Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Izo ni stori zako tu fatilia vizuri utajua wewe mtu unapigana naye unamuuwa alafu unamkamata unamrudisha kwao inakuingia akilini? JiongezeKwa hiyo wajeda wetu walienda kucheza madogoli? Wangelinda vipi amani wakati hata kujilinda wao wenyewe wameshindwa mpaka to the extent ya kukusanywa kama kuku wenye mdondo? Warudi tu waendelee na kazi wanayoiweza ya uchawa kwa Chura Kiziwi.
Tangu kutekwa kwa Jiji la Goma, askari wa SA, Malawi na TZ wapo chini ya Ulinzi na hatawatakiwi kufanya nyweee.Wamerudi wanajeshi 25 tu kutoka Tanzania wengi waliorudi ni kutoka SA na wale majeruhi 5 wengine wamebaki na siraha zao huko Camp hizo tetesi sio za kweli..
M23 wamechukua siraha za Jeshi la DRC na Polisi wao waliojiunga nao..
Brother wewe ni mropokaji,unafaham ni wanajeshi wangapi wa M23 wamepoteza maisha?Waiguse TZ mara ngapi wakati wameua na kujeruhi askari wetu?
Hans Pope aliuwawa mwaka 1972, ndani ya ardhi ya Uganda, jiulize alikuwa anafanya mini uganda?Ona mwehu huyu. Unathubutu kumsifia Amin, wakati Bukoba kuna makaburi ya raia na mkuu Hans Pope wa mkoa akikamatwa na kuuwawa Uganda.
Huna unacho fahamu, kwa nini una andika uongo!!Tangu kutekwa kwa Jiji la Goma, askari wa SA, Malawi na TZ wapo chini ya Ulinzi na hatawatakiwi kufanya nyweee.
Wakijitia jeuri wanakula chuma, na silaha zote walishanyang’anywa
Hiyo ndo vita, Upige au Upigwe…Hapa Tumepigwa na hatuna la kufanya
Kuna jamaa alisema kuna matawi ya CCM hadi huko🤣🤣🤣Tatizo siasa za ccm zimeingia kwenye majeshi yetu, kiasi kwamba ufahari wa majeshi yetu kwa sasa upo kwajili ya kuilinda CCM , kuiba na kukimbia na mabox ya kura na zaidi yale magwaride ya kuwatishia watanzania wakati rasilimali zinaondoka na waarabu.
"Kuna watu wanatudharau na kutuona sisi sio lolote kwa sababu za kijiografia, sijui mara Rwanda ni kainchi kadogo. Ila tu niwaambie watu hao wanajidanganya sisi ni tuko imara na ni wakubwa kweli kweli."'-Paul KagameHivi wajuvi wa mambo aya ebu nisadieni ,hakuna namna au kutafuta sasababu yoyote ya kuifuta Rwanda iwe moja ya sehema za nchi za Afrika mashariki , naona kama msubufu , shida nini kwamba ana nini cha juu kuliko nchi nyingine ndani ya Afrika mashariki?
Hili sipingi na linawezekana kabisa, kama TISS yenyewe tu imejaa UVCCM ambao kazi yao ni kulewa na kutishia watu kwenye mabar na kumbi za starehe, kwanin wapuuzi hao wasiwepo hata kwenye jeshi letu?Kuna jamaa alisema kuna matawi ya CCM hadi huko🤣🤣🤣
Umerudi tena! swali letu hujajibuSeems M23 na Rwanda wana ubinadamu kwa kuwarudisha mateka waliokamatwa nyumbani kwao bila kuwadhuru au kudai chochote, ingekuwa lile jeshi lako la Congo na interahamwe hao wote wangeliwa mshikaki
Dogo kama jambo hulijui kaa kimya. Kupayuka tu hakukusaidii zaidi inatuonesha kuwa wewe ni mjinga na mpumbavu!Mbona linashindwa kutumia nguvu kujilinda lisidhalilishwe na wanamgambo wa M23? Madogo hawa wanaoajiriwa kwa vimemo ndiyo wakapigane na watu wenye experience ya vita? Vita havipiganwi kwa maneno ya mdomoni, on the battlefield is where you show what you got.
Alitekwa, ndani ya ardhi yetu.Hans Pope aliuwawa mwaka 1972, ndani ya ardhi ya Uganda, jiulize alikuwa anafanya mini uganda?
Mbona umeshajibu swali unalouliza! Pengine hujatambua, nikufafanulieKama TZ itajiingiza kwenye huo mgogoro kwa namna yeyote ile inabidi iweke maslahi yake mbele yani iwe imeingia kupata faida na kulinda interest za nchi sio kutafuta sifa za kijinga. Congo imekua kubwa jinga toka ipate uhuru haijui amani ni nini kila siku inapigana tu hatuwezi kuwa saviors kusaidia wasioweza kujisaidia wenyewe.
