Mwisho wa mwaka taja sifa ya memba yoyote unayempenda na umpe na cheo

Mwisho wa mwaka taja sifa ya memba yoyote unayempenda na umpe na cheo

Kapoteza sana jukwa
kapotea sana jukwaani ,anapenda totoz na mada zake zote zinanifanyaga kutabasamu
Zero IQ
Mm ndo ninayekumbali sana , sikuuu utakuwa wapi nikukaribishe tunywe tule na marafiki
Mwamba ametutenga sana,alikua anafanya nicheke Kila nikisoma pigo zake.
 
Habari wanajamvi?
Tukiwa tumebakiza siku takribani 15 kupindua mwaka, kuongeza thamani ya upendo miongoni mwa member JF.

Taja memba yoyote unayempenda mpe na sifa yake na cheo

Mimi naanza hapa[emoji116]
DR Mambo Jambo
Huyu mkuu namuheshimu sana kwa mabandiko yake ya DINI, ananifundisha vitu vingi sana ila posti zake za udaktari nazirudiaga mara 10 10, sio uislamu wala ukristo.
Nampa 5star kwenye masuala ya DINI.

Kiranga
Huyu jamaa namkubali sana kuanzia kupanga hoja na kupangua hoja, kila punch anayorusha inafika.
Maarifa anayomwaga nampa 5star masuala ya Logic (mantiki)

Ritz
Huyu jamaa namkubali sana kwenye kuleta taarifa za hamas masaa 24 hata kama aljazeera haijapata taarifa yeye anayo
Ni msemaji wa hamas ukanda wa afrika mashariki.

Robert Heriel Mtibeli
Taikon wa fasihi huwa anagusa nyanja zote, ananifurahisha sana nyuzi zake, inabidi utulize akili kuzisoma. Huyu ni Taikoni wa fasihi hapa nampa nyota5

Twende kazi( kumbuka hii ni kwa ajili ya ku appreciate na funny)[emoji116]weka list nyingine chini hapa.
Mkuu ungebalance na dada ,shangazi , wachumba na mabinti zetu .
 
Back
Top Bottom