Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili

Mara ya kwanza alisukumizwa kuchukua form leo hii amejipeleka mwenyewe kuchukua form.

Urais ni mtamu nyie acheni zile story za eti kazi ni ngumu na sound kibao.
 
Mpaka sasa aliyechukua fomu ni mmoja.

2015 waliochukua walikuwa zaidi ya 20.

Ni matumaini Yangu kina Mwigulu ,Lukuvi ,Lowasa,Sumaye ,Mwakyembe ,na wengineo wengi watachukua ,tunahitaji demokrasia kuweni mfano
Mimi ningekuwa CCM ningechukua form.
 
Sasa ndo nini yani raisi Magufuli amechukua fom ya kugombea Uraisi?
Urais wake unaishia Oktoba 2020 na hivyo kuanzia Novemba 2020 anatakiwa Rais mwingine mpya, na ndiyo maana amechukua form. Ieleweke kuwa mpaka muda huu, Katiba yetu ya JMT inatuambia kuwa hatuna Rais wa kuanzia Novemba 2020 mpaka Oktoba 2025
 
Na alivyokuwa akiulalamikia. Huyu kiongozi wetu! Sijui!
Huwa anasema kazi ni ngumu ila anaipenda, sijawahi kumsikia akisema kuwa haipendi. Yaani ni kama kwenye masomo tu vile kwamba Biology ni ngumu sana, lakini unakuta mtu anaipenda pamoja na ugumu wake huo, kwa sababu anapenda huko mbele ya safari aje awe daktari!
 
ukisikia kujitekenya na kucheka wewe mwenyewe ndio hapo sasa. duniani tunaonekana wajinga sana na umasikini tulio nao basi tunaonekana kama katuni za porini. Katiba zetu za enzi za mkoloni bado zinatupelekesha
 
Waoga sana,zile kelele tu za bungeni
Watu waoga. Hivi hakuna mwana CCM wa kwenda kuchukua form ?Kweli watanzania sio jasiri. Ningekuwa nimefikisha miaka 40.Ningechukua kadi ya CCM leo leo na kwenda kuchukua form.
 
Alisema 2015 alikuwa ana beep. Huyu jamaa mnafiki jamani. Na leo tena anabeep ?Sasa Uraisi umekuwa mrahisi kwake ?
 
Sasa wewe ulitaka achukue form ya kugombea umiss magogoni au?
 
Mnafiki kujidai kazi ngumu eti mzigo lakini anarudi tena
 
Ndio maana ukifanya kitu cha hovyo na usipokuwa serious kwenye ishu fulani unaambiwa 'hebu acha kufanya siasa'.............
hahahahaha aisee ni kweli kabisa....kuna trafki nlimpiga saundi kwa road akaniambia....acha siasa ndugu[emoji1787][emoji1787]
 
Mwingine nani kachukua?
anaweza kuzuga kwa kumwambia Msukuma au kibajaji wale wabunge mbumbumbu vilaza wakachukue na wao ili kuwahadaa watanzania wajue CCM kuna demokrasia
 
Kutafuta ridhaa kwa kutia nia huku hakuna kuhojiwa, kugombea na wenzio ndani ya chama pia kutoongea hata kidogo atafanya nini halafu atapitishwa tena na CCM Mpya.

Utamaduni huu mkongwe , mazoea na desturi hii ni kuuwa na kudumaza demokrasia ngazi ya chama na inapelekea kuleta athari kubwa ngazi ya kitaifa hasahasa kama nchi ina kitu kinachoitwa Chama Dola ndani ya demokrasia ya vyama vingi vya kisiasa nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom