Ni ujinga wa smz tu kuendelea kununua umeme ghali zaidi kutoka huko, hata kenya wangewauzia kwa bei nafuu au kuanzisha vinu vyao vya kuzalisha umeme, hakuna bidhaa Zanzibar wanaipata bure kutoka Tanganyikani, soko la bara linaimarika kwa sababu wazanzibar wananunua bidhaa mbali mbali za chakula kutoka huko, Tanganyika inaneemeshwa ni zanzibar ndio mana likija suala kuvunja muungano huu na kuleta mpya mnapinga zaidi upande huo.Hayo ni matusi kwa Tanganyika. Umeme mnapewa bure. Nafaka zote Tanganyika, Mifugo ya nyama Tanganyika. Ardhi yetu mmeipora. Tanesco wakizima tu umeme wewe hicho kiswaswadu chako kinazima.
Zanzbar ndio nchi pekee duniani ambayo wananchi wake wanalipishwa kodi mara 2, kodi ya kwanza wananchi wanalipa ZRA lakini nyengine ni TRA, makusanyo ya TRA zanzibar hainufaiki na hata shilingi moja zote zinakusanywa na kuletwa huko ili muweze kulipana mishahara yenu na shughuli zenu za maendeleo.