Mwezi ujao napata milioni 30. Naomba ushauri namna ya kuzitumia

Mwezi ujao napata milioni 30. Naomba ushauri namna ya kuzitumia

Habari mwezi ujao naenda kupata mil 30 vijana wenzangu naombeni ushauri ili nisije kujuta baadae maana hela saiz sina. Na hiyo ela sizani kama nitaipata tena kama hiyo naombeni ushauri kama ungekuwa wewe ungefanyajee.
Nina mke na watoto 3
Ndugu pesa haifanyiwi bajeti kabla haijaingia mkononi mwako,hiyo sii yako hadi uione.Ushauri wa bure na pesa haitangazwi hiyo ni siri yako na fanya yako.Japo kuomba ushauri wa mawazo sii vibaya.🫠
 
Nunua bodaboda 10 uwape vijana wakuchumie hela, boda moja kwa siku 12,000 tzs kumi ni 120,000.
Kwa mwezi ni 3,600,000 tzs. Yaani utakua na uwezo wa kuongeza boda mpya kila mwezi mpaka uwezo wako wa kuzi control utakaposhindwa.
Hapo unachomesha vinginevyo uwe unaweza kumkabidhi kwa mnyama wa madoa atakaye zingua,vinginevyo chinga wapiga mziki mkubwa Rodini wanakufilisi asubuhi mapeema kabla hapaja kucha🤣
 
Back
Top Bottom