Mwisho wa ndege za kivita, funzo la vita vya Ukraine na Urusi

Naona umeona hakuna sehemu na kutoa udaku wako umekuja kuutoa uku unajua watu 500 kufa kwa siku saivi wangekuwa wangapi
 
kwa muonekano Russia kakutana na chuma ya pua aliingia kichwa kichwa , waafrika tujifunze kisaidiana kama ulaya sio wachambuz uchwara wa siasa za ulaya wakati jiran drc anawaka moto ila tupo kimya mpk USA awape ela ndo mkasaidie maiiran
Mwafrika ukipagana naye vita vya uchambuzi au vya kuwashindanisha Urusi na USA anaweza kukushinda mapema sana.
Ila ukitaka akae kimya mwambie muingie field ya kutafuta solution ya kumkwamua mwafrika kwenye mkwamo wa kijamii na kiuchumi utaona anavyoyeyuka.
 
War is not a rigged game [emoji23][emoji23] mabeberu huwaingizi kwenye vita kizembe watashiriki kwa mlango wa nyuma sehemu ambayo haina maslahi ya kitaifa watatumia mercenaries hayapendi hasara yameshajifunza.
Ukraine alivamia na hii sio mara ya kwanza kuvamiwa , 1945 , 2014 na 2022 waafrika sio wanyumbulifu ni watu wa kumezeshwa habari tu
 
urusi huvamia majiran zake na hii sio mara ya kwanza , hata ukraine alivamiwa 1945 pia wakataka ivamia 1990s pia 2014 na 2022 Sio kila kitu cha kulaumu mabeberu
 
T14 Armata
 
Kwa sasa mbinu endelevu ktk medani ni Kitengo cha upelelezi KIWE UPDATE...
 
Mleta mada hivyo vifaru vitaendelea kuwepo vitani miaka zaidi ya 100 ijayo. Kama unataka kuondoa armour basi tuambie movement ya wanajeshi itakuwa supported na nini. Wanajeshi hawatoenda kama gwaride vitani, hayo mambo yaliishia World War 1 kipindi wanatumia human wave tactics zilivyoanza kutumika machine guns wakawa wanafyekwa.
Na Urusi ndio ina tabia ya human wave tactics ndio maana vifo vyake vinavyotokana na mapigano kwenye WW 2 ni vingi kuliko Marekani+ Uingereza+ Ufaransa. Hata hapa Ukraine kuna muda ilitaka ifanye hivyo. Japan ilishaacha mara moja huo ujinga wa kamikaze na kujitoa mhanga.
Kadri ya miaka inavyoenda ndio vifaru vinazidi kuwa salama. Best tankers wenye kills nyingi waliishia WW2 ndio ulikuwa unakuta jeshi lina vifaru 10,000 sasa hivi kama Ujerumani hata 500 havifiki.

Urusi inachotakiwa kuzingatia ni combined arms ambayo inahitaji budget kubwa na makamanda huru sio mambo ya kubebana na misafara mnaitafuta Kyiv, zile ni siasa jeshi huru hulipeleki vile. Jeshi unalipeleka vitani ila unalidanganya kwanza eti mnaenda kwenye mazoezi hata kujipanga vizuri wanashindwa.

Kwenye ndege, WW2 zilitengenezwa ndege maelfu na makumi elfu na ziliharibiwa nyingi ingawa hazikuwa za gharama kubwa kama leo hii. Hata fighter aces karibia wote tulionao ni wa WW2 wengi Wajerumani. Marekani pekee iliipa Urusi ndege zaidi ya 14,000 (elfu kumi na nne sijakosea) kwenye lend lease ili ipigane na Hitler. Sasa miaka hii utaona ambavyo airforces zina ndege chache na ndege zina survivability kubwa huku zikiwa ghali.

Urusi inapoteza ndege kwa matatizo yake yaleyale. Ukraine ndege zake ni outdated kwa level za Urusi, kina Mig-29 na Su-27 za miaka ya 1970 zisizo na upgrades. Wakati Urusi inazo Su-30 na upgrades zake Su-30MK2, inazo Mig-35, Su-35 zote hizi zinazidi ndege za Ukraine uwezo. Urusi ilitakiwa ifanye SEAD na iharibu airbases na runways za Ukraine lakini ndio hivyo tena precision weapons wanazidunduliza. Waulize Israel wanazuiaje ndege za adui zisiguse anga lao.

