Mwigulu: Sijawahi kuwasiliana na Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa e-mail tangu nizaliwe

Watanzania wana kiwango kikubwa sana cha uelewa kiasi kwamba wanaweza kupambanua kati ya uongo na kweli. Mwigulu na wenzako mambo mnayotenda dhidi ya binadamu yamevuka kiwango cha uovu nadhani shetani pia anawashangaa.
 

Ukinitajia kuwa sijui hizo ni siasa za nini sijui huwa unaniudhi sana. Wewe ni mtu wa aina gani? Huu uliohusishwa nao ni uhalifu na ukihusisha mauaji halafu wewe unajieleza kama vile ni jambo dogo sana! Mbona unaonyesha maisha ya watu wengine hata hayakushtui yakipotea? Au kwako ni kafara?
Mwigulu, mtu mcha MUNGU na mkweli katika jamii yeyote kwanza habari hii ilipotoka tuu na kuonyesha kuhusisha maisha ya watu kupotea lazima ingemnyima raha na hata utetezi wake ungeonyesha jinsi gani kaumizwa na walao kutajwa tuu. Lakini sio wewe! Wewe ni kama vile umshtaki fisi kala mbuzi wako, utetezi wake utaonyesha kuwa hajala wako ila kula mbuzi sio issue kwake.
Hao Polisi watamuulizaje Ben kaingiliaje mawasiliano yenu bila kuwasiliana na nyinyi wenye hayo mawasiliano? Au wewe unaposema kahojiwa kwa kutengeneza e mail bandia jee hao Polisi walijuaje ni bandia bila kuwasiliana nanyi?
Kama kweli mlipanga hayo mambo, nakuhakikishia utakuwa na mwisho mbaya kisiasa na kimaisha ila KAMA yote yasemwayo unasingiziwa MUNGU atakupaisha na kuwa juu siku zote za maisha yako.
 

Kheeh! Leo nimegeuka kuwa mchungu kwa Serikali na CCM kwa kuwa walinisomesha nje wakaninyima nafasi ya ajira Mambo ya nje?

Sio lazima niajiriwe serikalini?Kuitumikia nchi sio lazima niajiriwe mambo ya nje.By the way,Serikali iliyonisomesha huko ilitumia kodi ya watanzania na sio kodi ya pango ya CCM iliyohodhi mali za umma.Naomba tuheshimiane na iwe mwisho kutoa kauli za kipuuzi kama hizi

Na kama mnadhani mnakomoa vijana kwa njia hii basi subirini mwisho wenu na chama chenu katika ramani ya siasa.Kitu ambacho hamtaweza kutunyang'anya ni elimu.Hamuwezi kuhujumu taaluma ambayo ipo kichwani.Mnashangaza!
 
ukisikia Nchemba amepewa uwaziri utajisikieje?

Sitoshangaa mana sijui uwaziri watu wanapewa vigezo gani mfano Ngeleja is good katika Law ila alipewa wizara ya Madini na nadhani wakaona is under performance na ndo mana wamemuweka Muhongo who is good katika hiyo Wizara so silaumu wala sipendekezi nani apewe uwaziri na nani aachwe ila nnachoomba mpe mtu kutokana na uwezo wake katika kuongoza na pia katika hiyo wizara au ni sawa kumpa mtoto mdogo jembe akalime wakati hata kulishika ni tabu ila itabd azuge kua anaweza kubeba ili watu wamsifie kua ni Jembe au atakuja kua na nguvu baadae while he is nothing.So tunamuomba Raisi katika kuteua mtu awe anaangalia uwezo wa wa mtu katika kuongoza na hata Fani kama ni yake au lah mana Magufuli anafanikiwa kujua wakandarasi wabaya kutokana na kua na timu ambayo haiwezi kumdanganya maana anajua hayo mambo na ndo watu tunaowahitaji taifa hili sio wau wenye elimu ya kufoji

Ni ushauri tu
 

....Mkuu Usiogope Mungu yupo pamoja nawe... yaweke kwa maanufa ya vizazi vyetu vijavyo!!!

.....Leo hachomoki mtu hapa...tumechoka!!!!
 
Mods tunaomba muweke hapo juu majibu ya Kamanda Ben Saanane.

Pia Mwigulu Nchemba nakuomba umrudie Mungu hii dec kabla hujaingia mwaka mpya, Pia jitahidi uwasiliane na watumishi wa Mungu wakupe msaada wa kiroho zaid na upate na ubatizo wa maji mengi.

