Mwenyekiti Mbowe, kweli Rais Samia amefanya mazuri ila sifa kwake zimezidi!

Naunga mkono hoja hii......Cdm waanze kumuandaa mrithi wa Mbowe sasa hivi mapema kwa faida yao na nchi kwa ujumla.

JokaKuu Pascal Mayalla Kalamu zitto junior
Mimi nina swali tu, kwako mkuu 'Proved', na kwa wengine wote watakaopenda kulijibu hili swali.

Kwa hiyo, katika mkutano wote, viongozi wote wa CHADEMA waliopewa nafasi ya kuzungumza, hakuna hata mmoja aliyegusia swala la KATIBA MPYA?

Ningependa kujua kuhusu hili.

Inawezekana CHADEMA wamepewa amri wasiguse kabisa juu ya jambo hili muhimu?

Kulizungumzia ni kama kuvunja sheria?
 
Angeenda bila kulewa asingekuwa huru kuyataja mazuri ya Mama Samia. Kafanya vyema sana. Inahitaji kujitoa ufahamu kwanza mbele ya BAVICHA ili uweze kuzungumzia mazuri ya CCM. Mbowe ni mtaalamu wa siasa za nchi hii.
Ninyi nyote mnaendeshwa na wivu uliopitiliza. Mlishasema Kanda ya Ziwa ni bado iko na Mtu aliyekwishatangulia mbele ya Haki. Hivyo Uzinduzi waleo usingekuwa na mapokezi mazuri. Uwanja umetapika. Kwanini msikose cha kuongea? Matokeo yake mnakimbilia eti Mh Mbowe kalewa. Upuuzi tu umewatawala.
 
Leo kani
Mbowe astaafu tu. Hata mvuto umepotea kabisa. Leo hata Sugu ammemzidi. Nadhani Lissu na Heche wapewe nafasi la sivyo Mbowe anaenda kuiua CHADEMA kwa kumfurahisha Samiah. Anajali utaifa wakati wengine hawajali Hilo.
 
Hakuna ubaya. Sasa kama Mhe. Rais anafanya mambo makubwa asikiri ukweli? Kwa wanaozunguuka nchini watajua Mhe. Rais Samia anafanya mambo makubwa sana. Hii miradi ikja kuanza kuleta matokeo kuna watu watatamani kujificha. #Tumpongeze Mhe. Rais.🙏🙏🙏
 
Katiba Mpya ilishakubaliwa, sidhani Kama Kuna haja ya kuidai. Maana Rais Alishaikubali.
 
Katiba Mpya ilishakubaliwa, sidhani Kama Kuna haja ya kuidai. Maana Rais Alishaikubali.
LOOoo.
Unaamini hivyo mkuu 'econo'?

Ilikubaliwa lini?

Kwa hiyo hakuna tena kitu cha kujadili, kuhusu katiba, hata kama "imekubaliwa"?

Mbona wakati huu ndio ingekuwa ajenda kubwa kabisa kuwaelimisha wananchi juu ya utarajio wa hiyo iliyokubaliwa!
 
Mbona anaongea kama Hana amani yaani kama anawasiwasi fulani hivi

Yupo pekee yake anamkubali Samiah, hivyo lazima aogope. Kwa Sasa hata Pambalu atatufaa Sana kuwa mwenyekiti ameongea vizuri na anahamasisha. Sio sifa kwa Samiah halafu unadai hujalamba asali.
 
LOOoo.
Unaamini hivyo mkuu 'econo'?

Ilikubaliwa lini?

Kwa hiyo hakuna tena kitu cha kujadili, kuhusu katiba, hata kama "imekubaliwa"?

Mbona wakati huu ndio ingekuwa ajenda kubwa kabisa kuwaelimisha wananchi juu ya utarajio wa hiyo iliyokubaliwa!

Nimesema kwa sababu Rais kasema atateua kamati hivi karibuni , sidhani Kama kuna haja ya kupiga kelele Tena. Tume ikiundwa na ikataka mjadala happy ndipo CHADEMA tutaingia na kudai yanayofaa.
 
Ajirekebishe kesho Musoma akileta porojo za leo tutamkataa. Mbowe analazimisha walichoongea sirini na Samiah chama kikifate. Maalim Seif aliongea kwa Siri na Amani karume lakini kilichotokea baadae wote tunajua.
 
Nimesema kwa sababu Rais kasema atateua kamati hivi karibuni , sidhani Kama kuna haja ya kupiga kelele Tena. Tume ikiundwa na ikataka mjadala happy ndipo CHADEMA tutaingia na kudai yanayofaa.
Basi sawa mkuu, endelea kusubiri.

