Mwigulu Nchemba ang'aka kuagiza mabasi 60, asema hana biashara hata ya bajaji

Mwigulu Nchemba ang'aka kuagiza mabasi 60, asema hana biashara hata ya bajaji

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amefadhaishwa kuambiwa ameagiza mabasi 60, amedai hana hata biashara bajaj. Mwigulu amesema hakuna haja ya kuchafuana.

Dokezo - Waziri aagiza mabasi 60, Kampuni ya Esther

=====

Mwigulu Nchemba: Imekuja tozo, mtu anasema ona waziri huyu ameagiza mabasi 60 kwenye kampuni yake, mimi sina kampuni hata ya bajaj. Hivi unaweza ukatoka chuo tu ukawa na bweni la wasichana na wavulana la kusaidia halafu uwe na kampuni ya biashara, sina biashara hata ya bajaji.

Kisa tozo, hii ni dhamana tu, hatuna haja ya kuchafuana. Unahangaika kuchafua mtu.

 
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema ameishi na kusoma kwenye mazingira magumu hivyo kama binadamu, yeye pia hapendi kutoza kodi kwa watu wengine.

Hata hivyo ni lazima kwa kila aliye na sifa ya kulipa kodi na tozo afanye hivyo kwa kuwa nchi haijengwi na Rais bali na wananchi wenyewe.

Ameomba kila mtu mwenye maoni au ushauri afike ofisini kwake kwa majadiliano, au anaweza kuandika popote na Serikali itaona na kusikia.

Akizungumzia shutuma zinazoendelea mtandaoni kuhusu yeye kuagiza mabasi 60 huku akiwapa watanzania mzigo mkubwa wa kodi na tozo, Mh. Waziri amesema kuwa yeye hana hata basi moja pia hamiliki hata kampuni yenye bajaji moja.
 
Kumekuwa na uongo mwingi sana kwa viongozi wetu, na hapa Kuna watu huusika kuwachafua kwa maslahi yao.

Mwigulu anasema hamiliki hata kampuni ya bajaji, ilaa anashangaa kuhusishwa na kumiliki kampuni ya mabasi.

Tuache kuwasingizia uongo hawa viongozi. Kama huna ushahidi ni bora ukakaa kimya.

Hawa wanaosema Waziri Mwigulu anamiliki mabasi ndio haohao walisema Lowassa anamiliki kampuni ya Richmond, Ila mwisho wa siku ndio haohao wakageuka na kuanza kumsafisha huku wakizungusha mikono
 
Back
Top Bottom