Cc😡Invisible
 
Last edited by a moderator:
mwigulu mwaka huu kabla haujaisha unapaswa kuokoka ,aya maisha ya duniani ni ya muda tu na ni ya kupita, laana za damu ya watu hazitakutesa wewe tu bali fikiri juu ya watoto wako kwa baadae,kaini alipo laaniwa, mpaka wajuukuu waliishi na hiyo laana,badilika mungu ni mwema ukitubu kwa kumaanisha anasamehe,usisubili mwaka huu uishe kabala ya kuchukua maamuzi magumu ya kuokoka ,vyeo vitapita ,pesa itapita ,umaarufu utapita,ila neno halitapita ,usimfurahishe mwanadamu wa kufa kesho mfurahishe mungu asiyekufa,maandiko yanasema na alaaniwe amtegemeaye mwanadamu,ivi oporesheni kama tokomeza damu za watu mnaweza kuzikimbia nyinyi viongozi na watoto wenu?
 
hata kipofu huona watu ni vipofu isipokuwa yeye wakati yeye ndo kipofu mwigulu ni mnafiki mkubwa wewe mipango yako hatafanikiwa kamwe shetani mkubwa weweee
 
Chemba ,unaonekana unakipenda sana chama kuliko Watanzania hii inapunguza heshima yako mbele ya uma.Chama kinaweza kufa,lakini nchi ikaendelea kuwepo.Unaweza kuwa maarufu bila hata ya kuwa kasuku wa chama,na maelfu ya watu wakakukumbuka kwa mema iliyoitendea nchi yako.Kuhusishwa na njama chafu kama hizi kunahalibu future yako ya siasa.Maelezo kwenye utetezi wako bado yanaleta utata.
 

ID ya Tawsira na Hamy D zipo reserve..
 
nilijua hutakubali. hivi kati yako na nchimbi nani kati yenu ni kiongozi hadi mpakwe matope?. hii thread haiwezi kukuondolea shutuma.
 

Ukiwa kama kijana unaejitambua na ulienda shule ni vyema kuhakikisha elimu uliyoipata inakunufaisha mwenyewe, familia yako na jamii kwa ujumla wake. Hakuna chochote katika hili kinachothibitisha uhusika wao lakini pia hatuwezi kusema moja kwa moja hawahusiki. Kinachoniuma sana ni kuandika kuwa fulani kahusika na kuuwawa kwa flani tena kwa njia za kidanganyifu kama hii ya email. Hao watu wanakutana kila mara na wajua wazi hatari ya mitandao swali kwanini wasiyazungumze haya walipokutana mpaka ati watumiane emails kupongezana? Tizama kwenye email kuna sehemu inasema tutakutana palepale pa siku ile kweli huu si utoto wawazi kabisa? Uweze kuandika jinsi ulivyoshiriki kuua na kuhujumu upinzani ushindwe kutaja wapi mtaenda kutana na mhujumu mwenzenu ambaye mmemtaja katika mawasiliano yenu? Jamani mbona twajidhalilisha kiasi na kushusha dhamani ya elimu yetu katika kiwango kikubwa hivi? Hii ni propaganda ya kitoto au iliyntengenezwa kitoto mno pamoja na kwamba siwakatilii kuwa Mvungi ameuwawa kutoka na kazi yake aliyokuwa aifanya. Hata hivyo sishangai katika siasa ya bongo inawezekana tu. Kama mtu ajitangaza yeye ni mtoto wa Nyerere na kumkana baba mzazi mhaya kweli itashindikana kutafuta mtoka kupitia wanasiasa walio na majina?
 
 

Dongo Chakani,UKISIKIA AAAIIIIIII ujue limempata!!!
 


Mkuu Ben, Hakuna marefu yasiokuwa na ncha.
Ngoja tusubiri uteuzi wa mkuuu wa nchi katika wizara ya mambo ya ndani itakuwaje. Na kama atatuwekea mtu sahiii basi tutatoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha kukamatwa kwa watu walio husika katika mauuaji ya mabomu na utekaji ambayo mpaka sasa hatujapewa jawabu.

Nina uchungu sana kwani nimepoteza mtoto wangu katika bomu la soweto na mpaka sasa nina ushaidi usiopungua 80% Mwigulu kuhusika na kifo cha mwanangu.
 

Hv ikithibitika kuwa ni email halisi na imetoka kwako ebu tuambie.adhabu itayokufaa...ict sio mchezo
 

....Mkuu Ben huyo zuzu weka pending!!!

Leo kazi moja tu kusafisha bendera ya Taifa letu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…