Sasa walienda kufanya nini?Askari wa US si ndio walikimbia kama kuku kule Afghastan? DRC sio nchi yetu hakuna haja ya kuua vijana wetu kutafuta SIFA
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa walienda kufanya nini?Askari wa US si ndio walikimbia kama kuku kule Afghastan? DRC sio nchi yetu hakuna haja ya kuua vijana wetu kutafuta SIFA
Wewe mkuu umekaririshwa na kushibishwa propaganda za wanasiasa zisizo na uhalisia wowote.Huwezi ingia Vita kiholera kisa mtu ameamua kukufanyia kebehi. Nchi yetu ( Tanzania) ni makini sana na hata Sasa itaangalia ila kama watahitaji watuchokoze na expansionism yao nao watajua hawajui. Askari lazima uwe mvumilivu hapo wamefanya kutupa zoezi Wala hakuna walicho Fanya Cha maana sana. Watadhani kuwa hatuna nguvu ila ni nani aliewahi toa nguvu halisi kwenye shughuli za kikanda bali ni fursa Fulani ya kusoma mazingira na kuona kama watatujia Nini tujihami.
Watanzania imefikia hatua tunaishi kwa mihemko kwenye mambo nyeti.
Please tuwe makini na tutoe taarifa za watu wasio watanzania(wahamiaji haramu) waliomo nchini ili kuendelea kuimarisha nchi yetu.
Tusibezane kiasi hiki hata familia Yako ukiwa wa kulialia jua huwezi kuwa imara.
Hili swali zuri, walienda kulinda amani ya DRC wananchi wawe salama kabisaa, shida SADC hawako serious sehemu ya kuleta jeshi la watu 5000, wewe unapeleka watu 1300 hata nusu ya matarajio hujafikia vip unaweza fikia malengo? watu ni muhimu kwenye uwanja wa vita ndio maana Urusi anakwenda kuomba Korea Kaskazini na Ukraine amefungua mlango kwa yeyote anaetaka duniani kuja pamoja na kushusha umri wa kuanza jeshini ili kupata watu wengiSasa walienda kufanya nini?
Tatizo ni ulimbukeni wa chama unakusumbua hivyo unadhani kila mtu ni limbukeni wa vyama vya siasa. Akili inayoongozwa na bendera hawezi kuwa na utimamu.Hamna kitu.
Chombo mojawapo ni Idara ya Uhamiaji ambayo inakampeni inayowashirikisha wananchi kutoa taarifa. Watanzania kasumba ya kama halijakupata hujishughulishi nalo litatulea madhara sana.Wewe mkuu umekaririshwa na kushibishwa propaganda za wanasiasa zisizo na uhalisia wowote.
Jambo la kuchunguza wahamiaji namna unavyolieleza kirahisi rahisi inashangaza.
Serikali ina vyombo vyake kufuatilia wahamiaji haramu na ndivyo vinavyotoa hadi vitambulisho vya uraia.
Je raia wa kawaida ana uwezo wa kutress na kutambua na kisha kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere?
Emb kuwa seriou basi.
Bado sana kumpa hiyo nafasi.
Jeshi letu lilienda kwa mgongo wa UN, Monusco na SADC.
Wajuvi mnajua wazi ukienda kwa mwavuli tajwa hapo juu ni sawa na umefungwa mkono mmoja.
Hauko kwenye mapigano ya moja kwa moja zaidi ya kujihami mnaposhambuliwa.
Pili.
Tulipeleka kikosi kidogo tu hivyo naona wengi tunachangia kimhemko
Ningekuwa Rais ningemrudisha huyu mzee awe CDF saiviMwisho wa Pride,
View attachment 3255696
Kwa hiyo wale wazanzibari wa humu jukwaani kina dega Gavana wanaotuambia kilichotokea huko visiwani mwaka 1964 ni mavamizi ya Tanganyika na sio mapinduzi huwa wanatudanganya ?Wewe umezaliwa juzi, Zanzibar ilikuwa na jeshi lake na ndilo waliofanya mapinduzi ya 64, Zanzibar walikuwa na kiti umoja wa Mataifa, Zanzibar walikuwa fedha zao, passport na mpaka mabalozi, na Zanzibar ndio waliotoa fedha nyingi zaidi kuliko Tanganyika kuanzisha hiyo Benki Kuu yenu huko Tz bara, hiyo BOT ni ya ushirika lakini Tanganyika walipora haki ya Zanzibar. wewe upo upo tu hujui chochote
Huyu jamaa kwa Sasa anafanya atakalo kwa nchi yeyote na hakuna wakumzuia.Duh hivi ina maana Kagame ndio mbabe rasmi wa kivita hapa Afrika Mashariki, kusini na kati?
