Mwigulu: Mkataba wa EPC+F ni Technical sana

Mwigulu: Mkataba wa EPC+F ni Technical sana

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
841
Reaction score
909
Waziri wa fedha Msomi Dr Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge kuwa mkataba wa EPC +F ni " Technical" sana kwa wananchi na wabunge kuweza kuelewa.

Akitoa ufafanuzi bungeni baada ya Mbunge Halima Mdee kuzuia shilingi ya mashara wa wàziri wa ujenzi kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa mkataba huo wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya km 2000.

Akijificha nyuma ya neno technical, waziri huuo ambaye anadai ni msomi, amesema watanzania wengi hawawezi kuelewa mkataba huo kwa kuwa ni technical.

Hata alivyotakiwa na Spika Tulia kuueleza kwa lugha rahisi, msomi huyo alianza kutoa mifano ya mikataba ya SGR kuwa ilifuata utaratibu huo.

hata hivyo maelezo hayo hayakuwaridhisha wabunge ambapo mbunge wa Kisesa alisema wabunge wana elewa hizo technicalities tofauti na anavyodai.

Amesema serikali imetoa majibu matatu tofauti kwa suala hilo na kuwataka kuomba radhi kwa kulidanganya bunge pia amemtaka waziri msomi atoe ushahidi kuwa ujenzi wa SGR lot 3 hadi 5 unafanyika chini ya utaratibu wa EPC+F.

Mbunge mwingine alimwambia waziri huyo msomi kuwa watanzania nje ya bunge sio wajinga kama anavyofikiri na kwamba wanauwezo mkubwa wa kuelewa na kuchambua mambo tofauti na anavyofikiri.

Kimbembe hicho kilitokana na mbunge Mdee kukariri maelezo ya CAG kuwa licha ya kusainiwa mkataba wa miradi hiyo utekelezaji wake umekwama.

Akijibu hoja hiyo waziri wa ujenzi, alisema setikali inatauta fedha za utwkelwzaji wake.

Hali hiyo ilisababisha mjadala mkali kwani EPC+F inamtaka mjenzi kutafuta fedha na kujenga barabara ambapo serikali utamlipa mjenzi huyo.

Badala yake serikali imeamua kutafuta fedha za ujenzi wa barabara na baadaye mje huyo atalipwa na serikali.

Spika alihoji sababu za serikali kumtafutia mjenzi fedha na baadaye mjenzi alipwa badala ya kutumia utaratibu wa sasa wa serikali kutangaza tenda na kumpata mkandarasi wa kujenga barabara husika .

Mawaziri watatu walilazikika kutoa ufafanuzi na kudai kuwa riba ya mikopo katika masoko duniani imepanda tofauti na ilivyokuwa wakati wa kuingia mkataba huo, hivyo serikali imechukua hatua ya kutafuta fedha za mradi huo ili mkandarasi aendelee.

Akihitimisha Mbunge Mdee alitaka setikali kufuta kifungu kinachoeleza mkataba huo kutoka katika hotuba ya bajeti na kuweka kifungu kinachoeleza hali halisi
 
Waambie wabunge ,watu waliobaki kwenye kazi za kutojali elimi ni waoa tuu ,yani kujua kusoma na kuandika ilihalia mimi mtu mdogo sana ata yaya wangu lazima awe amefika form four na awe na ujuzi wa sayansi ya chakula .
Mkuu
Ni kweli kwamba shule ni muhimu sana kwao, lakini hata kama hukusoma huqwzi kutumia akili ya kawaida kufahamu hapa nimepigwa au niko sawa?

Kingine ukiangalia wabunge waliopo utabaini kuwa wamekwenda shule, ingawa kuna kusoma na kuelimika.

Ninachokiona kinachotafuna taifa hili ni ubinafsi wa jao wanaoitwa viongozi wanaofikiri watanzania wa leo hawajui mambi technical.
 
Ukisema technical maybe before digital/smart devices hazijafika tz si kwa tz hii ya sasa ,hata ambao hawajasomea Sheria wanaweza elewa what does it mean in short nchi inapigwa and they know it ila kwakua ni sehemu za wakubwa wanakua hawana nguvu
 
Ukisema technical maybe before digital/smart devices hazijafika tz si kwa tz hii ya sasa ,hata ambao hawajasomea Sheria wanaweza elewa what does it mean in short nchi inapigwa and they know it ila kwakua ni sehemu za wakubwa wanakua hawana nguvu
Wanazipia kwelikweli, wakifikiri watanzania hawaoni au hawaelewi ndio maana katika hotuba yake ya kwanza ya bajeti kama waziri wa fedha alisema seerikali inaachana na utaratibu wa kununua magari kwa baadhi ya kada na badala yake wanaotaka watakopeshwa na kuyahudumia wao.

Leo hii kila wizara na idara zinashindana kununua magari technical ambayo wananchi hawayaelewi.
 
Duh! Masikini nchi yangu...
Nchi yako ina mambo technical sana ambayo wewe huwezi kuyaelewa.

Ukitaka kuyaelewa jiunge nao na wewe ufahamu mamno technical ya serikali kukopa fedha na kuipa kampuni tena ya kigeni ijenge barabara na baadaye serikali ilipe mkopo na kampuni wakati Kuna TANROADS, TARURA nk.
 
Mwigulu Bwege sana...hajui kwamba Kazi ya msomi kama anavyojitanabisha yeye ni kuchakata mambo magumu/technical yawe rahisi kwa mtu mwenye akili ya kawaida kuelewa...if a PhD holder can not comprehend that...we are doomed.
 
Huko kwenye EPC+F ni kwenda kujitafutia matatizo tu. Sio tu kwamba bank zina riba kubwa na middleman juu apate faida hapo hapo making the whole thing too expensive.

Majibu nayo ya waziri don’t make sense anaulizwa ume sign vipi mkataba halafu leo hujui interest za madeni au zimebadilika vipi.

Kwa kusikiliza ule mjadala hakukuwa na full contract agreements, isipokuwa MoU tu, huko kwenye ku-negotiate terms wamekuja baini ala kumbe hizo interest zenyewe ni balaa.

Sidhani kama utapata mkopo wa bank wa muda mrefu hasa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine ambao utakuwa na riba ya 4% kama waziri anavyotaka hizo ni hadithi za Ali Nacha hiko kitu ni impossible.

Kuelezea jinsi interest zinavyopangwa huko sasa ndio technical kuna maswala ya currency risk (inflation), transaction risks, economic risk na managing hizo risk huko utakutana na hadithi za; money market hedge, currency future hedges, currency option hedges, swaps, Forward Exchange contracts, to name a few.

Kama kuna currency risk, there must be interest risk na kwenye kuna mbinu za ku-manage risks huko na kuna hadithi za forward rate agreements, interest rate futures, interest rate options, interest rate (caps, floors and collars), interest rate swaps.

It can get very technical kwenye kupata hiyo mikopo na kukubaliana riba (you can’t get a fixed rate on long term loans) hasa mikopo ya muda mrefu jumlisha na middle man nae apate faida humo humo; it was a bad idea kwa ujenzi wa barabara.
 
Back
Top Bottom