Mwigulu Nchemba, tafadhali kafute mabango yako barabarani!

Mwigulu Nchemba, tafadhali kafute mabango yako barabarani!

Habari ndugu Mwigulu.

Wananchi wa Mbeya tunakuomba uje ufute maandishi yako uliyoweka kwenye mitaro na madaraja mbalimbali hapa Mbeya kwamba wewe ni Rais 2015.

Kutokana na jina lako kuondolewa mapema bila maelezo huko Dodoma wananchi wa Mbeya tunahitaji uje usafishe mji wetu haraka iwezekanavyo.

Nawasilisha ndugu Mwigulu Nchemba.

Akimaliza Mbeya aje Mwanza
 
Awe mpole tu maana alifanya siasa chafu sana hapo nyuma bila kujua taswira yake mbele ya jamii inafifia japo hivi karibuni ameonesha kubadilika lakini its too late. Kama ipo ipo tu hata baada ya miaka 30. Hili ni funzo kwa vijana msikubali kutumika vibaya siku zote muwe waadirifu, wenye kujitahidi kutumia hekima na busara. Tanzania 2015 kwa mapenzi ya Mungu atatuongoza kuchagua Rais wetu.
 
Tanzania tunatafuta kodi kuendesha nchi na ilhali rahisi kuzipata ? Anatakiwa alipie kila toleo tuingize Rea
 
Hata boko nako alipita muheshimiwa rais nchemba
 
Awe mpole tu maana alifanya siasa chafu sana hapo nyuma bila kujua taswira yake mbele ya jamii inafifia japo hivi karibuni ameonesha kubadilika lakini its too late. Kama ipo ipo tu hata baada ya miaka 30. Hili ni funzo kwa vijana msikubali kutumika vibaya siku zote muwe waadirifu, wenye kujitahidi kutumia hekima na busara. Tanzania 2015 kwa mapenzi ya Mungu atatuongoza kuchagua Rais wetu.

Huyu bwana alikuwa anatumika bila kujua mustakabali wake utakuwaje,Sasa kamati yake isiyo na maadili imemuona sio muadilifu kazi anayo!
 
Mwigulu anatakiwa kwenda kufuta hayo maneno haraka .Ukawa tukichukua nchi hayo mabango atayalipia kodi na kuyafuta kwa ulazima
 
Tena mengine yameandikwa kwa mkaa.........akafute haraka...........

NEMC mko wapi? Shughulikieni mchafua mazingira huyo. Mkishindwa najiaandaa kufungua Kesi mahakamani. Tumezoea kuona matangazo kwenye standi yenye maneno yafuatayo "Usitupe takataka, Usikojoe, Usiteme mate, Faini Shs. 50,000/. Jamani halmashaouri/manispaa husikia toze faini jitu hili chafuzi la nchi nzima.
 
:cheer2: Ha ha ha ha sasa jamani yeye ni rahisi kuyafuta kwa njia zile zile alizoandika....
wakumuuliza ni Baba wa watoto, Babu wa wajukuu Yeye alianzia kwenye Boda boda Friend of Lowassa.... akaweka stika mabasi makubwa manne hivi safari ya matumaini..... nguo zenye rangi ya mbuga zetu nazo friend of Lowassa ! Huyo ataanza kufuta nini hapo tafadhali nijuzeni mie maana namhurumia kama mama aliyetafuta mtoto with late ages akabeba mimba miezi mitano ikatoka bila kuonyesha dalili kama hata tumbo liliwahi kuwa na mtoto!

Imaging hata jina halikutokea licha ya kuonekana yaelekea jina lilikatwa siku aliyochukua fomu! nauliza kwa nini washauri wake mpk wapambe wake wasimpe mwongozo? Jina lenyewe (SAFARI YA MATUMAINI) NENDA KAISHI KWA MATUMAINI
 
me naungana nanyi kumtaka ndugu Mwigulu kufuta maandishi yake kwenye majabali na kote alikochafua. pia wale ndugu wanaojitambulisha kama friends of Lowasa walioshika kasi kufanya usafi mijini na kuchangia damu hospitalini siku chache zilizopita, si vibaya kama wataendelea na utamaduni huo waliouanzisha tena kwa kasi ileile ili tuamini kuwa walikuwa na uzalendo wa kweli
 
Hii kasi ya mwigulu angeitumia kusafisha mazingiza dar ingekuwa kama MOSHI kwa kipindi kisupi...yani daraja limekamilika halina week kashakuja usiku na kuliandika...😕
 
Ni nchi nzima kachafua

Si ndo alikuwa anajiita dogo jembe huyu! Kwa kweli kachafua nchi nzima na mwandiko unafanana! Nafikiri mwandishi wake atakuwa nani yule..... Ah mtela sijui mleta anajua mwenyewe. Akafute haraka.
 
Nadhani moja ya sababu ya kukatwa itakuwa ni hii, maana ni uhuni mtupu! Afatiliwe inawezekana hata shule alizosoma kaandika ujinga kama huu.
 
Moja liko pale karibu na dawasa nikipata huwa nacheka sn
 
Hata huku tanga kunani pia..nadhani alikodi vijana kwa ajili ya hiyo kazi maalum..

Mbona mwandiko unafanana? Atakuwa mtu mmoja alipewa hii kazi maalum. Lazima atakuwa yule 'kijana' wake aliyetoka CHADEMA.
 
Back
Top Bottom