Mwigulu Nchemba: Hakuna mwananchi atakayelipa mkopo, Serikali italipa

Kodi ndio italipa madeni asidanganye watu,
Wakiona yamekuwa mengi watatafuta pa kupachika kodi.
 
Haya mambo ndo ilitakiwa wabunge wetu wayajadili bungeni.ila ndo hivyo tena.
 
Hivi huyu #Mwigulu Nchemba ana akili timamu kweli?
Anaposema serikali italipa anakua na maana Gani,Ina maana kumbe serikali ni genge la Watu wachache waliohodhi rasilimali za hili taifa na wanafanya mambo Kwa matakwa Yao binafsi au Sio,
Hii kauli mbaya Sana na inaonesha dharau kubwa kutoka Kwa huyu bwana mbele za wananchi,
iseee nimejikuta na hasira Sana Aisee Hivi Hawa Watu wanatuona Watanzania mazuzu Sana kumbe,
Hio mizigo ya madeni inatufanya tushindwe kuendelea Ili Hali tuna rasilimali chungu mzima,
We are fighting for nothing since 1961 Bado tunakopa fedha za kujengea matundu ya vyoo
Shame!
 
Dah DR inakuwaje tena uchumi wa wapi huu mlipa deni ni mwananchi kupitia kodi za kila siku.
Zinatumika zaidi ya 800bil toka kwenye kodi yetu kulipa madeni sasa unasemaje kuwa mwananchi hatawajibika kulipa deni.
Uchumi wa wapi huu jamani?

Hawa ndio wenye Ph.D za mchongo; serikali inapata fedha zake toka kodi/tozo za wananchi ndio inalipa madeni. Itakuwaje tena huyu punguani anakuja na kuharisha kuwa madeni hayatalipwa na wananchi bali na serikali!!!! Inasikitisha sana pale nchi yenye wasoni wenye weledi wakiongozwa na watu wasiokuwa na weledi!!
Mama Samia chonde chonde mtoe huyu nanga hapo kwenye KIBUBU chetu na hapo umuweke huyo mama uliyempeleka Wizara ya ULINZI; hautajuta na utalala usingizi mzuri usio kuwa na unnecessary stress!
 
Ni kweli kwamba mwananchi hatadaiwa yeye binafsi.
Hata hivyo, serikali ya wananchi italazimika kulipa na hivyo kutumia pesa ambazo ingezitumia kwa ajili ya huduma kwa wananchi. Hii Ina maana kwamba wananchi watalipa kwa kukosa huduma ambayo serikali haitawaeza kuitoa wa sababu ya kulipa madeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…