Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Lameck Nchemba akiongoza kikao kazi cha kuchakata maagizo ya Rais Samia kwa Wizara hiyo.

Waziri amewaambia Wafanyabiashara nchini kote na Watanzania kwa ujumla wasiogope kuweka fedha zao Benki kwani zitakuwa salama na hazitachukuliwa.

Dkt. Mwigulu ameteuliwa hivi karibuni na Mhesh Rais Samia kuongoza Wizara ya Fedha akitokea Wizara ya Sheria na Katiba.

Hapa kazi tu & Zege halilali

MCL

=============

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani kuacha tabia hiyo kwa maelezo kuwa fedha zao haziwezi kuchukuliwa.

Dk Mwigulu ameeleza hayo leo Jumamosi Aprili 3, 2021 katika kikao na watendaji wa wizara hiyo na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Msajili wa Hazina (TR).

“Kwa wale wafanyabiashara walioona wakiweka fedha zao zitaonekana mtandaoni labda zitachukuliwa zote nitoe rai warudishe fedha kwenye mabenki zitaliwa mchwa au panya bila sababu, uchumi wa kisasa sio wa kuweka fedha kwenye boksi.”

“Kodi itatozwa tu kwa sehemu ya fedha inayotakiwa kukusanywa na sisi tujenge utaratibu wa kutii sheria kulipa kodi na kuwa wazalendo kwa nchi yetu.” Amesema Mwigulu.
 
Warudishe walizochukua kwanza, ile shule kule Arusha ambayo ilikua inatoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 100 na kusomesha vijana zaidi ya mia tano kwenye ngazi mbali mbali, warejeshewe zile millioni mia tano zao na tuwaombe radhi.
 
Ni pale Paka anapomwambia Panya wawe marafiki.....

Kwani walivyozikwepua hapo kabla walitoa taarifa ?, Leo Hawazikwepui kesho wakibadilisha mawazo ?

Kwahio kama kukwepua ilikuwa kosa, Je watawarudishia waliowakwepulia ?
 
Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewaambia Wafanyabiashara kuwa wasiogope kuweka fedha zao Benki kwani zitakuwa salama na hazitachukuliwa
Kweli ni Mwisho wa enzi. Yaani unyang'anyi ulivyokwisha ghafla utadhani imepita miaka mitatu tangu March 17? Kumbe waliokuwa wanasema tarehe hiyo haitasahaulika wako sahihi.
 
Kwa hiyo mwanzoni walikuwa wanachukua za nn? Wamegundua watu wameamua kuanzisha vibubu sivyo!

Hamna jambo jema kama kutenda haki! Haki huinua Taifa, haki huleta baraka, haki huponya Taifa!

Ahsante sana Mama yetu Samia, tuna imani kubwa sana na wewe!! Ahsante kwa uongozi sikivu, tunakuombea maisha marefu yenye furaha, na afya njema tele!
 
Akikabidhiwa makabrasha Wizarani hapo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dotto James kama ishara ya kukaribishwa rasmi ofisini , Mh Mwigulu amesisitiza umuhimu wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa .

Amewaasa wananchi wote wakiwemo Wafanyabiashara wakubwa na wadogo kurejesha pesa zao benki ili zitunzwe kisasa badala ya kuzihifadhi kwenye maboksi ambako zinaweza kuoza ama kuliwa na panya .
 
Back
Top Bottom