Mkuu, watutsi ni moja ya makabila yaliyomo nchini Tanzania.
Watutsi wamekuwepo hapa nchini hata kabla ya Tanzania kuzaliwa kama nchi mwaka 1961. Wamekuwepo kwenye dola la Bunyoro Kitara, wamekuwepo kwenye dola la Chwezi, na wamekuwepo chini ya Lumanyika kama Wanyankole na Wanyambo.
Kubwa zaidi dola la Waha ambalo ndilo lilikuwa kubwa ukanda huu (The Buha Kingdom) lilikuwa na wakina Mwami waliokuwa na asili ya Kitutsi. Watutsi wengine walikuwa ni wafanyakazi wa machifu wa Kinyamwezi ambao ndiyo walikuwa matajiri zaidi ukanda huu wote wakiwa ni wakulima wakubwa, wafugaji, wawindaji na wafanyabiashara wa pembe za ndovu. Watutsi waliajiriwa kama wachunga ng'ombe wa machifu kama Mirambo na Isike.
Hivyo sioni dhambi yoyote wala shida ya Watutsi kushika nafasi kubwa serikalini, kwasababu ni watanzania. Tena kuna wengine ni waungwana mno na wamelitumikia taifa hili kwa uzalendo mkubwa tu. Watutsi wako Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na Congo, japo hawaongei lugha moja. Kilichofanya Watutsi wa Tanzania wasiwe kama watutsi na Uganda, Burundi, Rwanda na DRC, ni sheria mbili ambazo ni: Chiefs (Abolition of Office: Consequential Provisions) Act of 1963 na The Nyarubanja Tenure (Enfrenchasiment) Act of 1965.
Hizi sheria zilivunja matabaka ya kikabila yaliyokuwepo kanda ya Ziwa na kubadilisha mfumo zima wa umilikaji mali. Kule Rwanda, Burundi na Kigoma, Ututsi na Uhutu vilikuwa ni Social Classes, tofauti na wengi wanavyotuaminisha. Kwamba Mtutsi alikuwa ni mtu yoyote yule mwenye mali kama ng'ombe na ardhi, huku Mhutu akiwa ni mtu yoyote asiye navyo. Ndiyo maana mtu alikuwa anaweza kutoka kuwa Mhutu, hadi kuwa Mtutsi kisa mali.
Tanzania tuliufuta huu upuuzi mapema kabisa, na mali zote zikawa na Ummah na tukapeleka watu kwenye vijiji vya Ujamaa kinguvu na kuwachanganya watanzania wote. Shule za kidini ambazo zilikuwa zimetengenezwa kwa lengo a kuelimisha watoto wa machifu zikataifishwa na nchi ya Tanzania ikaanza kupona taratibu wakati wengine kama Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya wakikabana makoo.
Sasa, haya yanayotekea sasa hapa ni kitu kitaalamu, muingereza Professor Roger Griffin anakiita Palingenetic Ultranationalism, ambapo taifa, jamii au kabila fulani ili kujijenga kisiasa linatafuta hadithi (A Unifying Myth) kwamba wao hapo kale walikuwa ni watu fulani wakubwa na mashughuli lakini baadaye, jamii yao ikapoteza huo umashughuli, hivyo sasa inabidi waungane tena ili kufufua jamii yao ya zamani. Kifupi ni siasa za Kifashisti tu, ambazo Mwafrika mjinga anazikumbatia.
Hapa wale wanaojiita Watutsi, wanaanza kuzungumzia dola la Wachwezi ambalo ndilo lilijaa Wahima, japo haliwahi kuwa kubwa kama wanavyotaka kusema. Wanasema maeneo yao yote yanaanzia Uganda, Tanzania kanda ya ziwa, Burundi, Rwanda na Congo, japo kiukweli hakujawahi kuwa na dola la namna hiyo. Hivyo ni siasa za kifashisti tu, kama zile za Adolf Hitler kusema Germans are a Master Race au Wazayuni kusema wao ndiyo binadamu wengine wote ng'ombe.
Bahati mbaya sana, ujinga kama huu huwa unauza sana na wengi hujikuta wameingizwa bila kutegemea na kutoka inakuwa shida. Mfano mzuri kabisa, ni kwamba mgogoro wa DRC kwasisi tunafahamu ni kwamba umeanza hata kabla ya Kagame na Museveni kuzaliwa na hautaisha hata wakiondoka. Paul Kagame hajaivuruga DRC ila anatumia mianya hiyo kujinufaisha. Paul Kagame and Rwanda are not destabilizing DRC, but they just take advantage of the pre-existing conditions.
Huu ugomvi ni wa kimaslahi zaidi kuliko ukabila. Ukabila unatumika kama kigezo tu, lakini zaidi zaidi ni maslahi na madini ya DRC. Ni kama na vita ya Angola 1975-1991, ilikuwa siyo Ukomunisti wala Ubepari, ilikuwa ni madini na maslahi tu, bahati mbaya ukabila ukaingizwa kama moja ya visababishi.
Kuna vijana wa kitanzania, huwa wanatoka kwao Bukoba, Kigoma na Tabora kwenda kabisa kupigana vita DRC wakisema wanalinda watu wao wanaouwawa na wakongo. Hili ni jambo la hatari mno na kipumbavu. Mwaka 2005, vijana wengi wa Kiislamu kutoka Tanzania, walikamatwa Somalia, na wakahojiwa na marehemu Dr Mahiga, wakasema walichukuliwa misikitini na kwenda kupewa mafunzo wakisema kwamba wanapigania dini.
