Mwigulu Nchemba ni mtuhumiwa wa kwanza kutekwa kwa Absalom Kibanda

Kwa jinsi serikali yetu na jeshi la polisi wanavomuogopa mkulu na Nchemba hakuna kitakachoendelea hapo. Lengo lao ni kuona CDM inakufa kifo cha Mende. Lakini watasubiri sana kuona CDM inakufa na haifi ng'o labda Muarobaini uzae embe.
 

Ninaanza kupata wasiwasi na uwezo wa Nchemba kama kweli alistahili nafasi aliyonayo ndani ya chama chetu. Nahisi kama alipewa nafasi hiyo kwa makusudi maalum ya kuhangaika na CHADEMA badala ya kujenga chama na kurudisha imani ya chama kwa wananchi. Kibaya zaidi ni kuwa strategies anazotumia kutekeleza jukumu lake mbadala la kukichafua chadema hazijakaa kisomi. Nilisema jana hapa kwamba Mh. Nchemba anaharibu chama chetu, sikutegemea kama angeweza kuandika maelezo kama yale aliyoyatoa kwenye thread yake akikanusha kutohusika na video ya lwakatale. Maelezo aliyoyatoa ni ya standard seven drop-out! Kwa kifupi Mh. Nchemba anawapa credits chadema badala ya kukijenga chama chetu, please JK drop him!!
 
Kwa mujibu wa Mwigulu, ni Polisi au vyombo vya usalama ndio waliotoa video mtandaoni, ina maana kuna askari wasio na weledi wasiotunza siri za serikali.Pili ni kwa nini askari hawana uhuru wa kufanya mambo yao mpaka JF ipige makelele. Nilitarajia wapuuze kelele za JF na kuendelea independelty na uchunguzi. Je ni video ngapi kwa sasa polisi imepokea kutoka sehemu mbalimbali na je wanazifanyia kazi? na mrejesho waweza kuutoa kwa umma. Je raia tupo salama iwapo chama fulani chapanga mauaji huku sheria za usajili zipo wazi kuwa hakifai?. je Tendwa amechukua hatua gani mpaka sasa? je anakumbatia vyama vya kigaidi?. Nini sura ya Tanzania kimataifa kwa kujitangazia kuwa sie ni magaidi? je tutapata wa kweli wawekezaji wa kweli?. je tutaaminika vipi kimataifa iwapo hatutaawaambia ni nani nyuma ya ugaidi, mfadhili, malengo yake na je wao wapo salama ?. Haya maswali ni muhimi kuyajibu.
 
what if badala ya Kibanda angeteswa na kuumizwa hule Mwandishi wa Mwananchi mlengwa na video hiyo ndugu Msacky? unaona dili lilivyokuwa kali hapo? hata hivyo inabaki kuwa CDM ilikuwa inawatafuta na kuwatesa waandishi wa habari.

Kuna tetesi kwamba jamaa waliotumwa walichanganya kati ya Kibanda na Msacky wa mwananchi ili kupata picha kamili na muvi!!; ki uhalisia Nchemba lazima akamatwe atoe ushahidi sababu anatamba anazo Video nyingi tu zainazopanga mauaji.
 
Kwa jinsi serikali yetu na jeshi la polisi wanavomuogopa mkulu na Nchemba hakuna kitakachoendelea hapo. Lengo lao ni kuona CDM inakufa kifo cha Mende. Lakini watasubiri sana kuona CDM inakufa na haifi ng'o labda Muarobaini uzae embe.
we uliona wapi serikali inajikamata? mwigiru is protected na ndiyo maana ana tamba na CD's kibao kazificha, nafikiri atakuwa anazitoa moja baada ya nyingine... mpo hapo watanzania?
 
Naibu katibu mkuu wa ccm kakaimu cheo cha Mkurugenzi wa makosa ya jinai<DCI> kazi mwaka huu tunayo tuombe tu 2015 tufike salama kwani nia yake tusitoboe huu mwaka,nchemba hakuna asilojua kuhusu kibanda wala lwakatare koz yeye ndio mpelelezi mkuu

CCM wako busy wanapaka mikakati ya kuchakachua Katiba wakati wanajitahidi kudivert attension ya wananchi!!
 
anza na mbowe alituma watu wamdhuru kibanda baada ya kuacha kazi tanzania daima
ha ha ha, mnaumiza watu namna hiyo ku-justfy vitu weak kiasi hiki? poleni sana.
 
CCM wako busy wanapaka mikakati ya kuchakachua Katiba wakati wanajitahidi kudivert attension ya wananchi!!
wala siyo katiba mkuu, wako busy ndani ya chama makundi yanapimana ubavu -- urais 2015 ndugu yangu, watu hawasalimiani, yaani ni mbwai mbwai tu - sangoma ndiyo usiseme. yetu macho.

yaani ni vita within.
 
