Mwenyekiti, Katibu Mkuu CHADEMA kigugumizi cha nini sakata la Wabunge wa Viti Maalum?


Mnaombea mfarakano eeh?

Ngoja tuwa delete hao wadada na kipandikizi chenu kwanza ndipo mtatambua kuwa kumbe tuko imara kuliko wakati wowote!
 
Wewe ndio unajua haramu ya uchaguzi ? Wakati viongozi wa upinzani wanajua kabisa kwamba wameshindwa kihalali. Endelea kujitekenya na kucheka mwenyewe wakati wenye chama chao wako mjengoni. Wewe baki kukesha humu JF wenzako wanapiga mpunga. Hapo ndipo utajua kwamba siasa ni sayansi siyo mihemuko ya kishamba. Kumbuka kwamba Mkuu wa nchi hajaribiwi na washamba wa siasa kama nyie.
Kuweka misimamo wazi siyo kuropoka.

Kwamba kuna mbunge bungeni na haafikiani na msingi mkuu wa chama kuhusiana na haramu ya uchaguzi wa 2020, kumlea huyo ni kulea kansa.

"If you disobey you go."

Hiyo si kuropoka. Huo ni msimamo thabiti!
 

Kwamba upinzani wanajua ulikuwa halali?

Rudisheni mrejesho kwa waliowatuma mpambano bado unogile.

Habari mbaya kwenu ni kuwa, kama mliahidiwa bonus mtasubiri sana!
 
Huyo Zitto na Lissu ndio mzigo kabisa. Hakuna upinzani nchi hii mpaka Mungu ainue kizazi kingine labda kuanzia mwaka 2050 !

Hiiii bagosha, nizakale!

Salimia muganza.
 
Kwani sasa diyo looser ? We vipi
 
Wahuni ni nyie mlioshindwa kihalali na kuanza kubwabwaja
 
Hana ubavu wa kuunda chama huyo
Well kitasajiliwa tu, he is good enough na unafahamu hilo, ndo sababu una admit kwa kumfananisha na gaidi, means msimamo wake unatisha, kwa hayo machane ana qualify kuunda chama na kikaaminiwa.
 
Kuweka misimamo wazi siyo kuropoka.

Kwamba kuna mbunge bungeni na haafikiani na msingi mkuu wa chama kuhusiana na haramu ya uchaguzi wa 2020, kumlea huyo ni kulea kansa.

"If you disobey you go."

Hiyo si kuropoka. Huo ni msimamo thabiti!
Tuone kama watakuwa wameonja sumu kwa ulimi
 
Mnaombea mfarakano eeh?

Ngoja tuwa delete hao wadada na kipandikizi chenu kwanza ndipo mtatambua kuwa kumbe tuko imara kuliko wakati wowote!
Mifarakano haiombewi mkuu hutengenezwa na hakuna wa kumlaumu zaidi yenu wahusika.

Mkisimama pamoja na kusimamia maslahi ya wanachama na nchi hakuna wa kuzua mfarakano. Lakini chama kila mmoja ana msimamo wake kwanini misimamo yenu isiwafarakanishe?

Huyu anaongea hili, huyo lile, huyo anajua hiki, yule kile na mengine mengi. Hapo sasa mnafarakana kimawazo baadae kivitendo kama jana. Na mkiendelea mtasambaratika na kuvunjika vipande. Ile dhambi ya kutaka kuivuruga Tanzania kipindi cha kampeni ndio inawatafuna na haitwaacha salama mtasambaratika mpaka mpotee kwenye ramani.

Tuliwaambia TUNDU ni Liability, mkatukana sana. Ni mwanaharakati asiye na dira, mkasema NI YEYE. Sasa msipochukua hatua NI YEYE anaenda kuua chama kwa uanaharakati wake. Atakifanya chama kama jukwaa lake kuendesha uana harakati badala ya kujikita katika kukipambanua chama kwa sera zake bora zilizokipa umaarufu.
 
Amka usingizini Bro. Wabunge 19; kila mwezi wakichangia chama chao milioni moja; kwa mwaka milioni 12 X 19 unapata milioni 228, mara miaka mitano unapata milioni 1,140 (Bilioni moja na ushee!!!!) ; sasa busara yao ni bora kuzipata hizi halafu mnagawana na Viongozi. Mwenyekiti anachukua chake na Katibu....nk. Wanachama wengine walie tuuuuu. Ukiongeza na yule wa Nkasi mshiko unazidi kunoga. HILO SWALA KWISHNEI. Kilichobaki ni usaniii tuuu kuwatuliza watu kama wewe. AMKA NDUGU YANGU.
 
Hizo nafasi ni za wanake tu! kwahiyo hata kama wangependa kumpoza kwa kumpatia HAIWEZEKANI! Ina maana zile kura alizopata Mh Lissu zipite bila kutambulika? Pingania mabadiliko ya katiba kama kweli unataka mabadiliko!!
 

Unapojinasibu kuwa "mliwaambia" hivi nyie huwa ni kina nani? Kwanini isiwe mnajitambulisha kabisa mamburula nyie?

Kiufupi ni kuwa yote uliyoandika ni utopolo mtupu.
 
Unapojinasibu kuwa "mliwaambia" hivi nyie huwa ni kina nani? Kwanini isiwe mnajitambulisha kabisa mamburula nyie?

Kiufupi ni kuwa yote uliyoandika ni utopolo mtupu.
Subiri utaona ulioandika wewe na mimi utopolo ni upi.

Poneni majeruhi kwanza ya uchaguzi na ya jana kwa mama zenu kisha mtulizane.

Tuliwaambia

Na bado tutawaambia
 
Ninajua Katibu Mkuu wa CHADEMA, John John Mnyika amelitolea ufafanuzi, lakini ili kurudisha confidence ya wana CHADEMA, ni vema ukitoa neno hata moja ili roho za wafasi na watanzania wa CHADEMA zipone.

Kuna mkanganyiko ambao unahitaji top Executive kuusemea. Najua 27/11/2020 kuna kikao cha Kamati Kuu kujadili suala hilo, lakini "Siasa" ziko hivyo, unatoka unalisemea.

Hili ni muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…