Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

Kama kawaida ya kusahau. Tumeanza tena kudai punguzo la bei ya mafuta wakati tulishambiwa kuhamia Burundi.
 
Wananchi tunahitaji kujua kama Kauli ya Waziri wa fedha Bwn. Mwigulu kwa wananchi wanaolalamikia makali ya tozo kuwa kama wanahisi wanaonewa wahamie Burundi ni ya serikali au ya kwake binafsi.

Tunataka kufahamu hivyo ili tuweke rekodi zetu sawa.

Kwakua Waziri ni sehemu ya Serikali na anaingia kwenye vikao vya baraza la mawaziri.

Kama baraza zima lilibariki tozo basi pia limebariki na kauli hii ya kuhamia Burundi.

Maana kama hukubaliani na tozo basi unapaswa kuhamia Burundi na wananchi wengi tu hawakubaliani nazo.

Serikali itufafanulie kuhusiana na hili jambo ili ukweli ufahamike maana kauli ya serikali ni amri kwa wananchi.
 
Hamia burundi na wewe.

Hawa kina Mwigulu mliwatengeneza nyie wenyewe.

Sasa chatu mlilofuga.......
 
Huyu jamaa kama vile yuko juu ya kila kitu/mtu.

Dharau imezaliwa pale, jeuri! Majivuno! Kejeli! Kiburi! Kujisikia! Kujiona ana akili sana!!
Ofcourse ana akili na yuko juu sana. Kumbuka ameshakuwa naibu waziri wa fedha, mambo ya ndani na sasa ni Waziri kamili na ana PhD.
 
Kuwa na PHD sio justification ya kukejeli wananchi.

Rais alisema kabisa hataki kiongozi anayepandisha mabega.

Ila wateule wake wanapandisha mabega na hawafanyi chochote.

Au ile kauli ilikua mahususi kwa ajili ya kuondokana na watu flani flani.
 
Kuna tatizo mahala, hii tabia ya hawa jamaa kila wakiulizwa maswali na wanachi wanatoa majibu ya kejeli naona inazidi kushika kasi.

Nimeanza kuhisi inawezekana hawa watatu Nape, Mwigulu, na Makamba wameshajiona wao ni "untouchables" wanaoonewa wivu na kila anayewauliza maswali, hivyo kwa pamoja wameamua kuja na majibu ya kejeli ili kuwakomesha.

- Makamba alipoulizwa kuhusu mradinwa Nyerere Dam kule bungeni na mbunge mwenzie alijibu tatizo ni uwaziri wake, alipoendelea kuulizwa nje ya bunge akasema; "kama hamuelewi mniue" hii ilikuwa kauli ya kijanja kuficha udhaifu wake wa kiutendaji ili aonekane anaonewa na wanaomuuliza.

- Mwigulu nae kila akiulizwa kuhusu tozo anasema kama zimewashinda kulipa hamieni Burundi, tena huyu amerudia kauli hii mara mbili; haya ni majibu ya dharau 100% kwa wale wanaoongozwa.

- Nape nae ndio kila siku anaropoka mitandaoni maneno ya kashfa hasa akiulizwa kuhusu upandaji wa gharama za data, yeye anakuja na majedwali ya kupika kutuonesha gharama za data zimeshuka toka awamu hii iingie madarakani, wakati kiuhalisia gharama za data ndio zimepanda mara mbili.

Hawa mawaziri watatu ni kama vile wamejitengenezea kakikundi chao, sasa wanamtengeneza kisaikolojia na Rais aone wao ndio wanaoonewa wakati waziri kuulizwa maswali na kujibu ni wajibu wake, Rais asipowakemea hawa, lazima watamharibia.
 
Mimi naliona jambo hili kwa mtazamo tofauti kidogo, binafsi naona tatizo liko pale juu kwenye ushungi. Hebu tufikirie kwa pamoja,

kwamba tulitegemea nini kwa kauli za, "Hili nalo mkalitizameni" "jinsia yangu hainiruhuru kukalipia watu" na kauli kama "kuleni urefu wa kamba" ukitulia utagundua mama ni bora liende. Kila mtu ajiamulie anavyotaka.

Na majamaa kweli wanajiamulia mambo kadri yatakavyowanufaisha mfano tu majuzi huyo huyo Mwigulu kajinunulia gari la 800 million. Sasa bila kuongeza matozo watawezaje kutumbua maraha na kuogelea kwenye anasa "wanazovimbiwa" nazo kwa sasa kisha wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa "anaupiga mwingi" na yeye likichwa linavimba
 
Wananchi tunahitaji kujua kama Kauli ya Waziri wa fedha Bwn. Mwigulu kwa wananchi wanaolalamikia makali ya tozo kuwa kama wanahisi wanaonewa wahamie Burundi ni ya serikali au ya kwake binafsi.

Tunataka kufahamu hivyo ili tuweke rekodi zetu sawa.

Kwakua Waziri ni sehemu ya Serikali na anaingia kwenye vikao vya baraza la mawaziri.

Kama baraza zima lilibariki tozo basi pia limebariki na kauli hii ya kuhamia Burundi.

Maana kama hukubaliani na tozo basi unapaswa kuhamia Burundi na wananchi wengi tu hawakubaliani nazo.

Serikali itufafanulie kuhusiana na hili jambo ili ukweli ufahamike maana kauli ya serikali ni amri kwa wananchi.

Hii ni kauli rasmi ya serekali na ukiendelea kuhoji tunakuhamisha mara moja.
 
Ndio i
Kuwa na PHD sio justification ya kukejeli wananchi.

Rais alisema kabisa hataki kiongozi anayepandisha mabega.

Ila wateule wake wanapandisha mabega na hawafanyi chochote.

Au ile kauli ilikua mahususi kwa ajili ya kuondokana na watu flani flani.
Ilikuwa kwa ajili ya team jiwe a.k.a mpora uchaguzi
 
Mimi naliona jambo hili kwa mtazamo tofauti kidogo, binafsi naona tatizo liko pale juu kwenye ushungi. Hebu tufikirie kwa pamoja,

kwamba tulitegemea nini kwa kauli za, "Hili nalo mkalitizameni" "jinsia yangu hainiruhuru kukalipia watu" na kauli kama "kuleni urefu wa kamba" ukitulia utagundua mama ni bora liende. Kila mtu ajiamulie anavyotaka.

Na majamaa kweli wanajiamulia mambo kadri yatakavyowanufaisha mfano tu majuzi huyo huyo Mwigulu kajinunulia gari la 800 million. Sasa bila kuongeza matozo watawezaje kutumbua maraha na kuogelea kwenye anasa "wanazovimbiwa" nazo kwa sasa kisha wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa "anaupiga mwingi" na yeye likichwa linavimba
Pale nasemaga hum, HATUNA Rais pale, ila kila Jambo hutokea KWa makusudi, na ili kusudi litimie lazima Jambo liwepo
 
Back
Top Bottom