Mwenyekiti, Katibu Mkuu CHADEMA kigugumizi cha nini sakata la Wabunge wa Viti Maalum?

Mwenyekiti, Katibu Mkuu CHADEMA kigugumizi cha nini sakata la Wabunge wa Viti Maalum?

Mnyika na mbowe okoeni chama. Hata kikifa kwa kukosa ruzuku, mtakuwa mmeingia kwenye historia ya mashujaa wa demokrasia Tanzania. Tafadhali fukuza Kenan na wabunge viti maalaum wote wa chadema. Hawa si wanachama wa chadema. Ni wahuni tu.
Utambulike kama shujaa huku umekufa kwa njaa?
 
Kuhusiana na hii ishu ya wabunge wa Viti Maalum CHADEMA.

Naona watu wengi wanashindwa kuelewa nini kinaendelea juu ya kilichotokea leo, wapo wanaotaka hao wabunge wa viti maalumu waliokwenda kuapishwa leo, wafukuzwe chamani kwa kuwa wamekwenda kinyume na msimamo wa chama kama anavyosema Mnyika (Katibu Mkuu wa chama)

Ila me binafsi naona kama wafuasi wa CHADEMA wanachezewa 'mind game' na viongozi wapo wakuu wote wakiwemo Mnyika na Lissu.

Kwanini basi me nafikiri hivyo?

Juzi tu hapa Lissu pamoja na Zitto waliitisha mkutano na waandishi wa habari, ajabu katika mkutano huo wamezungumzia jambo ambalo linafahamika kwa kila mtu.

Wamezungumzia jambo ambalo walishalizingumzia muda si, mwingi sana.

Sasa mtu unajiuliza nini lengo la hawa jamaa kuwaita wanahabari na kuwaambia kwamba hawatambui matokeo ya uchaguzi huu na hawatashirikiana na serikali iliyopo madarakani hivi sasa?

Si hata mwezi haujaisha wamelisema hili?

Kwanini juzi wameamua kulirudia tena?

Kwa sababu walikuwa wanajua nini kitatokea ndani ya muda mfupi ujao, na wao ni sehemu ya maamuzi hayo ila tu wanawahadaa wafuasi wao ili ionekane kwamba wao wana misimamo isiyoyumba.

Kinachofuata muda si mrefu ni Maalim Seif kujiunga na serikali ya Mwinyi then game over, hakuna cha uchaguzi haukuwa wa kidemokrasia wala haki za binadamu zimevunjwa.

Kazi kwenu mnaoamini.
 
Mnyika na mbowe okoeni chama. Hata kikifa kwa kukosa ruzuku, mtakuwa mmeingia kwenye historia ya mashujaa wa demokrasia Tanzania. Tafadhali fukuza Kenan na wabunge viti maalaum wote wa chadema. Hawa si wanachama wa chadema. Ni wahuni tu.

Hakuna chama kilichokuwa kinakufa kwa kukosa ruzuku. Kama wanachama tuliwapa hata options:


Kwa waliyofanya kina Halima hata tulichochanga kuwatoa magereza kinauma.

Na waende tu. Hawa ni mzigo na wametugharimu kwa kweli.

Kufukuzwa kwa wasaliti wote isichukue wiki tafadhali. Vinginevyo wengi wetu tutachukua maamuzi magumu!
 
Kuweka misimamo wazi siyo kuropoka.

Kwamba kuna mbunge bungeni na haafikiani na msingi mkuu wa chama kuhusiana na haramu ya uchaguzi wa 2020, kumlea huyo ni kulea kansa.

"If you disobey you go."

Hiyo si kuropoka. Huo ni msimamo thabiti!
Punguza jazba, usifoke!
 
Sisi: CHADEMA hawawezi kupeleka viti maalum..

Viti maalum:Tunashukuru chama chetu kwa kutuchagua kuwa wawawakilishi.. Tutafanya kazi kwa uaminifu kama kambi rasmi ya upinzani..
 
We na makamanda wenzio ndo mnajichanganya, chama kilishajipambanua kama chama kisichoeleweka kinasimamia nini na kinataka nini. ili uendane nao na we inabidi usieleweke tu

Maumivu hayatakaa yawaishe.

Kila mnachojaribu mnatahamaki tuko vizuri zaidi.

Kwamba kina Esther kwani hatukujua ni maafisa vipenyo mliowapenyeza kama kina katawi?

Habari mbaya kwenu: "mapambano bado yanaendelea na kuvuja kwa pakacha hakujawahi kuwa issue kwa mchukuzi."
 
Maumivu hayatakaa yawaishe.

Kila mnachojaribu mnatahamaki tuko vizuri zaidi.

Kwamba kina Esther kwani hatukujua ni maafisa vipenyo mliowapenyeza kama kina katawi?

Habari mbaya kwenu: "mapambano bado yanaendelea na kuvuja kwa pakacha hakujawahi kuwa issue kwa mchukuzi."
Mliwajua ila mkaendelea kuwa nao! Hivi hua mnajisikia hata mnayoyaongea?
 
Mbowe hana cha kupoteza yeye anaangalia ruzuku tu,jishangae wewe mishipa ya shingo imekutoka kujifanya unakijua chama kuliko Mbowe na mkwe wake.

Hivi vyama ni biashara za watu,ukiingilia maslahi ya watu unatolewa kama Chacha.
 
Hiki ndo ambacho nilikua nakiwaza, nadhani tumemfahamu Tundu Lissu kwa muda mrefu, ni wakati wa kuanzisha chama chake sasa, hakika watu wenye misimamo kama yake tupo na labda itakua ndio njia mpya kuelekea serikali mpya. Ila kwa Chadema i think tumeona sura harisi ya walio wengi kule katika uongozi, tamaa na kutokujiamini na kutochange mbinu vinawamaliza very slowly, God forbid !!!!
Nani atasajili chama cha yule kichaa.Kitakuwa chama cha siasa au cha kigaidi??
 
Kinachofuata ni shughuli za kisiasa kuruhusiwa kuendelea kama kawa badala ya kusubiri 2025. Fursa zaidi kwa CHADEMA kuitisha mikutano kujinadi kwa Watanzania.
 
Mliwajua ila mkaendelea kuwa nao! Hivi hua mnajisikia hata mnayoyaongea?

Kwani hata sasa mmekwisha? Habari mbaya kwenu ni kuwa hatuna pressure nanyi muda ukifika tutakula sahani moja nanyi. Mmoja mmoja na kila mmoja kwa wakati wake.

Mbona wa bao la dakika 90 angalipo bado hajarudi nyumbani?

Kwani Mamvi au Sumaye au Manywele na wengine hawakuvumiliwa kimya kimya hadi ilipobidi? Nani anawakumbuka?

Akili zenu kutoyaona yote haya ni kuwa hazina akili. Chukueni mbali hizo takataka na pia hata zote ambazo zingalipo.

Inachukua kuwa mzalendo haswa kupambana tokea tuliko. Huku njaa ndiyo kwao.

Ogopa njaa uolewe!
 
Nani atasajili chama cha yule kichaa.Kitakuwa chama cha siasa au cha kigaidi??
Well kitasajiliwa tu, he is good enough na unafahamu hilo, ndo sababu una admit kwa kumfananisha na gaidi, means msimamo wake unatisha, kwa hayo machane ana qualify kuunda chama na kikaaminiwa.
 
Mbowe na mnyika mkumbuke tuliwachangia fedha msifungwe. Hao kina Halima halikadhalika. Uchafuzi wa Oktoba umewaacha watu na vilema, wengine wamekufa. Leo hii mnakisaliti chama!! Wallahi, wasipofukuzwa uwanachama, CHADEMA bye bye. Katafuteni kazi nyingine.
 
Back
Top Bottom