Inategemea anamfanyia nani?Huyu jamaa kwa Sasa anafanya atakalo kwa nchi yeyote na hakuna wakumzuia.
Unadhani PK alikua anaropoka hovyo alipo sema We're not the same old idiots you dealt with 50 years ago,' that resonated far beyond Kigali.”Najua habari hii imewauma sana makamanda ninawafahamu wa JWTZ!
Najua habari hii imemuua sana kamanda Luteni Generali Mstaafu Mwakibolwa. Najua habari hii imemsononesha sana General Mstaafu Davis Mwamunyange. Najua habari hii haijamlaza vizuri mwamba Luteni General Abdulrhman Shimbo.
What we use to know as Tanzania Pride iliyokuwa inabebwa na Jeshi letu la Wananchi (Tanzania People's Defence Forces) imefikia tamati baada ya wanajeshi wetu kudhalilishwa huko Rwanda kwa kusubilishwa kwa masaa mpakani na Wanajeshi (Mamlaka za Rwanda).
Wanajeshi wetu waliosubilishwa mpakani ni sehemu ya majeruhi wa vikosi vya SADC waliopokea kichapo kutoka kwa Wanajeshi wa Rwanda na Washirika wao M23.
Inasemwa pia Wanajeshi wetu kama sehemu ya wanajeshi wa SADC wamenyang'anywa silaha zao na wanamgambo wa M23 na kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Hawawezi fanya chochote bila ruhusa ya M23.
Itakumbukwa hadi miili ya Wanajeshi wetu waliouwawa bado haijarudishwa na inawezekana jamaa wanatuwekea ngumu ili tuendelee kuwalamba miguu na ili watuoneshe kuwa sasa wao ndo mabwana zetu kivita.
Naumia sana Nchi yangu kufikia hapa. Naumia sana Jeshi langu JWTZ kufikia kudhalilishwa hivi.
Kuna haja ya kujitafakari na kuanza upya. CCM ni janga.
View attachment 3249000
=======
Takriban wanajeshi 200 wanaohitaji wakihitajihuduma ya matibabu wakiwemo wale wa Afrika Kusini, Malawi na Tanzania walioko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa ujumbe unaojulikana kwa jina la SAMIDRC waliondoka Goma na kuvuka mpaka na kuingia Rwanda kuelekea Kigali kwaajili ya kupata ndege za kuwarejesha makwao.
Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini alitangaza wikendiiliyopita kwamba wanajeshi wao waliojeruhiwa katika mapigano na M23 nchini DRC wataanza kurejeshwa makwao wiki hii.
Donatien Mugabo, mkazi wa Gisenyi nchini Rwanda,ambaye ameshuhudia magari yaliyokuwayamewabeba askari hao yakiondoka mpakani kwa upande wa Rwanda, ameiambia BBC kuwa walikuwa kwenye mpaka huo kwa saa kadhaa.
![]()
Walifika mpakani Jumatatu saa sita mchana, na waliondoka mpakani baada ya saa kumi na mbili jioni, Donatien anasema.
Haijabainika ni nini kilisababisha wacheleweshwe mpakani.
Vyombo vya habari vya Goma - jiji linalodhibitiwa na M23 na nchini Rwanda vilipigwa marufuku kupiga picha au kuzungumza na wanajeshi, kama ilivyokuwa wakati mamluki wa Ulaya walipoondoka Goma kupitia Rwanda.
Magazeti ya Rwanda yanaripoti kuwa wanajeshi 129 wanatoka Afrika Kusini, 40 kutoka Malawi na 25 kutoka Tanzania.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi walikotoka askari hao hawajazungumzia kuachiliwa kwa askari hao wanaotajwa kuhitaji matibabu.
Israel aliwatandika Hezbollah na jeshi la kulinda amani la UN lipo pale pale, hawa watu sio sehemu ya jeshi la nchiSasa kama jeshi linajua limefungwa mkono mmoja lilienda huko kufanya nini, kutalii?
Nenda ukatafutw hqbari, jeshi lipo goma peke ni 1300 kwa camp moja, ila hawa wana camp 3 ndani ya Muji goma, kwa hio unasema jeshi 5k hawapo? South African wametuma 2900, Tanzania na Malawi wakatuma 2100.Umeelewa nilicho andika? Malawi, Tanzania na South Africa hawa ndio walikubali kupeleka wanajeshi wao , jumla ya wanajeshi waliotakiwa kwenda ni 5000 tu, ila mpaka kufika january walikwenda 1300 sasa unawezaje kuzuia M23 na jeshi la Rwanda? hao Burundi wanashida kibao sio sehemu ya kikosi cha Sadc kule DRC