johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 841
- 909
Waziri wa fedha Msomi Dr Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge kuwa mkataba wa EPC +F ni " Technical" sana kwa wananchi na wabunge kuweza kuelewa.
Akitoa ufafanuzi bungeni baada ya Mbunge Halima Mdee kuzuia shilingi ya mashara wa wàziri wa ujenzi kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa mkataba huo wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya km 2000.
Akijificha nyuma ya neno technical, waziri huuo ambaye anadai ni msomi, amesema watanzania wengi hawawezi kuelewa mkataba huo kwa kuwa ni technical.
Hata alivyotakiwa na Spika Tulia kuueleza kwa lugha rahisi, msomi huyo alianza kutoa mifano ya mikataba ya SGR kuwa ilifuata utaratibu huo.
hata hivyo maelezo hayo hayakuwaridhisha wabunge ambapo mbunge wa Kisesa alisema wabunge wana elewa hizo technicalities tofauti na anavyodai.
Amesema serikali imetoa majibu matatu tofauti kwa suala hilo na kuwataka kuomba radhi kwa kulidanganya bunge pia amemtaka waziri msomi atoe ushahidi kuwa ujenzi wa SGR lot 3 hadi 5 unafanyika chini ya utaratibu wa EPC+F.
Mbunge mwingine alimwambia waziri huyo msomi kuwa watanzania nje ya bunge sio wajinga kama anavyofikiri na kwamba wanauwezo mkubwa wa kuelewa na kuchambua mambo tofauti na anavyofikiri.
Kimbembe hicho kilitokana na mbunge Mdee kukariri maelezo ya CAG kuwa licha ya kusainiwa mkataba wa miradi hiyo utekelezaji wake umekwama.
Akijibu hoja hiyo waziri wa ujenzi, alisema setikali inatauta fedha za utwkelwzaji wake.
Hali hiyo ilisababisha mjadala mkali kwani EPC+F inamtaka mjenzi kutafuta fedha na kujenga barabara ambapo serikali utamlipa mjenzi huyo.
Badala yake serikali imeamua kutafuta fedha za ujenzi wa barabara na baadaye mje huyo atalipwa na serikali.
Spika alihoji sababu za serikali kumtafutia mjenzi fedha na baadaye mjenzi alipwa badala ya kutumia utaratibu wa sasa wa serikali kutangaza tenda na kumpata mkandarasi wa kujenga barabara husika .
Mawaziri watatu walilazikika kutoa ufafanuzi na kudai kuwa riba ya mikopo katika masoko duniani imepanda tofauti na ilivyokuwa wakati wa kuingia mkataba huo, hivyo serikali imechukua hatua ya kutafuta fedha za mradi huo ili mkandarasi aendelee.
Akihitimisha Mbunge Mdee alitaka setikali kufuta kifungu kinachoeleza mkataba huo kutoka katika hotuba ya bajeti na kuweka kifungu kinachoeleza hali halisi