Unanikumbusha kuna dogo alikuja kunitembelea huku US kutoka Tanzania. Alikuwa jirani yetu wa zamani tumekua pamoja, nikafurahi sana kuonana naye kaja kwangu kunitembelea.
Akawa anaangalia viatu fulani hivi kwangu, anasema viatu vikali sana.
Nikamwambia hivyo vya kawaida tu, tena vya Mchina hivyo. Alikuwa kama anavitaka, mimi nilikuwa kama namtahadharisha kuwa vinaweza kum disappoint.
Akaniambia hata kama vya Mchina, vya Mchina vinavyoletwa huku US na vinavyoletwa Africa ni tofauti kabisa.
Nikasema si utani.