Udini, ukabila na uvyama, havina Maana katika matukio kama haya, matukio ambayo utake usitake Lazima ufe, Haina Afya hata kidogo kuendeleza utani usio na tija
Huyo anayeandika mambo ya Corona wanapokufa sjui wa CCM, achana naye, Mimi Naamini ni ujinga tu wa kutafuta like ambapo hata yeye akikaa na kutafakari, inamuumiza moyo,
Like haziwezi kuleta faraja yoyote Kwa mtu anapoleta nyuzi zinazomsuta hata yeye mwandishi
Mambo ya kufanyia siasa yapo, lakini kuna mengine yanahitaji utu, na akosaye utu juu ya mambo yenye utu, yaletayo simanzi huyo ni wa kupuuza
R.I.P na poleni sana wafiwa wote