Elections 2015 Mwigulu Nchemba: Huu Unyama Una baraka zote za Dr. Slaa na genge lake

Duh!!!! Kinachonisikitisha huyo mwenye kitambi ni mtu mzima na heshima zake anakubali kudhalilishwa mbele za watu kisa siasa, wale wanaosema kuwa mwana CCM na kuishabikia lazima uwe na akili za maiti hawakukosea
 
Mwigulu atuwekee ushahidi wa kuonyesha kwamba ni CDM waliwafanya hivyo na siyo yeye mwenyewe ili apate vifaa vya kufanyia kazi,Mwangosi na wale wahanga wa bomu kule Arusha si nao tuliaminishwa kwamba ni CDM,nani anaweza kuwa anajihujumu mwenyewe kwa kupiga bomu kwenye mikutano yake mwenyewe,
Mytake: si ajabu chemba anawaonya wanakalenga kwamba anaouwezo wa kuwafanya wanakalenga kama hawa mnaowaona endapo watahudhuria kampeni za wapinzani.Kazi kwenu wana kalenga kupima mbichi na mbivu.
 
Michango yenu inaonyesha ni jinsi gani mnafurahia binadamu wenzenu kuwa vilema au kufa huo ndio ushindi wenu bila shaka kwa taharifa yenu hamtapata madaraka nchi hii kwa style hiyo shame cdm.

Kwa nini hawakamatwi?
 
Kuwa msukule ni dhambi kubwa sana.Hawa watu wamefanywa kuwa misukule na CCM bila wao kujitambua.Wanadhalilishwa hadharani lakini wao hawajitambui kuwa wanadhalilishwa kwa sababu wameshakuwa mandondocha tayari yakuwaletea kura CCM.
 
Hapo sasa ndio huwa nabaki hoi na nchi hii. Huyo ni msomi tena mchumi wa daraja la kwanza sijui nini, hana ubunifu kabisa kila siku amebaki kama bibi yangu kutumia mbinu zile zile za kizamani. Yaani Mwigulu kila kampeni anapanda na mtu yuleyule anamwaga sera, sasa sijui ni sera gani za mtu aliyeumizwa ambazo zitamkomboa mwananchi. Anaweza kujitetea kwamba anataka kuwaonyesha wananchi jinsi cdm walivyowabaya ni kweli. Ila miaka yote na mtu huyo huyo wakati hasemi sababu zinazosababisha umeme upande bei kiasi hiki. Sitaki kuamini kwamba wasomi ndio hao hawana ubunifu kiasi hiki.
Ila ni kosa letu watanzania tumezoea kuchagua viongozi kwa mazoea, na hatuna muda wa kuwauliza maswali magumu na wenyewe hawataki maswali magumu bali wanataka kura zetu kwa kutujia na watu waliojeruhiwa. Kama kweli ana uchungu na hao watu waliumizwa mbona hajaenda na Dr. Ulimboka anayesema anamjua mpaka aliyemteka? Nazidi kuwadharau wasomi wa nchi hii.
 
Mm hata waliomwua Daudi Mwangosi (r.i.p) walikuwa CDM pia ? Nadhani kama si hasa zimewashinda, msitafute visingizio!:music:
 
Chadema ni sawa na Alshabaab tu. Viongozi wao wanatumia maisha ya watu kama mtaji wa siasa
Lukosi jana ulisema bora Wazanzibar wajitenge leo unasema CDM kuna Alshabaab ngoja sasa Wazanzibar wajitenge halafu uone Alshabaab wa ukweli unaowalilia.
 
Bwana Mwigulu Nchemba,hii albamu yako imeshabuma.Unachotakiwa ni kutoa 'single' au albamu nyingine tu.Kwa hii,haiuziki tena.Kama umeishiwa sera si useme ufundishwe nyingine??
Mwigulu ni --------, hii ni ile tomato source aliyo peleka Arusha Sombetini na kuwashauri Ccm wajipake na kujifunga vitambaa ili wadanganye wamepigwa na Chadema, issue ikashtukiwa. Kama ni kweli wamepigwa waonyeshe pf3 na hospitali waliyopata matibabu. Ccm imeufa, kla siku kuhubiri mapigano tuu badala ya sera.
 
Last edited by a moderator:
Chadema ni sawa na Alshabaab tu.

Viongozi wao wanatumia maisha ya watu kama mtaji wa siasa

Tanzania ni nchi inayozingatia utawala wa sheria na muhimili wa mahakama umepewa jukumu la kusimamia nguzo hii...

Kama kweli hao watu wana uhakika wametendewa kadhia yoyote na Chadema aua wafuasi wa Chadema, kwa nini Mwigulu asifungue kesi ya jinai mahakamani?

Hiki anachokofanya ni kiini macho kwa kuwa Watanzania wa huko vijijini ni maamuma wasioelewa A wala Z ya siasa za Tanzania.

Na watu hawa ndio wamekuwa mtaji wa siasa za ukandamizaji za CCM...
 

Majeraha mtaji siku hizi mkuu,,,,, hawa jamaa watakuwa hawana ajira hata ya kujiajire aisee
 

Polissm wana akili za mbwa. Ni wale wa kuambiwa, shika! Nayo ndio yanakimbilia hata bila kujiuliza. Ndio maana Mwigulu anayafanya Midoli yake.
 
Aiseee Chadema watamaliza watu kwa uroho wa kwenda ikulu.
Dr.W.Slaa ni kweli haya yana baraka zako?
Hebu thibitisha kama hakuna baraka zako kwenye haya.

Kwakweli ni bora CCm hitawale milele kuliko chadema kwenda ikulu.

Bila shaka Kigaila ataleta mikwara ya kutoa siku tatu Mwigulu athibitishe lasivyo watafungua case alaf baada ya hapo kimya kama hile ya kumpa siku tatu Rais.
 
Last edited by a moderator:
Haingii akilini watu wazima kufanywa maonyesho namna hii si udhalilishaji huu. Huyo wanaemtuhumu kufanya hayo kwanini hawamshitaki na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
 

DR SLAA aache YA MAANA AJE KUTHIBITISHA UJINGA HUU ?
 
Last edited by a moderator:

CDM kwa nini haitaki kumpeleka Mwingulu Nchemba mahakamani kwa matamshi haya? Kwa nini wakae kimya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…