Naibu katibu mkuu wa ccm kakaimu cheo cha Mkurugenzi wa makosa ya jinai<DCI> kazi mwaka huu tunayo tuombe tu 2015 tufike salama kwani nia yake tusitoboe huu mwaka,nchemba hakuna asilojua kuhusu kibanda wala lwakatare koz yeye ndio mpelelezi mkuu

Ulitaka akaimu nani? Jamaa si anaumwa na yupo india au? May b ameona ndo anafaa kukaimu au ulitaka akukaimishe wewe? Wao si ndo wana Serikali?
 
anza na mbowe alituma watu wamdhuru kibanda baada ya kuacha kazi tanzania daima

Sina ugomvi na wewe M 23, shida yangu ipo kwa huyu ali like huu upuuzi mnyalukolo Chris Lukosi, hivi katika akili ya kawaida hata wewe unaweza kuamini kitu hiki kweli? Mbowe ni miongoni mwa watu ambao naamini wanatumia akili sana katika mambo yake, waliohama toka Tanzania Daima wapo wengi, yupo pia Charles Mlinga a.k.a Mchokonozi n.k, mbona hawadhuliwi nae, boss wake huyu Kibanda aliisha lituhumu jeshi la polisi kuhusika na hii kitu, wataalam wanasema kabisa, namna alivyo teswa kibanda inaonekana wahusika wamefuzu mafunzo ya halia ya juu na tena hufundishwa kwenye vyuo maalumu tu, hapa mtu binafsi kama Mbowe anawezaje kufanya hili? Kweli ukiwa sisiem hata akili nazo zinakuruka, sijui mkiwa huko hua mnakula chakula cha aina gani hadi kiwe kinatoa akili kichwani namna hii.
 
Ningeomba Akamatwe alaf ateswe japo hata kwa nusu saa ili aone na kuonja mateso wanayoyapa binadam wenzake....!
 
Nchi hii ina vituko vingi sana ndugu yangu, nakwambia Mwigulu hawezi kuwa shahidi wa kesi ya Lwakatare achana na kuhojiwa na police, this country belongs to them bwana
 
hizi ndizo siasa za tanzania, inatia hasira sana kuona jinsi gani wapumbavu wachache wanatusababishia kua na maisha ya wasiwasi, sina imani na jeshi la polisi wala usama wa taifa kwani wamekaa kichama cha mapinduzi zaidi ya kufanya kazi za kizalendo, kwa hali hii sioni jinsi gani tutafika.
 
nimejaribu kufuatilia kwa karibu utendaji wa viongozi wengi wa kamati kuu wa ccm ila kwa karibu na uamkini zaidi nimefuatilia ndgu mwigulu mchemba.kwa mam,bo mengi niliyomwona mwigulu akijihusisha nayo kuanzia uchaguzi wa igunga,arumeru,vikao vya bunge la tisa,tuhuma za kutumiwa sms za vitishi na viongozi wa chadema na sasa nma ambavyo anajiingiza hovyo hovyo na bila akili wala utashi kwenye hii movie ya video ya lwakatare kwa kujua ama kutokujua amedhihirisha namana ambavyo ccm ililamba "garasa" kumopa uongoxi wa juu ndni ya chama.
Hebu tujiulize;
1. Yeye anawezaje kufanya mawasiliano na njama kwa kumtumia kada wa cdm ndugu ludovick kwa kutumia namba zake za simu zinazotambulika kila kona?
2.hivi mwigulu anawezaje kumtumia pesa ludovick kwa kutumia namba yake ya simu iliyopo kwemnye kumbukumbu za bunge bila kuogopa kuwa zinafahamika?
3.hivi mwigulu anawezaje kufanya vikao hiotelini na vijana wasaliti wa cdm yeye mwenyewe bila hata kutumia vijana wengi wa ccm walioko pale lumumba wasio na kazi?
4. Hivi anawezaje kwenda loliondo kutoa kauli za kijinga na za kitoto mbele ya wamasai wenye uelewa na werevu wa kutosha hata akifikia hatua ya kupingana na kauli ya waziri wa maliasili na utalii kana kwamba wamasai hawajui kuwa yeye na waziri wantoka chama kimoja?

Haya ni baadhi ya mengi ambayo mwerevu yeyote(sio mnajimu feki kama wassira) anaweza kujiuliza wakati akitafakari uwezo wa akili na kiutendaji wa mwigulu mchemba.ni bahati mbaya sana kuwa kati ya makada wote ccm waliona kuwa mwigulu ndio kada majanja na mwerevu kuliko wengine na ndio mana wakampa uongozi.hana anachoisaidia ccm.anaganga njaa kwa hasara ya chama na taifa
 
CCM imeshakufa hata Mwigulu akibaki ndani ya chama hicho hembu niambie kwa strategy zipi za kiuchumi,kiafya,kisheria,kijamii,kibiashara,kimahusiano, kimiundo mbinu,kisiasa,kiutawala bora na zingine na zingine ambazo zitaifanya CCM iwe hai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…