Lakini ukiangalia ukweli vijana hawa walikuwa wameenda kule zaidi zaidi kwasababu za kiuchumi, maana walikuwa wanalipwa na huku nchini walikuwa hawana ajira. Ndilo suala kama hili tulipambana nalo Kibiti mwaka 2017, watu wana maslahi yao lakini wanaamua kutumia mwamvuli wa dini kuingiza vijana wa kiislamu kwenye matatizo yasiyo na kichwa wala miguu mwishowe wakawaponza Waislamu wote wa Wilaya ile ambayo ilifungwa kabisa na mauaji ya kutisha yakaendeshwa na vyombo vya usalama.
Mwaka 2013-2014, ilianza hii minong'ono na Louise Mushikiwabo akamtukana Jakaya Kikwete na kuseme kilekile ambacho CDF alikisema kwamba kuna watu wa nchi jirani wako kwenye nafasi nyeti za serikalini, hivyo hawatatumia nguvu kupigana na Tanzania zaidi zaidi watamwaga fedha. Wajinga wengine wa kule Ngara wakaanza kufurahia, na kilichofuata ni kwamba Wilaya nzima ilizingirwa na Ethnic Cleansing ikaanzishwa kwa kivuli cha Operesheni Kimbunga, kufukuza wahamiaji haramu.
Watu wengi, hasahasa Wanyambo na Wahayo, wakajikuta kwenye Cross-Fire, ya kutaifishiwa mali, mashamba na hata kuuwawa. Watutsi wengi waliokuwepo serikalini wakaitwa na kuanza kufanyiwa Harassment, kwa kivuli cha Security Measures. Kuna wachungaji ni watanzania waliitwa na familia yake nzima na kuanza kuhojiwa, tena siyo mara moja. Kule mpakani wakawa wanafanya kile Trump alikifanya mwaka 2019 kuwatengenisha watoto na wazazi wao. It was a total nightmare.
NAMALIZIA NA MIFANO MIWILI HAI:
Mosi, mwaka 1991, wakati Saddam Hussein anavamia Kuwait, kabila la Bedoons ambao wako hadi Iraq, waliona nchi ya Iraq ndiyo kinawara wao wa kuwarudisha to Former Greatness, waliisaliti nchi yao na kumuunga mkono Saddam Hussein kwenye uvamizi wake haramu wa kumega kipande cha nchi huru. Vita ilipopamba moto na mambo yakawa mabaya kwa Iraq, jeshi la kuwaita likaanza kuchinja Bedoons. Walikuwa wanaenda kijiji baada ya kijiji, na wanaua watu na wengine wakafukuzwa kazi. Vita imeisha tu, serikali ya Kuwait ikawavua uraia Bedoons zaidi ya 50,000 kwa usaliti, mpaka leo wanahangaika.
Pili, wajapani nao hasahasa baada ya kupata maendeleo, hasahasa baada ya kumtandika Urusi (Russo-Japanese War 1905) na Uchina mwaka 1931 (The Invasion of Manchuria) wakaanzisha huu ujinga wa Palingenitic Ultranationalism. Waliamini kwamba wao ni watu wa tofauti, kumbe ni hatua za maendeleo tu ya binadamu ambayo kila jamii hupitia.
Wakajidanganywa mwaka 1941, wakavamia Marekani na kuua watu zaidi ya 2000. Huku wajapani wote waliokuwepo duniani wakishangilia, hasahasa wale waliokuwa ni raia wa Marekani. Kilichofuatia hakikuwa kizuri. Raisi Roosevelt akatangaza Executive Order ambayo ilimtaka kila raia wa Marekani mwenye asili ya Kijapani kufungiwa kwenye A Concentration Camp, kwasababu walionekana wangeweza kufanya uzandiki. Watu zaidi ya 120,000 walikamatwa na kufungiwa ilhali ni raia wa Marekani.
Hili likajirudia kipindi cha Senator McCarthy (The Red Scare), miaka ya 1950's ambaye alifukuza maelfu ya wachina Marekani kwasababu wengi wao walikuwa wanaonesha kuvutiwa mno na sera za kikomunisti za Uchina na kufanya ujasusi na kuhujumu Marekani. Watu wengi walikataziwa kusoma kichina wala kuvaa mavazi ya kichina, huku wengine kama Morris Chang, mwanzilishi wa TSMC wakinyanyaswa sana na kuwekwa Dentention.
====================================================
Kagame na Musseveni wakianzisha ujinga wowote na Tanzania, basi watawaponza watu wengi sana kuanzia Bukoba, Kigoma, Mwanza na Tabora. Kipindi cha vita serikali hutumia Propaganda kuwajaza watu upepo, na moja ya mbinu ni kutumia ukabila kama ilivyokuwa Operesheni Kimbunga, ambayo watanzania wengi walileteana unoko hata mtu na ndugu yake.
Watu kama Bashungwa, Masingilingi, Doto, Mafwele na wengine watapitia kipindi kigumu mno cha kuteswa na kubaguliwa au hata kuhatarisha uhai wao. Vita ya Kagera tu iliwaponza mno Wahaya, baada ya baadhi yao kukamatwa kama majasusi wa Uganda na hakuna anayelizungumzia hili. Wahafidhina kwenye vyombo vya usalama kama kina Mzee Mlawa wakachukulia ni kabila zima, na waliwanyoosha kwelikweli. Ni kwamba tu Mzee Nyerere alikuwa na busara nyingi mambo hayakwenda mlama.