Mwigulu Nchemba: Hakuna mwananchi atakayelipa mkopo, Serikali italipa

Mwigulu Nchemba: Hakuna mwananchi atakayelipa mkopo, Serikali italipa

Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Lameck Nchemba (PhD) leo amewaondoa wasiwasi wananchi wanaolia kwa sababu ya ukubwa wa deni la taifa (Trilion 70+) kwamba hakuna mtanzania hata mmoja atakayegongewa mlango au kutakiwa kutoa mali zake binafsi ili kulipia deni la taifa. Amesema deni hilo litalipwa na serikali yenyewe kwa fedha zake bila mwananchi yeyote kutakiwa kutoa hata senti moja ili kulipia deni. Msikilize wewe mwenyewe kwenye klipu hii hapo chini 👇 👇 👇 👇 👇
View attachment 2068601
Dr Mwigulu alisema hayo wakati Rais Samia alipokuwa akihutubia Baraza la Mawaziri ikulu Jijini Dodoma ili kuweka mambo sawa baada ya Spika wa Bunge kuwa mbogo kuhusiana na ukubwa wa deni la taifa ambapo Spika alisema kuwa serikali ya Samia isipokuwa makini kwenye ukopaji, ipo siku nchi hii itauzwa kwa sababu ya ukubwa wa madeni.

MAONI YANGU
Nawaomba wananchi tutulie, tuache kupapalika bila sababu kwa kuwa sasa tumehakikishiwa kwamba hatutahusika hata chembe kwenye ulipaji wa deni la taifa. Nawashangaa sana watu wanaowapotosha wananchi kwa makusudi kuwa watahusika kwenye ulipaji wa deni la taifa huku wakijua fika kwamba serikali itajilipia yenyewe deni lake. Tuache upotoshaji ndugu watanzania. Kuna makundi ya watu wabaya wanaotumia na watu wasioitakia mema nchi hii kuifarakanisha serikali na wananchi wake. Tuwe makini! ✍️
Kodi ndio italipa madeni asidanganye watu,
Wakiona yamekuwa mengi watatafuta pa kupachika kodi.
 
Kweli kabisa mkuu. Hata MwanaHalisi Online imeandika pia. Swali la Msingi. Tozo ni kodi mpya ya Simu. Wizara ya Fedha siyo ya Muungano. Watu mil1 wa Zenj watozwe zao. Na sisi mil 60 tutozwe kwa maendeleo yetu. Ratio ni ileile. Why pesa za Bara ziende Zanzibar?

Walikomaa Zanzibar ikope kama nchi. Wameruhusiwa tiyar. Ni kwa nn pesa za Tanganyika Ziende Zanzibar?
Haya mambo ndo ilitakiwa wabunge wetu wayajadili bungeni.ila ndo hivyo tena.
 
Hivi huyu #Mwigulu Nchemba ana akili timamu kweli?
Anaposema serikali italipa anakua na maana Gani,Ina maana kumbe serikali ni genge la Watu wachache waliohodhi rasilimali za hili taifa na wanafanya mambo Kwa matakwa Yao binafsi au Sio,
Hii kauli mbaya Sana na inaonesha dharau kubwa kutoka Kwa huyu bwana mbele za wananchi,
iseee nimejikuta na hasira Sana Aisee Hivi Hawa Watu wanatuona Watanzania mazuzu Sana kumbe,
Hio mizigo ya madeni inatufanya tushindwe kuendelea Ili Hali tuna rasilimali chungu mzima,
We are fighting for nothing since 1961 Bado tunakopa fedha za kujengea matundu ya vyoo
Shame!
 
Dah DR inakuwaje tena uchumi wa wapi huu mlipa deni ni mwananchi kupitia kodi za kila siku.
Zinatumika zaidi ya 800bil toka kwenye kodi yetu kulipa madeni sasa unasemaje kuwa mwananchi hatawajibika kulipa deni.
Uchumi wa wapi huu jamani?

Hawa ndio wenye Ph.D za mchongo; serikali inapata fedha zake toka kodi/tozo za wananchi ndio inalipa madeni. Itakuwaje tena huyu punguani anakuja na kuharisha kuwa madeni hayatalipwa na wananchi bali na serikali!!!! Inasikitisha sana pale nchi yenye wasoni wenye weledi wakiongozwa na watu wasiokuwa na weledi!!
Mama Samia chonde chonde mtoe huyu nanga hapo kwenye KIBUBU chetu na hapo umuweke huyo mama uliyempeleka Wizara ya ULINZI; hautajuta na utalala usingizi mzuri usio kuwa na unnecessary stress!
 
Ni kweli kwamba mwananchi hatadaiwa yeye binafsi.
Hata hivyo, serikali ya wananchi italazimika kulipa na hivyo kutumia pesa ambazo ingezitumia kwa ajili ya huduma kwa wananchi. Hii Ina maana kwamba wananchi watalipa kwa kukosa huduma ambayo serikali haitawaeza kuitoa wa sababu ya kulipa madeni.
 
Back
Top Bottom