Taarifa zinazotoka kwa CAG kitaalamu huwa tunaziiita AUDIT QUERIES, ambapo kiuhalisia TPDF huwa haifanyiwi ukaguzi, bali MINISTRY OF DEFENSE. Ushawahi kutoka mtafaruku hivihivi kipindi cha Magufuli, ambapo kuna mikataba ilisema TPDF imenunua silaha asilimia 20% tu huku asilimia 80% vikiwa ni vitu vidogo-vidogo (Miscellaneous). Mzee akafura kwelikweli, ila baadae akafahamu kwamba mambo ndivyo sivyo akauchuna.
Yaani kwamba, wewe MTANZANIA wa kawaida, unataka ufahamu Trilioni 1 za TPDF zinaenda wapi kama ambavyo unafahamu fedha za WIZARA YA MAJI ??? Halafu, unaposema Trilioni 1 nzima imepotea napata wasiwasi mkubwa na uelewa wako. Hivi Trilioni 1 unaifahamu kweli ndugu yangu, hadi ipotee kirahisi kwenye mifumo ambayo iko INTERGRATED kama Tanzania ???
Kukupasha tu, kina Robert Msalika Makungu (D-DGIS) walipojaribu kuficha matumizi ya holela ya Trilioni 1 na vijana wake wa TISS, Prof Assad akaiona kirahisi na Msalika ikawa kwisha habari yake. Mnaposema Trilioni 1 ya jeshi inapotea, napata shida mno kuelewa. Maana hiyo hela mpaka likapewa jeshi, kuna mlolongo mzito na mrefu. Nakubali kuna wizi, lakini hela huwa kiwango kikubwa hivyo huwa hazipotei kirahisi, hasahasa kwenye vyombo vya usalama.
Mnapoifananisha Tanzania na nchi jirani na kuikandia pia, napata shida na uelewa wenu. Nani amekwambia kwamba Rwanda na Uganda hakuna rushwa jeshini ??? Caleb Akandwanaho a.k.a Salim Salehe alistaafishwa jeshini na kaka yake Museveni kwasababu ya kupiga pesa ndefu, yeye na wenzake. Hadi Museveni aliona aibu yani. Hapa Tanzania kina General Kombe waliwahi kugusa baadhi ya vipesa na kufanya matumizi ya kiholela, kesho tu mambo yakafika Msasani kwa Mzee Mchonga, kombe akatolewa jeshini na kupelekwa kwingine.
Mwaka 2001, kipindi cha Donald Rumsfield zilipotea USD Trilion 2, ambazo ni sawa na Trillion 6000 za kitanzania kule PENTAGON, na mpaka leo hazijulikanai zilipo, ila mwaka 2019, ikafahamika kwamba vita ya Afghanistan aligharimu USD Trilion 2. So Go Figure.
NB: Nakubali Tanzania kuna madhaifu, na una haki ya kulalamika. Lakini huu ujinga wa kuamini kwamba Tanzania is Abyss while Kenya, Uganda and Rwanda are Paradise huwa unanishangaza mno. Mtu mwenye uelewa atafahamu kabisa kwamba EAC nzima kumejaa mataifua yanayonuka RUSHWA, UJINGA na UMASIKINI, hakuna wa kumcheka wala kumvimbia mwenzake.