Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili

Kuchukua fomu ni hiari sio lazima ukiona hakuna mwingine kachukua jua ni hiari .CCM tuko kidemokrasia mtu ana hiari ya kuchukua au kutochukua fomu.Hivyo ukiona hakuna aliyechukua zaidi Ya raisi Magufuli ujue wazi kuwa watu wametumia hiari yao kutochukua fomu sio kesi
Unaubariki uwongo? Kakini haishangazi mbona hata data za covid19 umi alisema tz wapo wagonjwa 4, pm akasema wapo 66
 
Pohamba wewe wacha kuchekesha walio nuna, yaani form imechukuliwa moja alafu unasema zilikuwa chache!!! [emoji23][emoji23][emoji23]
Fomu za kugombea Urais zilikuwa chache ba zimeisha leo,
 
Membe anahitaji form
Huo ndiyo ukweli, tena wa heri. Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa Dr. John P. Magufuli leo 'amenyakua' fomu ya 'kuchukua' tena Urais kupitia CCM. Kila mtanzania anajua kuwa tayari Dr. Magufuli 'ameshapitishwa' kimaneno na kivitendo kuwa mgombea Urais wa CCM kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hata TLP ya Mrema imempitisha. Leo hakuchukua fomu ya kuomba kugombea.

Angekuwa amechukua, kama ilivyo kwa watani zetu CHADEMA, basi makada wengine wa CCM wangejitokeza na kuchukua. Wenye sifa za Urais ndani ya CCM wamejaa tele kuliko mchele. Lakini, hakuna mwenye uthubutu hata kiduchu wa kuja hapa Makao Makuu ya CCM Dodoma kuchukua fomu. Ni kama fomu ya kugombea Urais ndani ya CCM ilichapishwa moja tu kwa ajili ya Dr. Magufuli. CCM tumekubali utaratibu umeze matakwa ya Katiba na Kanuni zetu za CCM.

Maneno na matendo ya watoa-fomu yanakataza kusogelea chumba cha kuchukulia fomu. Macho yao yanaogopesha makada kujitokeza na kuomba fomu za Urais. Ilipaswa Dr. Magufuli aanze kupimwa ndani ya chama kuhusu kukubalika kwake. Angepimwa na makada wengine juu ya kwanini yeye apewe bendera ya CCM uchaguzini katika nafasi ya Urais. Angepita au kutopita kidemokrasia. Haipo hivyo. Haikuwa hivyo. Haitakuwa hivyo.

Kwanini tushupalie demokrasia kwa watani zetu (vyama vya upinzani) huku demokrasia chamani mwetu ikiminywa? Nani tunamtapeli ikiwa ukweli ni kuwa hautakiwi upinzani ndani ya CCM kwa nafasi ya Urais?

Uchaguzi huu utaingia kwenye maajabu ya dunia!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma
 
Aliwahi kusema kuwa alibeep tu kwenye urais!
Huyu si alisema kwamba urais kazi ngumu analala na mafaili kibao na angejua ugumu wa kazi hiyo asingeomba,SASA INAKUWAJE AMECHUKUA FORM TENA? Huku Lumumba Je wengine wameruhusiwa kuchukua form? MEMBE NAYE KACHUKUA?
 
Hilo linawzekana kama ndugu zetu wa damu wameweza sisi ni kina nani tushindwe?
Tumeomba sie Wanyonge na baadae tutamlazimisha afumue katiba atawale Muda uliobaki wa maisha yake yote
 
Nasikia pale lumumba amewekwa kipara kipya amepewa jukumu moja tu akimuona Membe anaingia lumumba ampigie simu Bashiru ili akimbie na form
Competition muhimu vipi kuhusu jasusi mbobevu ajaenda kuchukua fomu. Tunamuhitaji alete ushindani Mana yeye peke yake ndio anaye jiamini kuleta upinzani ndani chama. Wengine wanaogopa kukatwa.
 
Back
Top Bottom