Mwaka 2011 Kuna project ambayo ilitakiwa tuipresent kwa katibu mkuu was baraza x tulikuwa watatu na tulimchagua mmoja wetu ambaye alitakiwa awe msemaji, dakika kumi kabla ya kuanza mkutano tukaonyeshwa chumba cha mkutano watu wamejaa wrote wapo na notebooks, laptop ni wataalam kutoka idara mbalimbali za serikali pamoja na bank ya Crdb.
Jamaa tuliyemuandaa kuzungumza akashikwa na yoga akanikanyaga mguu akaniambia hatoweza kuzungumza ameshikwa na woga, basi chap nikatoka nje nikajifanya Kuna documents nimesahau ndani ya gari nikaruka Posta ya zamani nikachukua nyagi ndogo nikabugia fasta nikachukua chewing gum na ndizi mbivu nikala nikarudi nikaingia mkutanoni nikafanya presentation ya hatari pangua maswali moja baada ya nyingine.
Yule katibu akasema vijana wadogo mna mambo makubwa na mko vizuri sana, tulitoka pale tukaenda feri kupunga upepo jamaa zangu hawakuamini kama no mm au mzimu, interview zangu zote nilipiga nikiwa nimelamba kilaji kidogo na zote nilifaulu, ninapoenda nagonga nusu glass ya royal stag iko poa na haina harufu so ni ngumu kwa mtu yeyote aliyekaribu kuhisi harufu.