Kama unaijua Kenya vizuri utaihurumia tu.
Binafsi, sipendi kikundi kidogo ndani ya CCM na wanasiasa wengine ndani ya vyama vya upinzani ndio wanaturudisha nyuma.
Ukiachana na thamani ya shilingi, GDP na GDP per Capita ambazo Kenya iko juu kidogo, Tanzania inaizidi Kenya karibu kila kitu.
Tembea Kenya ujionee umasikini wa kutisha.
Hapa Tanzania, tunaita Tandale, Mwananyamala, Buguruni, Kwa Aziz Ally ni Uswahilini, nenda Kenya uone Uswahilini.
Tanzania nyumba za mabati huwa tunacheka eti wanakaa Polisi, nenda Kenya uone nyumba za mabati Kenya ni nyumba za kupanga.
Miundombinu mizuri mingi ni ya wageni au ya kulipia. Tanzania Daraja la Tanzanite mnapita bure.
Daraja la Nyerere la kulipia ila anachukua pesa mi serikali. Kenya imejengwa barabara ya kulipia pesa wanachukua wachina mpaka 2027.
Tembea Kenya vijijini huko Mombasa, Kilifi, Lamu, kuna umasikini wa kutisha vibaya sana.