MastaKiraka
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 5,736
- 18,648
Na kazi hii ilifanywa na wazawa, kuna jamaa hapa jukwaani alikuwa anasema TZ iko nyuma ki teknolojia compared to Kenya na kwamba kwa TZ hakuna programmers/developers competent ukilinganisha na Kenya.Integrated System imekuwa implemented in 2017, halafu wewe unamsifia Samia.
Ama kweli tenda wema nenda zako, kwenye hii dunia.
Centralised Digital Technologies za finance zipo sokoni toka 2010. Ni mambo ya 5th Industrial revolution.Na kazi hii ilifanywa na wazawa, kuna jamaa hapa jukwaani alikuwa anasema TZ iko nyuma ki teknolojia compared to Kenya na kwamba kwa TZ hakuna programmers/developers competent ukilinganisha na Kenya.
Kuna watu uelewa wao wa jambo/mambo/hoja huwa na upungufu, hivyo msamehe mleta uzi kwani licha ya kuwa uelewa wake ni finyu sana, lakini pia ni mmojawapo wa majeruhi wa demokrasia ya 21 March 2025, hivyo anatafuta kusajiliwa rasmi kwenye "chawa wa mama" ili mkono uende kinywani.Kenya kaja kujifunza namna ya kuweka kumbukumbu za madeni. Wewe unasema huo utaratibu sifa apewe Samia lakini huo utaratibu umekuwepo toka Nyerere, wa kujua nani katukopesha ila wewe unasema sifa apewe Samia, hapo ndio shida ya uchawa inapokuja.
Huu utaratibu wa kuweka rekodi sahihi za madeni tunao miaka yote, na miaka yote watanzania tumekua tukiambiwa deni letu ni kiasi gani. Sasa Samia anaingiaje hapo?
Kama mtu kafanya jambo jema asifiwe ila hii sio hoja kabisa.
Haya mapambano umeyaona wapi wewe?mapambano dhidi ya Rushwa,
Umesoma vizuri thread na kuangalia video clip? Umeelewa?Mtoa mada unapaswa kuwa specific tuinazidi Kenya kwa lipi? Maana shilingi yetu ni mara ngapi kwao? Maswala ya Katiba na utawala bora ndo hivyo tena. Utekaji ulitaka kuanza kilichotokea kama wewe ni mfuatiliaji umeona. Mambo yaliweka hadharani na ujinga utaishia hapo, bongo sasa duu. Hii nchi tulichowashinda wengine ni UCHAWA na sio kingine chochote
Nasemaje, umieni sana haters na umieni zaidi.....hakuna ulijualo. Marehemu JPM amesifiwa kwa miradi mingapi ambayo kwa macho yetu tuliiona ikianzishwa na Kikwete?!!! Mbona hamsemi?!!! Mnachuki zenu na huyu mama, huo ndo ukweli. Bahati mbaya Kadiri mnavyomchukia ndivyo anavyozidi kuchanja mbuga ndo maana nasema hamna chaguo jingine zaidi ya kuandaa ndoo zaidi za machozi tu.Sasa nibubujikwe na machozi kwanini kwa mfano.
Binadamu tunatofautiana, wengine wana soni ya kuchukua sifa ambazo sio zao. Na wengine wala hawakosi usingizi.
Ni kama juzi alivyokuwa Tanga yaani hana noma kabisa ‘bi tozo’. Maboresho ya bandari ya Tanga kazi inaanza kipindi cha Magufuli dunia nzima inaona, halafu anajidai hela katoa yeye.
Ndio kama huyu mleta mada, video inasema wazi kabisa mfumo umewekwa lini yeye kaamua tu kumpa sifa mtu mwingine.
Si bora angesema Tanzania tu.
Sio tusihilo..angalia wanaume wanavyokushangaa.shame on youUsilete umalaya humu kajiuze mbele huko.
Watakao umia sio mimi bali ni watoto ambao wana miaka 20 leo wafikifikisha miaka 40 kusoma historia kuona DPW kapewa bandari kwa mtaji ambao mpaka sasa ajaweka ushahidi.Nasemaje, umieni sana haters na umieni zaidi.....hakuna ulijualo. Marehemu JPM amesifiwa kwa miradi mingapi ambayo kwa macho yetu tuliiona ikianzishwa na Kikwete?!!! Mbona hamsemi?!!! Mnachuki zenu na huyu mama, huo ndo ukweli. Bahati mbaya Kadiri mnavyomchukia ndivyo anavyozidi kuchanja mbuga ndo maana nasema hamna chaguo jingine zaidi ya kuandaa ndoo zaidi za machozi tu.
Umesoma nakuangalia video clip vizuri? Umeelewa mada inazungumzia nini?Watakao umia sio mimi bali ni watoto ambao wana miaka 20 leo wafikifikisha miaka 40 kusoma historia kuona DPW kapewa bandari kwa mtaji ambao mpaka sasa ajaweka ushahidi.
Lakini anavuna bure
Watoto ambao kesho wataona jinsi tulivyoshindwa kesi za uwekezaji kishamba, na kugawa baadae kuwapa ‘rare earth mineral zetu’ wawekezaji kwa mikataba ya hovyo.
Wataumia namna mtu kama Kafulila akifanikiwa kugawa rasilimali zetu kama bure.
Tanzania ina wasomi na vichwa vingi, kitu ambacho najifunza ukifikia level fulani ya uelewa, kuwajua watanzania; na CCM inavyowachezea. Acha kupoteza muda wako fanya mengine, hayo mwache mungu aamue future yao.
If anything unaanza kujiona mpumbavu kupoteza muda wako JF badała ya kutumia huo muda kufanya mambo ya maana.
