Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua

Dini ingelikuwa na kanuni kama za kisayansi, hakuna kiumbe ambaye angelipotea.

Lakini 'wajasiria dini' na makanisa ya manabii wa uongo yanayoibuka kama uyoga kila uchao ndiyo kikwazo kikubwa sana cha great thinkers na pingamuzi kuu la binadamu.

Tupo tunaomwamini Mungu na kumkiri masiya Yesu kristo kwamba yuhai na mafundisho yake ni halisi.

Lakini mfumo mliotuletea wa sadaka sijui matoleo ya kausha damu ili kuboresha maisha yenu, tunamwachia Mungu mwenyezi ndiye muamuzi wa haki.

Sitafuata maelekezo wala mafundisho kutoka midomoni kwa nabii wala mitume, kwa sababu najua kusoma na kuandika, nitasoma miongozo mwenyewe kutoka biblia na vitabu vya ritrujia kuliko kulishwa matango pori na kupoteza muda na rasilimali kwa matapeli.

Mnaoyaamini hayo na ngonjera zao, endeleeni na kusoteshwa.
 
Nawasihi watu wangecoment kabla ya kusoma comment za wenzao maana wazo la kwanza kukujia mara baada ya kusoma Uzi huu ndo upande ulipo kiimani, Mungu ni Alfa na Omega
 
Tofauti Mohammad alikuwa ni mtume na hakuna mtume baada yake hawa wengine ni wahuni ...
 
Huu ni muemdelezo wa story ile ile ya ZUMARIDI na GeorDavie!

Kiufupi ni small time talk kwa ajili ya small minds! Mind candy for the fools!
 
Ile ya zumaridi ilikuwa kali zaidi. Manake yeye aliokuwa anaenda na kurudi Kila siku hadi anaelezea muundo wa maghorofa ya mbinguni yalivyo huko. Tena yeye aliokuwa anaenda live sio katika roho kama hao wengine
Hadi nani sijui akataka kumuoa sijui Paulo sijui nani 🙌
 
Dah! "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" si maneno yangu ni ya MUNGU mkuu
 
Tofauti Mohammad alikuwa ni mtume na hakuna mtume baada yake hawa wengine ni wahuni ...
1. Nani alimpa mamlaka ya kujiita mtume wa mwisho?
2. Je, unaamini Mohammad alipaa na farasi mwenye mabawa kwenda Al Aqsa?
 
Hawajawahi kukutana huko mbinguni .. ila sababu zumaridi anaenda mara kwa mara awaulize wenzie kama washafika huko ..
Haha............ wametuona wakuja hivyo kuendelea kutudanganya kila Siku

Hiyo hukumu ya Mungu na ishuke ili tuone mwisho wa hawa manabii wa uongo 🙌
 
Yeye Musa alimtambuaje km ni yeye wakati hata picha yake halisi hatuijui, Musa kwa mujibu wa bible alizaliwa karne za kale, hivi kwann hawa wachungaji ni waongo waongo sana..!!?

Haya atueleze mbinguni kukoje? Umeme upo au ndo wanatumia mwanga wa jua??
 
Swali no 3.

Miili ya WATAKATIFU ni kama aliyoonekana nayo Musa na Elia au Ule mwili alipofufuka nao Yesu.

Ni mwili kama kioo, hazuiliki, inapita popote ni mwili wa kiroho.
Kwani Mussa na Eliya walipomtokea Kristo Yesu, Biblia ilitoa ufafanuzi timilifu wa namna miili yao ilivyokuwa?
Au ilisema tu Mussa na Eliya walitokea na Petro akasema wajenge vibanda vitatu au?
 
Kwani nimesema walitoka kaburini?Roho zao zipo mahali ili siyo Mbinguni. Mpaka ufufuo ndipo watakwenda Mbinguni na miili mipya.

Usiwe na haraka twende polepole.
Hapo Mahali ni wapi?

Mimi nasema wapo Mbinguni sababu zinathibitika Kwa neno lisemalo BWANA atakuja pamoja na WATAKATIFU wake.

Aliko Yesu na ndiko waliko wamwaminiye .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…