Mwigulu Nchemba: Hakuna mwananchi atakayelipa mkopo, Serikali italipa

Ama kweli hizi phd za mawaziri wetu naanza kukubaliana na wanaozitilia mashaka. Mchumi mzamivu kama anasema serikali ndiyo inalipa madeni na si wananchi hii inaleta ukakasi si kidogo. So kodi za wananchi zinaenda wapi? Tozo za wananchi zinaenda wapi? Masurufu ya wananchi yanaenda wapi? Serikali yenyewe hizo hela za kulipa inazichimba shimo gani? Hayo labda alikuwa anawaambia wanyaturu wenzie ws Kiomboi vijijini wasiojua hata kodi ni nini na kuwa labda serikali ni dudu linalotema hela.
 
Dah DR inakuwaje tena uchumi wa wapi huu mlipa deni ni mwananchi kupitia kodi za kila siku.
Zinatumika zaidi ya 800bil toka kwenye kodi yetu kulipa madeni sasa unasemaje kuwa mwananchi hatawajibika kulipa deni.
Uchumi wa wapi huu jamani?
Mkuu iamini serikali; hakuna mwananchi atakayeombwa fedha ya kulipa deni la taifa. Serikali italipa. Full stop.
 
Dah DR inakuwaje tena uchumi wa wapi huu mlipa deni ni mwananchi kupitia kodi za kila siku.
Zinatumika zaidi ya 800bil toka kwenye kodi yetu kulipa madeni sasa unasemaje kuwa mwananchi hatawajibika kulipa deni.
Uchumi wa wapi huu jamani?
Anamaanisha hakuna pesa ya ziada itakayowekwa kwa mwananchi kwa ajili ya kulipa mkopo zaidi ya makusanyo ya tozo na kodi zilizopo, misaada na michango. Kwa ufupi mapato ya serikali.
 
Zanzibar haina mapato ya kutosha kujiendesha kama nchi. Kwa kuwa sote tunajenga nchi moja, sio vibaya pesa kukamuliwa kutoka Tanganyika na kuwapelekea wazaznzibar ili nao wajikwamue kiuchumi. Nao ni wenzetu, tusiwatenge.
 
Kwa sheria ipi?
 
Anaposema serkali italipa anamaanisha nini?
1. Kwamba Tozo si za wananchi
2. Kuwa kodi ya mwananchi
3. Kwamba maliasili si za wananchi
Hivi Serkali ina mapato tofauti na wananchi na maliasili zao?

Huyu ni Phd holder
Shida ya mtu aliyetokea kijijini akachunga ng'ombe akasoma akapata cheo huwa anakuwa limbukeni wanajidai Sana Mana hakutegemea ni sawa mtu Aliye win jackpot atasumbua mtaa mzima tumjue.
Basi Kama vipi Kodi zetu zitufanye Mambo yetu ya kijamii afu tuone hiyo serikali watoe hela zao
 
Wamekariri tu madesa akatapika kwa exam akafaulu basi. Amefanya Nini Cha kusaidia Taifa lake ama Kijiji chake kuwa ni msomi
 
Kwa sheria ipi?
Rais mwenyewe ni SHERIA; lolote analoamua kwa manufaa ya nchi halipaswi kupingwa na mtu yeyote. Hata Mwendazake aliamua kujenga reli bila kumshirikisha mtu yeyote na hakuna aliyehoji. Sasa hivi watu wanahoji kwa kuwa wanamdharau Rais Samia kwa sababu ni mwanamke.
 
Maana ya kuwa na Sera, sheria na Katiba ni ipi?
 
Huu muungano hutakuja kuitoa CCM madarakani au utaleta mpasuko. Maana naona mama yupo busy na zanzibar yake.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Madeni yote ya Tanzania tunalipa sisi wananchi kupitia kodi. Mwigulu ni muongo anapaswa kushitakiwa kwa kupotosha. Waache kukusanya kodi basi kama wananchi hatulipi kodi.
 
Maana ya kuwa na Sera, sheria na Katiba ni ipi?
Rais akiona nchi haiendi anayo mamlaka ya kutupa sheria na sera pembeni na kutawala kwa sheria zake binafsi. Na kumbuka Rais ni kama Mungu; huwa hahojiwi na mtu yeyote. Mbona Mwendazake alikuwa anatawala kwa sheria zake binafsi mlikuwa hamseni? Kwanini sasa?
 
Ndugu yangu una akili kichwani kweli??? Madeni yote ya Tanzania tunalipa sisi wananchi kupitia kodi. Mwigulu ni muongo anapaswa kushitakiwa kwa kupotosha. Waache kukusanya kodi basi kama wananchi hatulipi kodi.
Haya sio maneno yangu mkuu; ni maneno ya Mwigulu Nchemba . Hebu msikilize kwenye klipu hapo juu.
 
Huu muungano hutakuja kuitoa CCM madarakani au utaleta mpasuko. Maana naona mama yupo busy na zanzibar yake.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Kama anaipenda Zanzibar. Akawanie Urais Zanzibar. Mambo ya kuchukua pesa za Bara na kupeleka Zanzibar hatutaki! Watu mil 2 vs mil 60+
 
Una bwabwaja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…