Mtuflani Official
JF-Expert Member
- Dec 31, 2019
- 1,952
- 4,416
Juzi tu hapa nimeona wananchi Muleba wanajenga kituo cha Afya kwa pesa zao. Ingependeza Waziri akatuonesha vituo vya Afya anavoongelea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa nimejifunza kitu kimoja kuwa kipanya ni mtu wa ndani anayejua mipango yote huko ndani ndio maana katuni zake zinafikirisha sana ila ziko wazi sana kutoa ujumbe sahihi.
Waambie MATAGA wanafikiri hiyo ni miradi ya Mama.Serikali hii inapoteza fedha kwa miradi isiyo na maana. Mfano ujenzi wa SGR Reli ni upotevu wa fedha . Ilitakiwa waiimarishe reli ya kati na kurekebisha sehemu kadhaa korofi kwa kujenga madaraja au mahandaki siyo kutandika reli mpya ya SGR mwanzo-mwisho...
Sawa, tupate na mrejesho wa hizo zahanati zikimalizwaWaziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema katika kipindi cha wiki nne Serikali imekusanya Sh 48.4 bilioni kutokana na tozo za miamala ya simu, na zaidi ya Sh22 bilioni zimepelekwa katika vituo vya afya zaidi ya vituo 90...
Kipanya anajua afu anajua tena
Lameck kadanganya Data. Kwa mahesabu yangu kwa siku wanakusanya 10 billion. Kwa iyo billion 300 kwa mwezi. Billion 248 zingine wanazoficha zinaenda wapi? Waache kutupotosha mara moja. Billion 48 kwa mwezi ni kidogo sana.Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema katika kipindi cha wiki nne Serikali imekusanya Sh 48.4 bilioni kutokana na tozo za miamala ya simu, na zaidi ya Sh22 bilioni zimepelekwa katika vituo vya afya zaidi ya vituo 90...
Hakukuwa na haja ya serikali kujiingiza ktk mradi mkubwa wa ujenzi wa reli mpya ya SGR. Ilitakiwa waiimarishe reli ya kati ya mkoloni kwa kujenga madaraja na mahandaki sehemu korofi na kuimarisha reli nzima ya zamani. Mzigo huu wa mafuta unapelekwa Uganda kwa reli hii hii ya zamani huo ni uthibitisho tosha kulikuwa hakuna ulazima wa ujenzi wa reli Mpya ya SGR mwanzo mwisho ulio na makolombezo yote ya ufahari usio na ulazima wowote kiuchumi.
Acha ujinga, nani kasema anataka kukatwa. Tunataka kukatwa kodi halali, siyo hii y kisengeKodi watu hawapingi,, shida ya nchi hili ni ubadhilifu, kesho na keshokutwa unasikia fedha zimechotwa, sijui nanii kapiga bilioni 2, halafu wanachekeana, lau kama wangekuwa serious(mafisadi wachukuliwe hatua, matumizi ya serikali yapunguzwe, wabunge mishahara ipunguzwe, walipe kama wengine, na kero ndogo ndogo) sio tu kodi, bali wananchi tungekuwa tuko radhi kuchangia mradi fulan.. Tuliweza kuwachangia watani(yanga) [emoji23][emoji23]ndio tushindwe vitu vya msingi kwa serikali yetu bwana.
Ukimsikiliza Nchemba, unagundua kwamba tuna mawaziri wenye uwezo mdogo sana wa akili. Ni mtu hawezi hata kuzungumza na umma. Hawezi hata kuonesha kwamba ana digrii moja. Hata usoni haoneshi kama ana akili timamu. What a hell with this creature?Wakuu,
Waziri wa Fedha, Dr Mwigulu Nchemba anazungumza na waandishi wa habari muda huu kuhusu miradi ya Serikali pamoja na Tozo za miamala ya simu pamoja na mafuta. Kuwa nami kukujuza yanayojiri
==========
Mwigulu Nchemba-Waziri wa Fedha na Mipango
=▷ Itakuwa aibu mtanzania yoyote alie hai, kuna mradi umekwama kwasababu tu viongozi waanzilishi labda hawapo duniani au hawapo kwenye madaraka, itakuwa aibu ya kila mtanzania alie hai leo.
=▷ Katika kipindi cha wiki nne Serikali imekusanya Sh 48.4 bilioni kutokana na tozo za miamala ya simu, na zaidi ya Sh22 bilioni zimepelekwa katika vituo vya afya zaidi ya vituo 90
=▷ Kipindi cha mwezi mmoja Serikali imekusanya Sh 24 bilioni, kutokana na tozo za mafuta ambazo ni mahususi kwa ajili ya kujenga barabara.
=▷ Kama serikali tutaendelea kupokea na kuyafanyia kazi maoni yote, na haijalishi mtoa maoni yuko Serikalini au la, kwetu maoni ni maoni muhimu maoni hao yanalenga kujenga nchi yetu
=▷ Tuliokuwepo hapa ni dhamana tu, la msingi hata yote tunayofanya ni yetu na ni njia ya kupangalia namna ya kuyafanya, ndio maana ndio maana kiongozi wetu mkuu alisikia sauti hizo na akaelekeza kwamba haya mambo yafanyike.
=▷ Imechukua muda, ni utaratibu tu za kiutekelezaji wa maelekezo na sababu nitazielezea mbele, huwa tunahusisha na makundi mengine ambayo yako nje yetu sisi.
=▷ Mheshimiwa Rais akishakuwa na malengo mazuri namna hii na kule vijijini kwenye maeneo yetu, yakishakuwa mazuri hivi tusigombane kuhusu malengo wala khusu utaratibu. Tushauriane tu namna ya kufanya vizuri kwa ufanisi mzuri zaidi.
=▷ Tunapata ufanisi zaidi tukifanya hivyo, watanzania wanaoishi vijijini na wanaoishi mjini wote wajione wako Tanzania.
=▷ Hii ndio itakayotuondlea pengo la walionacho na wasianacho, zamani ilikuwa inatokea wanafanya mtihani, kijiji kizima hatokei hata mtoto mmoja aliefaulu kwahiyo kuboresha hii miundombine, afya watanzania tukibebe kwa yowe kabisa kwa sababu ni chetu. Niwaombe watanzania kuendela kuwa watulivu na wavumilivu.
Yeye alipo hajui hata bei ya petrolSiasa za kisanii kuna siku zitalighalimu taifa letu.