Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Lameck Nchemba (PhD) leo amewaondoa wasiwasi wananchi wanaolia kwa sababu ya ukubwa wa deni la taifa (Trilion 70+) kwamba hakuna mtanzania hata mmoja atakayegongewa mlango au kutakiwa kutoa mali zake binafsi ili kulipia deni la taifa. Amesema deni hilo litalipwa na serikali yenyewe kwa fedha zake bila mwananchi yeyote kutakiwa kutoa hata senti moja ili kulipia deni. Msikilize wewe mwenyewe kwenye klipu hii hapo chini [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
View attachment 2068601
Dr Mwigulu alisema hayo wakati Rais Samia alipokuwa akihutubia Baraza la Mawaziri ikulu Jijini Dodoma ili kuweka mambo sawa baada ya Spika wa Bunge kuwa mbogo kuhusiana na ukubwa wa deni la taifa ambapo Spika alisema kuwa serikali ya Samia isipokuwa makini kwenye ukopaji, ipo siku nchi hii itauzwa ili zipatikane fedha za kulipia madeni.
MAONI YANGU
Nawaomba wananchi tutulie, tuache kupapalika bila sababu kwa kuwa sasa tumehakikishiwa kwamba hatutahusika hata chembe kwenye ulipaji wa deni la taifa. Nawashangaa sana watu wanaowapotosha wananchi kwa makusudi kuwa watahusika kwenye ulipaji wa deni la taifa huku wakijua fika kwamba serikali itajilipia yenyewe deni lake. Tuache upotoshaji ndugu watanzania. Kuna makundi ya watu wabaya wanaotumiwa na watu wasioitakia mema nchi hii kuifarakanisha serikali na wananchi wake. Tuwe makini! [emoji3578]