Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwananyamala wao wamepokea mwili WA Marehemu kutoka kwa Nani?Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Desemba 11, 2024 amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
View attachment 3177965
Ulomi aliyekuwa akifanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo yaa Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu 11 Desemba 2024.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro zinaendelea, baada ya simu zake kuita bila kupokelewa.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Desemba 16, 2024 baba mkwe wa Ulomi, Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mke wa marehemu, akimjulisha kuwa amepata taarifa kuwa mwili wa mumewe uko hospitali.
Pia, Soma:
• Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta
• TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi
• Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea
Nimeumia hadi hamu ya kula imekata!kama namjua.Binadamu tumefikia huku.Hatari.Mungu awape faraja ndugu,jamaa,mke na wote waliogushwa.
Aaghh wapi, hapa ni kumshukuru MUNGU Tu kuwa hata huo mwili umepatikana!Dah uchunguzi uanzie kwa walioupeleka mwili hapo hospitali, hii itatoa a lead ya walipoupata na mazingira gani then mambo yatajipambanua tu
R.I.P Ulomi

Na mwili ukiletwa lazima uongozi wa hospital wafahamu mchakato mzima🤔Nani kauleta mwili?
Mwili umekuja una hali gani?
Majearaha> Majeraha yanaonesha ya ajali au kitu kingine?
hii haihitaji uwe MOSSAD kuuliza na kufafanua.
Inashangaza sana, yaani ungeokotwa porini au mbugani huko ingekuwa hakuna pa kuanzia ila hospital ya taifa, inajulikana mwili umetoka wapi na kifo kimesababishwa na nini.Na mwili ukiletwa lazima uongozi wa hospital wafahamu mchakato mzima🤔
let be reasonable guys. Serekali haiwezi kuuwa watu hovyo ikuuwe ww nani!!?? Yani serekali ije ikuuwe ww tigopesa kuweni na heshima kidogo basiHuyu kaka hakuumwa lakini leo anakutwa amefariki.
Mnaotenda huu ukatili mtakosa amani ya moyo hata kama mnaishi kwenye mahekalu na kuendeshwa kwenye VX.
Hizi damu na masononeko lazima zitawawesesha kupita maelezo.