Nakubaliana hapo kwenye leadership style sio lazima zifanane na there is no single approach of winning trust.
Isitoshe Magufuli zilipendwa ata iweje na Samia is entitled to steer the ship on her terms
Hoja yako nzuri kuna ya kuchukua na kuna ya kufikirisha.
Mama mi namwona tu kama caretaker president hadi 2025 tu. Baada ya hapo atulie zake astaafu kwa heshima awaachie wenye energy, wenye charisma, watu wanaoweza kucommunicate na kushawishi. Hapo tupo pamoja, lakini pia ieleweke hakuwahi kujiandaa kuwa president, ni president wa circumstances tu.
Ila kwangu naona katika kipindi hiki cha mpito tuna wajibu wa kusaidia jahazi lisizame kwa kumsaidia mambo yaende. Falsafa ya tozo haina shida hata kidogo. Shida ije kwenye coordination za hizo tozo na matumizi ya hizo tozo. Kwa mfano what the hell are ewura doing kwenye muamala wa tanesco? Mimi kwanza nina ishu na maagency kibao ya serikali yaliyopo tu kinyonyaji. Yanachojua ni kwenda mtaani kunyonya hela za watu tu, tija za uwepo wake haupo kabisa.
Kuhusu hierarchy of needs za watu wetu mimi naona sometimes huwa tunaentertain na kuhurumia upuuzi bila sababu zozote za msingi. Watu wa nchi si kwamba ni maskini in a real sense. Ni just wapuuzi na baadhi ya upuuzi ni kutokana na tamaduni za asili zinazowafanya waonekane maskini kumbe siyo maskini.
Chukulia mfano mmasai na ng'ombe zake 300 lakini hataki kumpeleka mtoto shule. Huyo ni maskini? Huyo anashindwa kuchangia ujenzi wa shule kupitia kodi au tozo? Sometimes serikali inabidi kutumia brutal force, top down algorithms ili kufanya huduma za msingi zipatikane hata kama watu hawaperceive hizo huduma kama basic needs. Leo hii kuna shule kibao umasaini na zote zimelazimika kuwa boarding ili kubypass culture ya kimasai isiyokuwa favourable kwa mtoto kwenda shule na isiyofavour wanafunzi wa kutwa.
Nafikiri pia in your mind unawahurumia akina mama na wazee na watu wengi tu ambao kiukweli ni ndugu zetu wa vijijini na hata mjini ambao ni maskini kweli kweli. Yes, kama ni maskini kweli kweli hawezi kufikiwa na hiyo miamala (maana hata simu hana, haweki vocha, hawezi kupokea mpesa wala airtel money, na hawezi kutuma pia, nyumba haina umeme wala maji mtiririko vitakavyohitaji afanye transactions kupata hizo huduma).
How do you help such people? Ni kuwapelekea miundo mbinu wezeshi kama barabara za lami vijijini, maji tiririka vijijini na umeme vijijini, na shule vijijini na huduma za afya vijijini). Uwepo wa hizo huduma kote kote ndio ukombozi wa kweli wa mtu maskini. Kama Mwigulu alivyosema katika hayo mambo ya msingi hatutakuwa na debate. Debate iwe je kama tutatozana kufika huko ni vibaya? Na kama tutatozana njia gani bora? Njia za zamani za kuwaroza watu wachache doesn't seem to work. Kuna wakati police traffic waligeuka kufanya kazi ya TRA wakapewa hadi lengo la kutimiza kila mwaka na mlipiga mayowe, hata mimi niliyapiga maana si kazi ya police kutafutiza faini.
Katika kufikia hayo malengo mujarabu mzigo usipokuwa distributed kwa wananchi wote utawaelemea watu wachache. Na si afya nchi kujengwa na watu wachache, hilo tulikwepe kwa namna zote.