Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

Mzawa tapeli unamlinda Kwa maslahi ya nani na Kodi anakwepa?
 
Mbumbumbu kama huyo kesho atakuja tena ooh tusijenge Sgr itaua biashara ya malori na mabasi
 
Ni kweli,Ila upande wa kulipa Kodi mchina nae hajambo kwa kukwepa. Maana hata sasa wale wachina wa kkoo bado wanakwepa Sana Kodi.
Akili ya kukwepa kodi huwa haina tabaka, hata mzungu ukizubaa tu unapigwa, toka dhana ya mfanyabiashara duniani ni kupata faida kubwa kadri iwezekanavyo toka zamani nyakati za yesu, wakwepa kodi walikuwepo!
 
Tuache mihemko, Duniani kote kwenye nchi zilizoendelea magulio yapo kila kitongoji.

Tusikariri maisha kwamba lazima watu wote wajazane Kkoo..

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Shida sio uwepo wa magulio , shida ni nani anafanya hayo magulio na mikataba ipi
Wachina ni watu wa shortcuts sana na wezi plus roho mbaya , na michezo michafu mingi wanaijua na kuifanya ,
 
Sisi wananchi tunachotaka ni bidhaa kwa bei ya chini nyie madalali mtajijua dunia ni soko huria ,kariakoo walijaa Wachagga wezi wezi tu kuibia WATU wasiojua bei acha wachina wawavunde tena serikali iwahi haraka

USSR
Nyani hushangilia kifo cha mwenye shamba ,wakiamini kuwa watakuwa huru kutafuna mahindi bila bugdha , wasichojua kuwa mwaka unaofuata hakuna wa kulilima hilo shamba.
Kuna siku tutakuja kuona umuhimu wa hawa wafanyabiashara wa ndani , mchina hana la maana analotaka kutunufaisha zaidi ya kujichukulia pesa.
 
Na hafahamu nini maana ya biashara.
😂😂😂 Aseee na analalamika KWA kujiamini kabisa kiatu icho icho anaagiza china mpaka anakivaa KWA elfu30 kuna watu wengine tuache tu kuwajibu huenda yupo igunga anahadithiwa basi akalibeba hivo hivo
 
Ulinde raia matapeli Kwa maslahi ya nani? Kwani wachina wanakuja Bure? Wataingiza pesa nyingi kuliko viduka vyenu hivyo,tafuteni kazi za kufanya mapema
Viongozi wanatokana na jamii wanayoishi.

Kuwaita raia matapeli ni kuwakosea.

Raia kuwa matapeli ni kushindwa kwa majukumu ya msingi ya Serikali.

Ukiona utapeli unazidi basi jua serikali imefeli pakubwa.

Raia matapeli viongozi nao watakua matapeli tu.
 
Maisha ni ushindani na sio kubebwa.
Maisha sio mazoea thus ukipata usiweke kituo ongeza vyanzo vingine.
Waache wauze
 
Hao wachina wasijae kariakoo tu waruhusiwe wajenge masoko yao KILA mkoa Ili tupate bidhaa bei chini.
Hata hizo bidhaa za kariakoo zimetoka China
 
tatizo watanzania tunapenda urahisi sana, kama wachina hawana ujanja ujanja katika kulipa kodi wapewe. Hamna haja ya kumwacha mtanzania asiyelipa kodi kariakoo
 
Imepitishwa lini?

Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania ilipinga hili
Waambie biashara ni upinzani,pili hata wachina wajae nchi nzima,hawatokosa kuuza kila mmoja na riziki zake
 
Tuache mihemko, Duniani kote kwenye nchi zilizoendelea magulio yapo kila kitongoji.

Tusikariri maisha kwamba lazima watu wote wajazane Kkoo..

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app


Nchi nyingi Duniani kuna China Town masoko ya Wachina na local Markets Masoko ya wazawa

Hakuna cha kushangaza hapo ni vitu vipo Duniani
 
Wanaibia wanunuzi na serikali kwa ujumla kwa tamaa ya faida kubwa isiyoendana na huduma (bidhaa). Mfano kiatu anauza 50,000 apate faida ya 15,000 nje ya kodi. Kiatu hichohicho nikiagiza China kinagharimu 30,000 kila kitu hadi nakivaa
China hakuna kiatu cha elf 30 ni 15 kushuka chini
 

Hacha ushamba wewe sio kila kitu mnapinga pinga na kupiga kelele Tembelea Nchi zilizoendelea ukaone China Town
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…