Komboweni lile ziwa nyasa kwanza liloibiwa na Malawi lakini mkaikombowe na Mombasa kenya maana ni sehemu ya ardhi ya Zanzibar na Tanzania. vita ya uganda mulipigwa push sana ni mataifa kadhaa, nyinyi uhodari wenu ni kupiga watu tu siku za uchaguz labda na kutembea na magari ya maji motoJitekenye tu.mbona rahisi tu mwambieni mme wenu mwingine museveni aungane na m23 na pk wenu mje muichukue Kagera Kama mlivyoichukia goma. Si umesema Kagera siyo Tanzania na imepakana na Uganda na Rwanda saaa kama nyinyi na wanaume sogezeni kwato zenu utaijua vizuri Tanzania maana mnavipele vinawawasha sisi atukuni tunapasua tu
Unaongea ya maana na ya hovyo kwa pamoja. Huwezi kuanzisha vita na kila nchi ya jiranj ukidai mipaka kabla ya uhuru au MGAWANYO wa mkoloni. Ni ukichaa na ukorofi huo na ndicho anachokifanya Kagame. Kutangaza ubabe kwenye uchaguzi uko sahihi, sababu uchaguzi maana yake raia anataka kutoa hisia na maamuzi yake kupitia sanduku la kura. Kumpiga, kukimbia na kura zake kwenye masanduku, na kuzuia uwazi (observation) au kutangaza mshindi hewa ni ukatili kwa demokrasia.Komboweni lile ziwa nyasa kwanza liloibiwa na Malawi lakini mkaikombowe na Mombasa kenya maana ni sehemu ya ardhi ya Zanzibar na Tanzania. vita ya uganda mulipigwa push sana ni mataifa kadhaa, nyinyi uhodari wenu ni kupiga watu tu siku za uchaguz labda na kutembea na magari ya maji moto
Vita ya uganda mulipata msaada toka mataifa ya nje likisaidiana na jeshi la zanzibar taja vita vingineMimi najua HISTORIA ya nchi yangu. Ndiyo maana nimekwambia Nyerere kazaliwa kayakuata makanisa .Sasa Sasa unasemaje alisimika kanisa. wewe Utalopoka sana tu kwa kutokujua lolote sifia au mabwana zako na huo udini wako wa kipumbavu. Lakini iddi amini alileta za kuleta kapewa za huo za jeshi tiifu kabisa JWTZ. m23 yako hiyo haiwezi kufanya chochote kwa Tanzania hii. Mtapigwa Kama ngoma. Sasa ffu toka waliwatoa mbio mapoli ya kigoma na Kagera mkarudi Rwanda mbio sembuse JWTZ.
Niliwahi sema wanajeshi ni wale waliostaafu.siku hizi kuna vijana wameingia jeshi ili tuu kuringia baka baka akivaa mtaani kwenye weledi wa kazi mbinu ya kivita na uzoefu bado sanaNajua habari hii imewauma sana makamanda ninawafahamu wa JWTZ!
Najua habari hii imemuua sana kamanda Luteni Generali Mstaafu Mwakibolwa. Najua habari hii imemsononesha sana General Mstaafu Davis Mwamunyange. Najua habari hii haijamlaza vizuri mwamba Luteni General Abdulrhman Shimbo.
What we use to know as Tanzania Pride iliyokuwa inabebwa na Jeshi letu la Wananchi (Tanzania People's Defence Forces) imefikia tamati baada ya wanajeshi wetu kudhalilishwa huko Rwanda kwa kusubilishwa kwa masaa mpakani na Wanajeshi (Mamlaka za Rwanda).
Wanajeshi wetu waliosubilishwa mpakani ni sehemu ya majeruhi wa vikosi vya SADC waliopokea kichapo kutoka kwa Wanajeshi wa Rwanda na Washirika wao M23.
Inasemwa pia Wanajeshi wetu kama sehemu ya wanajeshi wa SADC wamenyang'anywa silaha zao na wanamgambo wa M23 na kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Hawawezi fanya chochote bila ruhusa ya M23.
Itakumbukwa hadi miili ya Wanajeshi wetu waliouwawa bado haijarudishwa na inawezekana jamaa wanatuwekea ngumu ili tuendelee kuwalamba miguu na ili watuoneshe kuwa sasa wao ndo mabwana zetu kivita.
Naumia sana Nchi yangu kufikia hapa. Naumia sana Jeshi langu JWTZ kufikia kudhalilishwa hivi.
Kuna haja ya kujitafakari na kuanza upya. CCM ni janga.
View attachment 3249000
=======
Takriban wanajeshi 200 wanaohitaji wakihitajihuduma ya matibabu wakiwemo wale wa Afrika Kusini, Malawi na Tanzania walioko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa ujumbe unaojulikana kwa jina la SAMIDRC waliondoka Goma na kuvuka mpaka na kuingia Rwanda kuelekea Kigali kwaajili ya kupata ndege za kuwarejesha makwao.
Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini alitangaza wikendiiliyopita kwamba wanajeshi wao waliojeruhiwa katika mapigano na M23 nchini DRC wataanza kurejeshwa makwao wiki hii.
Donatien Mugabo, mkazi wa Gisenyi nchini Rwanda,ambaye ameshuhudia magari yaliyokuwayamewabeba askari hao yakiondoka mpakani kwa upande wa Rwanda, ameiambia BBC kuwa walikuwa kwenye mpaka huo kwa saa kadhaa.
![]()
Walifika mpakani Jumatatu saa sita mchana, na waliondoka mpakani baada ya saa kumi na mbili jioni, Donatien anasema.
Haijabainika ni nini kilisababisha wacheleweshwe mpakani.
Vyombo vya habari vya Goma - jiji linalodhibitiwa na M23 na nchini Rwanda vilipigwa marufuku kupiga picha au kuzungumza na wanajeshi, kama ilivyokuwa wakati mamluki wa Ulaya walipoondoka Goma kupitia Rwanda.
Magazeti ya Rwanda yanaripoti kuwa wanajeshi 129 wanatoka Afrika Kusini, 40 kutoka Malawi na 25 kutoka Tanzania.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi walikotoka askari hao hawajazungumzia kuachiliwa kwa askari hao wanaotajwa kuhitaji matibabu.