Kizazi hiki ni muda ambao fighter pilot ana survivability kubwa angani kuliko miaka ya nyuma. Kuna hata ejection seat na AEW. Kwenye helicopters uko ndio kidogo hazina maisha sana hiyo ndio suicide yenyewe. Ukipanda juu unakutana na AD systems ukija anga la wastani unakutana na MANPADS. Hapo anayesalimika ni aliyetengeneza helicopter yenye countermeasures nzuri zaidi kama flares, chaff na electronic means

Na sasa drones zinazidi kuongezeka, kuanzia 2030s tutaanza kuwa na drones zikiwa integrated na manned fighter jets kwenye 6th generation fighter jets. Kwa sasa ndege kama F-35 zinatengenezewa drones rafiki ambazo zinabebwa na airlifter kama C-5 Galaxy zinaachiwa angani kisha datalink inaziunganizha na F-35 ya karibu iziongoze. Ziko expendable na zinatumika kama chambo. Picha ni rendering, project iko njiani

Manned fighter jets zitaendelea kuwepo.
 
Nikifikia hapo ndo naamini mabeberu wanafanya mambo yao kwa uhakika! Siku za mwanzo kabisa za uvamizi wakati wengi tuliamini ni OP za siku chache tu maana kwa mizani Russia vs Ukraine ilikuwa ni Dimbwi na Bahari, tuliamini ndani ya siku chache tu mchezo utakuwa umekwisha mabeberu wenyewe walisema vita itaenda zaidi ya miaka 5 wengi tuliona ni utani lakini sasa mambo yote yako wazi
 
mrusi Anavuna alicho panda!
Halafu Mtz yeyeto anae ishabikia russia hajui kitu mbaya aliyotufanyia mrussi wakati iddi amin alipo tuvamia na kuzuka vita ya Kagera!
[emoji116][emoji116]
mrusi alimsaidia idi amini kwa kumuuzia ndege vita na kutupa masharti magumu tulipo muomba atuuzie heat seeking missiles ambazo zilituishia!
Kukosa Hekima ya nyerere Kuomba msaada wa Anti aircraft Missiles Msumbiji na Algeria na wao kutusaidia amini angeendelea kutamba mwanza na ndege zake!; vita ingekuwa endelevu na kuwa fursa kwa mrusi ili Iweze kuuza silaha zake [emoji56][emoji15]
 
Supersonic fighter jet hazishambuliwi na kitu. Kuna ndege zina speed kuliko mabomu yenyewe. Na zina presicion kubwa kushambulia
Zikirudi kushambuli uwanja ukilipuliwa zitatua wapi??[emoji101][emoji101]
 
Supersonic fighter jet hazishambuliwi na kitu. Kuna ndege zina speed kuliko mabomu yenyewe. Na zina presicion kubwa kushambulia
Hakunaga anti aircraft missile ambayo ni subsonic, zote ni supersonic tena Mach 3 na ziada hadi 4. Interceptors zinazidi ndege kwa speed na hakuna ndege inaweza outrun the missile ukiachana na SR-71 Blackbird ya Marekani inayoenda sustainable flight ya Mach 3 na point ila wanasema zimestaafishwa (ziko in good shape, anytime wanaweza zitumia).

Ndege kibao supersonic za Urusi zimeangushwa hapo Ukraine
 
kwa muonekano Russia kakutana na chuma ya pua aliingia kichwa kichwa , waafrika tujifunze kisaidiana kama ulaya sio wachambuz uchwara wa siasa za ulaya wakati jiran drc anawaka moto ila tupo kimya mpk USA awape ela ndo mkasaidie maiiran
Waafrika tutakapa acha wizi,ufisadi ikiwa ni matokeo ya tamaa,ulafi,na upungufu wa uelewa wa nini tunacho hitaji kama mtu mmoja mmoja,jamii au taifa.Ndio tutaweza kuona upo umuhimu wa kufanya mambo kama ya kitaifa na sio kama mtu mmoja mmoja 🤔
 
urusi huvamia majiran zake na hii sio mara ya kwanza , hata ukraine alivamiwa 1945 pia wakataka ivamia 1990s pia 2014 na 2022 Sio kila kitu cha kulaumu mabeberu
Vipi kuhusu marekani huko libya na iraq hayo ya juzi tu hapo......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…