Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Dini ingelikuwa na kanuni kama za kisayansi, hakuna kiumbe ambaye angelipotea.Heri wewe mwenye kuandika haya hakika unyakuo ni wakati wowote endelea kuwa safi maana kufumba na kufumbua unyakuo utatokea na watakaobaki duniani ile miaka 7 ya dhiki kuu itaanza rasmi na wapo watakaokuwa wanarudia kusoma tunayonadika hapa mara kwa mara na wataanza kuuliza Rabbon upo wapi, Salari upo wapi na wengine wengi watatajwa lakini watashangaa mbona IDs hizi zimekuwa kimya ndipo watakumbuka tuliyokuwa tunaandika mara kwa mara kilio na kusaga meno kutakuwa kwingi sana.
Ana heri yeye amuaminiye bwana Yesu sasa na kuishi maisha matakatifu kujianda na unyakuo.
Lakini 'wajasiria dini' na makanisa ya manabii wa uongo yanayoibuka kama uyoga kila uchao ndiyo kikwazo kikubwa sana cha great thinkers na pingamuzi kuu la binadamu.
Tupo tunaomwamini Mungu na kumkiri masiya Yesu kristo kwamba yuhai na mafundisho yake ni halisi.
Lakini mfumo mliotuletea wa sadaka sijui matoleo ya kausha damu ili kuboresha maisha yenu, tunamwachia Mungu mwenyezi ndiye muamuzi wa haki.
Sitafuata maelekezo wala mafundisho kutoka midomoni kwa nabii wala mitume, kwa sababu najua kusoma na kuandika, nitasoma miongozo mwenyewe kutoka biblia na vitabu vya ritrujia kuliko kulishwa matango pori na kupoteza muda na rasilimali kwa matapeli.
Mnaoyaamini hayo na ngonjera zao, endeleeni na kusoteshwa.