Kuchomoka hapo safari ndefu sana, tutabaki laumu wazungu kwa madhaifu yetu.
Nisingechangia bila ya kufanya hivyo kwanza.Umesoma nakuangalia video clip vizuri? Umeelewa mada inazungumzia nini?
Sana, ukifuatilia vizuri utabaini huyo mdhibiti wa bajeti amekuwa akipigwa vita vikali na serikali yake yaani hawataki uwazi wa aina hiyoUmeisikiliza clip vizuri lakini?
Nimejionea hii taarifa nikasukumwa kuandika huu uzi kuhusu serikali ya Tanzania ya sasa!
Kwa muda mrefu nimekua mkosoaji nguli wa serikali za CCM kuanzia kwa JK hadi kwa Samia!
Kwa hivi karibuni trend ya uchumi wa Tanzania, mapambano dhidi ya Rushwa, harakati za matumizi ya nishati safi, ujenzi wa miundombinu na maboresho makubwa katika utumishi wa umma huyu mama Samia anastahili pongezi za pekee!
Kikubwa kilichonifurahisha na kunisukuma kuandika huu uzi ni juu ya usafi katika mwenendo mzima wa usajili na uwazi wa matumizi ya madeni ya nchi. Mkaguzi mkuu wa Hesabu za kenya anasema wanapaswa kujifunza na kuiga huu mfumo bora kabisa toka Tanzania.
Hii video hapo chini ni kutoka nchi ya Kenya tunayoamini na kuisifu ipo mbali sana kuliko Tanzania katika katiba na mengine mengi wanakiri kuja kujifunza Tanzania juu ya uwazi katika fedha!! Rais Ruto alikiri Tanzania inaizidi Kenya kwa exports!!
Hakika mwanamke anaweza na anaweza tena!
Huu uzi umenifanya niwakumbuke akin mama shupavu sana akina Benazir Buto, Angela Markel, Margaret Thatcher na Her majesty the Queen Elizabeth II wa Uingereza!!
My Tribute to Samia Suluhu Hassan! Hongera Samia hongereni wanawake Mnaweza!
Kenya karibu kila kitunkizuri siyo cha Wakenya, ni cha Wageni.Una mawazo mazuri sana! Ukiongeza na haya ya kwenye uzi Tanzania tutakua nchi bora sana! Kufika ni hatua na tupo pazuri! Kuna watu wanajidharau kama nchi lakini hiyo Kenya wanayoiona bora wanatamani kuwa kama Tanzania.
Kama unaijua Kenya vizuri utaihurumia tu.Unaifananisha Kenya na Tanzania kwa kutumia specific to general approach. Actually Kenya ipo juu kiuchumi kulikon Tanzania, kawaida ni kwamba tajiri hujifunza hata njia za utafutaji za masikini, ili azidi kuwa tajiri.
Unabonga hapa kama vile ni kitu rahisi, kidogo kisichohitaji credit yoyote.Centralised Digital Technologies za finance zipo sokoni toka 2010. Ni mambo ya 5th Industrial revolution.
AI sasa hivi ukishafanya system integration kuna software zinamaliza kila kitu wewe ni kuweka data tu. Inakupa patterns, trends, unaweza ku-pre set financial objectives za future prediction kutokana na uwezo wako wa cashflow kumudu madeni and so forth in realtime (ndio mambo ambayo huyo mama wakikenya yaliyo mshangaza).
Dunia ya leo kuna technologies kama; data analytics tools, robotic processes automation na machine learning. Hela yako tu na kuwaambia manufacturers unataka wa pre-set algorithm zipi kwenye mfumo wako wa finance kutokana na uwezo wa hizo technologies.
Huyo mama wakikenya atakuwa mhasibu (au financier) wa zamani ambae aja-update skills zake miaka mingi ndio maana kashangaa kuona centralised system ya Tanzania. Either way maana yake tupo mbele ya Kenya kwenye uelewa wa matumizi ‘big data’ kwa namna alivyoshangaa.
Kuuchezea mfumo inakuwa ngumu data zikishawekwa ndio maana, watu huko TRA kariakoo wameona isiwe tabu wachome na ofisi yenyewe kabisa kufuta physical evidence baada ya wizi wao hiyo ndio serikali ya mama imejaa majizi.
Mazuri mengi ya usimamizi aliweka Magufuli; huyu wa leo sio wakujali anataka watu wale kwa urefu wa kamba yao.
Hivi vitu akina Tindo Proved Mrs besigye Lord denning hawavijui wanasubiri story Za akina Lissu Kuhusu kenyaKama unaijua Kenya vizuri utaihurumia tu.
Binafsi, sipendi kikundi kidogo ndani ya CCM na wanasiasa wengine ndani ya vyama vya upinzani ndio wanaturudisha nyuma.
Ukiachana na thamani ya shilingi, GDP na GDP per Capita ambazo Kenya iko juu kidogo, Tanzania inaizidi Kenya karibu kila kitu.
Tembea Kenya ujionee umasikini wa kutisha.
Hapa Tanzania, tunaita Tandale, Mwananyamala, Buguruni, Kwa Aziz Ally ni Uswahilini, nenda Kenya uone Uswahilini.
Tanzania nyumba za mabati huwa tunacheka eti wanakaa Polisi, nenda Kenya uone nyumba za mabati Kenya ni nyumba za kupanga.
Miundombinu mizuri mingi ni ya wageni au ya kulipia. Tanzania Daraja la Tanzanite mnapita bure.
Daraja la Nyerere la kulipia ila anachukua pesa mi serikali. Kenya imejengwa barabara ya kulipia pesa wanachukua wachina mpaka 2027.
Tembea Kenya vijijini huko Mombasa, Kilifi, Lamu, kuna umasikini wa kutisha vibaya sana.