukuzwa. Cha MUHIMU, cho chote utakachokuwa unakifanya, ujitahidi kukiona kwenye fikra zako kuwa ni rahisi na ni cha kawaida, nacho kitakuwa hivyo.
3. WAKIANZA KUKUCHEKA, WEWE JICHEKE KWA BIDII KUWAZIDI
Kwa mtu ambaye hajazoea kuongea kwenye umati wa watu, endapo atakosea na watu wakamcheka, kunaweza kumsababisha apaniki na kushindwa kuendelea kuongea. Kuna watu walishawahi kukutana na hiyo kadhia.
Lakini kama unataka hiyo isikukwamishe, ukikosea, na hata kupelekea watu kucheka, wewe usijali. Badala yake, jumuika nao kucheka, ila tu wewe ujitahidi kucheka kwa bidii kuwazidi wote.
Hiyo itasaidia katika namna mbili.
Ya kwanza, itakuepusha kuwa na aibu na kujiona kuwa umekosea, badala yake, akili yako itatafsiri kuwa umeamua kufanya hivyo kwa ajili ya kunogesha hotuba. Utakapomaliza kucheka utajihisi kuongezeka kwa ujasiri na uwezo wa kulimiliki "jukwaa"
Ya pili, hadhira yako itafurahi na kuongeza umakini wa kukufuatilia. Wengine wanaweza wakafikiri uliamua "kulichomekea" hilo kwa lengo la kuchekesha, kitu ambacho ni sahihi pia wakati mwingine pindi unapotoa "hotuba".
Acha niishie hapo. Na kama wewe ni msomaji wa Vitabu, nakushauri uvisome vitabu vya DALE CARNEGIE, hasa hivi vitatu:
(A). HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE
(B). THE ART OF PUBLIC SPEAKING
(C). HOW TO STOP WORRYING AND START LIVING
Kwa kufanya hivyo hatakuwa ametatua tatizo kwa kuzalisha tatizo jingine?Tafuta bangi mbichi changanya kwenye mboga yoyote ya majani ichemke vzr kula na ugali Baada ya wiki Moja utaona Kila mtu kama sisiminzi na hapo ndo kujiamini kutaanza
Awa yake ni kujiamini tu.yaani kiujumli hili tatizo la kutojiamini limenianza toka nikiwa mtoto mpaka kufikia sasa japo nahisi limepungua kidogo labda kutokana na kukutana na watu wa tofauti tofauti kila wakati
kwa mfano kuna kitu nimewahi buni nikapeleka shuleni veta nikaambiwa nikitolee maelezo nilishindwa kabisa kila nikijitahidi mikono inatetemeka tu,
Hongera kwa madini mkuu, naamini kupitia hii post yako wengi watajifunza kujiamini wanapokuwa kwenye kadamnasi
🙏🙏Hongera kwa madini mkuu, naamini kupitia hii post yako wengi watajifunza kujiamini wanapokuwa kwenye kadamnasi.
Duh!!Anza kuwa na mademu si chini ya watatu utanishukuru