Mleta mada hivyo vifaru vitaendelea kuwepo vitani miaka zaidi ya 100 ijayo. Kama unataka kuondoa armour basi tuambie movement ya wanajeshi itakuwa supported na nini. Wanajeshi hawatoenda kama gwaride vitani, hayo mambo yaliishia World War 1 kipindi wanatumia human wave tactics zilivyoanza kutumika machine guns wakawa wanafyekwa.
Na Urusi ndio ina tabia ya human wave tactics ndio maana vifo vyake vinavyotokana na mapigano kwenye WW 2 ni vingi kuliko Marekani+ Uingereza+ Ufaransa. Hata hapa Ukraine kuna muda ilitaka ifanye hivyo. Japan ilishaacha mara moja huo ujinga wa kamikaze na kujitoa mhanga.
Kadri ya miaka inavyoenda ndio vifaru vinazidi kuwa salama. Best tankers wenye kills nyingi waliishia WW2 ndio ulikuwa unakuta jeshi lina vifaru 10,000 sasa hivi kama Ujerumani hata 500 havifiki.
Urusi inachotakiwa kuzingatia ni combined arms ambayo inahitaji budget kubwa na makamanda huru sio mambo ya kubebana na misafara mnaitafuta Kyiv, zile ni siasa jeshi huru hulipeleki vile. Jeshi unalipeleka vitani ila unalidanganya kwanza eti mnaenda kwenye mazoezi hata kujipanga vizuri wanashindwa.
Kwenye ndege, WW2 zilitengenezwa ndege maelfu na makumi elfu na ziliharibiwa nyingi ingawa hazikuwa za gharama kubwa kama leo hii. Hata fighter aces karibia wote tulionao ni wa WW2 wengi Wajerumani. Marekani pekee iliipa Urusi ndege zaidi ya 14,000 (elfu kumi na nne sijakosea) kwenye lend lease ili ipigane na Hitler. Sasa miaka hii utaona ambavyo airforces zina ndege chache na ndege zina survivability kubwa huku zikiwa ghali.
Urusi inapoteza ndege kwa matatizo yake yaleyale. Ukraine ndege zake ni outdated kwa level za Urusi, kina Mig-29 na Su-27 za miaka ya 1970 zisizo na upgrades. Wakati Urusi inazo Su-30 na upgrades zake Su-30MK2, inazo Mig-35, Su-35 zote hizi zinazidi ndege za Ukraine uwezo. Urusi ilitakiwa ifanye SEAD na iharibu airbases na runways za Ukraine lakini ndio hivyo tena precision weapons wanazidunduliza. Waulize Israel wanazuiaje ndege za adui zisiguse anga lao.
Kizazi hiki ni muda ambao fighter pilot ana survivability kubwa angani kuliko miaka ya nyuma. Kuna hata ejection seat na AEW. Kwenye helicopters uko ndio kidogo hazina maisha sana hiyo ndio suicide yenyewe. Ukipanda juu unakutana na AD systems ukija anga la wastani unakutana na MANPADS. Hapo anayesalimika ni aliyetengeneza helicopter yenye countermeasures nzuri zaidi kama flares, chaff na electronic means
Na sasa drones zinazidi kuongezeka, kuanzia 2030s tutaanza kuwa na drones zikiwa integrated na manned fighter jets kwenye 6th generation fighter jets. Kwa sasa ndege kama F-35 zinatengenezewa drones rafiki ambazo zinabebwa na airlifter kama C-5 Galaxy zinaachiwa angani kisha datalink inaziunganizha na F-35 ya karibu iziongoze. Ziko expendable na zinatumika kama chambo. Picha ni rendering, project iko njiani
Manned fighter jets zitaendelea kuwepo.