Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi hajui kuwa anaingilia kesi iliyokomaa mahakamani kule Igunga ya Tindikali? Mbona ana dharau mahakama?
Sikufikiria kama unaweza kuwa mpuuzi kiasi hicho,hata watu machozi hayajakauka ya Mwangosi wewe leo unakuja na ngonjera za kijinga kiasi hicho nimekudharau sana na sidhani kama una familia wewe,na hata kama unayo basi mwanao ana akili kushinda wewe mbulula.Kwa kweli mwigulu nchemba ameongea kweli hawa chadema wanataka tuwe kama wasomalia kila siku vita,tunashukuru watanzania wanaelewa umuhimu wa aman yetu na hawapo tayari kuiingiza nchi kwenye dimbwi la damu.Tunatamani upinzani ila sio chagadema.
kuna mambo ya msingi ambayo mtanzania makini anatakiwa kujiuliza kuhusu hii picha ya Mwigulu Nchemba anayo endelea nayo.
1. Aliyekuwa mgombea wa CHADEMA kata ya Ubagwe wilaya ya Ushetu mkoa wa Shinyanga Bwana Ahmad Ngoma alichomewa Nyumba na vijana wa Greenguard ambao baadae walivamia msafara wa mbunge Kasulumbai. Mbona halisemei hili na halioni kuwa ni tukio la kinyama la kusababisha familia ya mtu kukosa makazi?
2. Kijana wanaye sema amemwagiwa tindikali na vijana wa CHADEMA kama mtakumbuka kesi yake ndio iliwafanya kina Kileo kupewa kesi ya ugaidi ambayo ilifutwa na mahakama na kina Kilewo na wenzake kufutiwa mashtaka ya kigaidi, sasa hivi kuna kesi ya kuhudhuru mwili ambao upande wa serikali unasema ushahidi bado hauja kamilika. Kama Mwigulu ana ushahidi kwa nini atembee na kijana huyo kwenye mikutano na asipeleke ushahidi ili hao anao sema ni vijana wa CHADEMA wafungwe?, Huko nako sio kuingilia uhuru wa mahakama?
3. Mwigulu analalamika kuwa kwenye kijiji cha Waswa walitegewa misumali na CHADEMA, CHADEMA jana walikuwa na mkutano kwenye kijiji hicho iweje CHADEMA wajitegee misumali wenyewe?! Lakini taarifa zilizopo polisi ni kwamba vijana waliotega misumali na kuweka mawe barabarani wanajulikana mbona hawaja kamatwa vijana wa CHADEMA?
4. Mhanga wa ushetu alikuwa dereva wa CCM aliye endesha gari iliyowateka vijana wa CHADEMA kwenye uchaguzi mdogo wa USHETU, Mbona hasemi kuwa gari ya CCM ilivunjwa vioo na dereva kujeruhiwa na wanakijiji wenye hasira baada ya kuona mwenzao katekwa?!
5. Kwenye tukio la ushetu walikamatwa vijana 15 pamoja na mbunge Kasulumbai wa CHADEMA, hadi leo hakuna hata kijana mmoja mmoja wa CHADEMA aliyerumande kwa tukio hilo na hakuna ushahidi wa wao kuhusika. Kama Mwigulu anawajua vijana wa CHADEMA walio husika na tukio hilo kwa nini asiisaidie Polisi ili anao ita vijana wa CHADEMA walio husika na tukio wakakamatwa?!
Umeskip dose leo eeh?
Chadema ni sawa na Alshabaab tu.
Viongozi wao wanatumia maisha ya watu kama mtaji wa siasa

![]()
![]()
![]()
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Ifakara wakati wa Mkutano wa Kufungua Kampeni uliofanyika Jana Tar.27/02/2014.Hapa akiwa na Wahanga wa siasa chafu zinazodaiwa Kufanywa na Chadema kupitia Vijana wake wa Redbrigade.Mwenye T-shirt ya Njano ni Mzee Alphonce John ambaye alitopolewa Macho kwa dispisi wakati wa Uchaguzi wa Udiwani huko Kahama Mwezi uliopita.
Mwigine mwenye Shati la Kijana ni Kijana Musa Tesha ambaye alimwagiwa Tindikali na Vijana wanaodaiwa Kuwa wa Chadema huko Igunga wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo.Mh:Mwigulu Nchemba jana amesisitiza Wananchi wa Kalenga kuwa makini na siasa Chafu za Chadema zinazofanywa sehemu mbalimbali hasa kwenye nyakati kama hizi za Uchaguzi.Amesisitiza kuwa kwenye Chaguzi zozote Vyama vya siasa vinashindanisha Sera na hoja kuhusu Maendeleo ya Wananchi wa eleo hilo,Mkataba wa CCM na Wananchi ni Maendeleo katika Taifa hili,Umoja na Mshikamano ndio ngao ya MwanaCCM yeyote.
Mwigulu Nchemba amesema dhambi ya Mauaji na Unyama unaoendelea kwenye mikutano ya siasa na maeneo mbalimbali haitamwacha Dr.slaa Salama kutokana na yeye kuwa kiongozi anayebariki Siasa chafu hizo.
Chanzo:Kalenga

Kuna watu wanapost humu kuwa Mwigulu ni muongo, eti kwanini wahusika hawajacgukuliwa hatua, kumbe kuna kesi mahakamani? Hebu tuambieni watuhumiwa ni akina nani?