Hii ndiyo siasa. Wakati huu kwa CHADEMA 'focus' yote ingekuwa hapo. Hakuna jambo kubwa zaidi ya hilo kwa sasa; kwa maana matatizo mengi ya nchi yanatokea hapo kwenye hiyo katiba.

Wewe utayaita makelele, lakini kwa wenye fikra hiyo ndiyo ajenda kuu wanayopashwa kuisimamia CHADEMA kwa wakati huu.
 
Mbowe kazingua Sana. Watu tulikua na kiu Sana, yeye kashindwa kuikata. Na suggest twende na slogan mpya.
 
Leo kani

Mbowe astaafu tu. Hata mvuto umepotea kabisa. Leo hata Sugu ammemzidi. Nadhani Lissu na Heche wapewe nafasi la sivyo Mbowe anaenda kuiua CHADEMA kwa kumfurahisha Samiah. Anajali utaifa wakati wengine hawajali Hilo.
Ana cha utaifa wowote huyo mlamba asali, angekuwa anajali utaifa angeongea kuhusu katiba mpya na mfumuko wabei. Anajali tumbolake tu.

Bado kuna mengi yanakuja.
 
Ajirekebishe kesho Musoma akileta porojo za leo tutamkataa. Mbowe analazimisha walichoongea sirini na Samiah chama kikifate. Maalim Seif aliongea kwa Siri na Amani karume lakini kilichotokea baadae wote tunajua.
Sasa usije ukakuta unajichanganya mwenyewe mkuu wangu 'econo'.
Hayo ya "sirini", ndiyo hayo hayo yahusuyo hiyo Katiba; kwa sababu mambo ya katiba siyo mambo rafiki kwa CCM hata kidogo.
 
Mkuu, Rais kakubali mchakato wa katiba mpya uanze na kasema anateua tume mpya ya Katiba. Sasa hapo utadai Nini?. Tutadai tukiona muda umeenda na Tume haiundwi. Leo, Mwenyekiti alitakiwa kutoa mwelekeo wa nini tukiseme kwa miaka miwili ijayo. Reformations zipi titazileta kuhusu uchumi, elimu, vijana, uvuvi nk.
 
Kwa hiyo kinachomuudhi Mbowe na haters wengine ni wingi wa sifa Kwa Rais au?

Narudia tena Kauli Mbiu Yangu kwamba hakuna Rais atamfikia Dr.Samia kwenye utekelezaji wa ilani ya ccm na sababu ni kwamba Rais Samia Yuko focused sana kwenye vitu basic sio mambo ya kijinga kijinga
 
Mkuu wangu, tuliache hili, naona hatutafika mwisho wake leo.
Kwa chama kama CHADEMA, hiyo ahadi unayoiweka hapa ndiyo iwe kizuizi cha wao kuongelea ajenda muhimu kama hiyo?

Kwani wao kuzungumzia swala hilo ni kuikataza hiyo tume iliyoahidiwa?

Sijui, lakini pengine tutapata nafasi katika wakati maalum, tutakapokutana hapa wewe na mimi kupongezana kuhusu hilo la Kamati teule!
 
..wanaozungumzia kulamba asali ni wanaCcm.

..Ccm siku zote hawajibu hoja, bali hujaribu kumchafua mtoa hoja kwa propaganda zao.

..hata ktk hii mikutano ya Cdm tutegemee mambo mengi ya kizushi na kipropaganda kutoka kwa magenge ya Ccm.

..sitegemei kusikia Ccm wametoa hoja mbadala kuhusu Katiba Mpya, Tume Huru ya uchaguzi, Mfumuko wa bei, Ukosefu wa ajira, au hoja zozote zinazotolewa na wapinzani.
 
Ana cha utaifa wowote huyo mlamba asali, angekuwa anajali utaifa angeongea kuhusu katiba mpya na mfumuko wabei. Anajali tumbolake tu.

Bado kuna mengi yanakuja.

Kanidissapoint, leo alikuwa anaipa CHADEMA point tatu kaishia kujikanyaga na kulaumu Viongozi wake kazidiwa Hadi na Kiwanga au Pambalu wameongea wakaeleweka.

Mara taifa moja, Mara sijalamba asali, Mara mama Samiah mzuri etc. Leo alitakiwa alete slogan ya kutembea nayo miaka miwili ambayo itahusu wananchi na Mageuzi ya kiuchumi. Hapo leo CHADEMA ingevuna point tatu. Ila nawashukuru Viongozi wote wameukataa ujinga wa Mwenyekiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…