Mwigulu adai wananchi ndio walioshauri tuweke tozo


Kwa hivyo wananchi ndio wakulaumiwa?. Kweli tuna Viongozi wasanii. Ndio ufafanuzi alioisema.
 
Hili jamaa bhana! Bure kabisa. Kwa hiyo yule jamaa yake Zungu ndiyo anawakilisha mawazo ya wananchi wote wa nchi hii!

Sijui ni kwa nini kila anachotamka mdomoni mwake mara zote huwa ni pumba tu.
 
Pia tulisema waongeze wigo wa ajira Watu wawe na vipato.

Watekeleze basi na hilo.
 
Amerogwa huyo
 
Hayo maoni ya wananchi waliyakusanya lini na kwa njia gani?

Aache uongo, hizo tozo zimepitishwa na lile bunge la CCM lisiloweza kuihoji chochote serikali kisha Rais akaweka saini.
Mbunge wako alikuwakilisha
 
Amedanganya!!! Hata kama wananchi walishauri kuongeza wigo wa mapato hawajashauri fedha zao ziibiwe hovyo na kutumika kipumbavu kama vile kuagiza v8 za nusu bilioni!! Mwigulu please give us a break!!!
 
Mwiguluuuu, za kuambiwa changanya na za kwako!! Hao wananchi waliaokushauri na wapi hao?
 
Exactly.

Huu upuuzi unaofanywa na Hawa maccm, hatuwezi kukoma, unless tunakuwa na uchaguzi huru.

Uchaguzi huo huru utapatikana pale tu, nchi itakapopata Katiba mpya ya Rasimu ya Warioba na wala si kwa Katiba pendekezwa ya hao Masisiem
Yaani nchi imejaa viongozi waliojiweka mamlakani ndio maana hawana hofu kwa chochote vyombo vya ulinzi wanachukua orders kutoka kwao ndio maana wanajaa vichwa.
 
Mimi nimemwelewa Mheshimiwa Waziri Mchunga ng'ombe;yaani walijadiliana na Wana-Yanga wenzake(timu ya Wananchi).
 
Labda wananchi wa iramba au Burundi!
Mama yetu SSH mwangalie huyu waziri wako kwa jicho la 3, hakutakii mema kabisa!
 
Ungeweka hata sh 200 tusingestuks na siyo kama ulivyofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…