Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua

Kondoo wanaabdaliwa kisaikolojia Ili watapeliwe kwa kishindo. Ajabu serikali inajua Hawa ni matapeli na wanawahujumu na kuwafilisi wananchi lakini inatazama pembeni wananchi wakamuliwe vizuri.
 
Amen...

Ungeambatanisha na clip ingekuwa vyema sana.
 
Mkuu Rabbon nina swali,
1. Hivi mbingu zipo gapi?
2. Mtu/ binadamu akifa na kama ameenda mbinguni je huwa wanakuwa mbingu ya gapi?

3. Mtu/binadamu akifa na ikiwa amepata neema ya kuingia mbinguni kabla ya ufufuo je huko mbinguni roho za wanadamu huwa zinapewa mwili tofauti na huu wa duniani au huwa zipo katika mwonekano upi?

4. Yesu Kristo aliwahi kusema, watu watakapofufuliwa wale watakao kuwa mkono wa kuume watakuwa kama malaika, maana malaika hawaoi wala kula huko nk nk, kwa nini tena kwenye ufunuo wa Yohana kuna sehemu inasema watakaoingia mbinguni watakula karamu na mwana kondoo, je inawezekanaje mbinguni kula wakati watakuwa Km malaika, kuna kula tena mbinguni?
 
Watu wanapata mauza uza afu wanajihisi wamefika mbinguni.

Ingekua rahisi hivo, Basi mateja wote wangemwona yesu maana wao kuona mauza uza ndo jadi Yao
 
Zuma riidi ni Pepo katika form ya mwanadamu,

Fuatilia hata Kuzaliwa kwake, kulikuwa tofauti mamaye ameeleza vyema,

Kuhusu majengo marefu hata kuzimu kavu, yapo.

Lakini pia Mbingu ni halisi IPO.
Huyu Zumaridi wa Mwanza mkuu ndiyo nifuatilie uzaliwa wake. Kama hutajali naomba nipate stori zake za kuzaliwa.
 
halafu haya mambo ya imani mkuu inabidi uwe mjinga na mpuuzi
ila ukiingiza tu akili za darasani lazima upigwe mtama
 
Ingia U-tube,

IPO video mamaye akielezea Kuzaliwa kwake.
Mkuu fanya km unafanya assignment ya Maths unafanya huku unaongea ongea. Nina maana km unaweza andika km huwezi anzisha uzi tuelewe.
 
Swali no 3.

Malaika Hawaii Kweli Wala kuolewa.

Lakini Malaika wanakula na kunywa,

Mbinguni Kuna kula na kunywa, na Kuna vyakula vya Kila aina,

Imeandikwa pia yapo maji na mtu wa Uzima, na matunda yapo nk nk.

Kuna kula ila hakuna vyoo. Miili ya kule miili kama ya Malaika ni tofauti na hii tuliyonayo.

Mbinguni Kila mtu ana nyumba yake, na Malaika ndio watatuhudumia, sisi tutakuwa na rank ya juu Mbinguni kuliko Malaika. Kushinda majaribu ya Dunia Si KAZI ndogo,nitajibu swali Moja Moja πŸ™
 
Na huyu naye ameanza kutoa kauli za kina Zumaridi?
 
Ni kweli wapo watakaookolewa kwenye dhiki kuu na ni wengi ila kama maandiko yanavyoonyesha kwenye kitabu cha ufunuo kuokoka kipindi hicho itakuwa ni kwa shida sana maana imagine huwezi kuuza wala kununua ina maana hakutokuwa na ajira kwa urahisi kwa watakaokoka hasa ile miaka 3.5 ya mwisho then hata kama ukitaka kufanya biashara si rahisi maana haupo linked na global antichrist digital financila system.

Halafu heri ni wale watakaokuwa wamenyakuliwa na ndio ambao wataingia karamuni mwa Yesu miaka 7, wanarudi duniani na miili ya utukufu kumpiga vibaya sana mpinga kristo na majeshi yake na kutawala dunia na miili hiyo ya utukufu.
Ndiyo maana ni vizuri sana kwa mwamini kukesha kwa maana ya kuwa tayari wakati wowote maana aliyeokoka na akaukosa unyakuo ni hatari sana kwake.
 
Hebu leta ushahidi kuwa huko ulikoenda wewe ndiko mbinguni alipoenda Mwakasege
Pima kupitia BIBLIA neno la Mungu,

Hayo niliyoona na aliyoona Mwakasege yameandikwa au hayamo ndani ya BIBLIA.
 
Aamen

Ubarikiwe πŸ™
 
Ukristo sio dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…