My week end is super crazy

My week end is super crazy

Ndo hivyo.

Kuna dogo alikuwa analikia sana game kila ikitoka lazima apate, tena apate mapema kabla ya wenzake.

Lakini akishaipata anacheza hata wiki haifuki anaitupa pembeni kashaisahau.

Anashughulika na mambo mengine.

Lakini asipopata sasa, huo muziki wake 😂😂😂
😀😀😀
Ila watoto wana visa jamani😀
Nimempigia picha huyo dogo nimejikuta nacheka😀

Ila pamoja na hekaheka zao zote huwa wanaburudisha sana.

Wana uwezo wa kukukera mpaka ukatamani kumtupa dirishani hlf ndani ya dakika akakufanya utabasamu na usahau yote😀
 
My week end is wacko.

Kuna watoto wazuri wa rafiki yangu watakaa na mimi mpaka katikati ya Nov. ila sijui nisemeje nisionekane wicked aunty ila wamekuja J nne na tayari niko super stressed na Nov. naiona mbali sana

Stress zilianzia kwa jinsi mtoto wangu hataki ku share Tv yake na wenzie sbb wenzie ni wadogo na vitu wanavyopenda kuangalia ni tofauti.

Nikatoa amri waangalie kwa kupokezana ila haikusaidia watoto coz bado hao madogo wageni mmoja wa kike wawili wa kiume.Vitu anavyopenda kuangalia wa kike hivi vijamaa viwili havipendi fulu kugombana.

Yaani ni mashitaka kila dakika.Huyu wa kwangu analalamika madogo wanaharibu vitu chumbani kwake na madogo wanalalamika kaka anawapiga na kuwafukuza chumbani kwake wasiangalie Tv.

Nikasema hizi stress zitaisha kila mtoto akiwa na tv chumbani kwake,nikatuma mtu akaninunulie Tv ndogo 4,zikaja zikafungwa kila mtu akafurahi nami nikasema nitapumua sasa ila nimejidanganya😃😃.eti baada ya kila mtu kupata Tv yake na interest ya kuangalia Tv ikaisha.Yaani madogo hawana muda na hizo Tv.Hela zangu zimepotea bure😭😭.

Hao wawili wa kiume ni mapacha wako very smart ila ni WATUNDU sana.Wamekaa siku mbili tu ila wameshaharibu vitu vingi halafu sasa vikiharibu kitu ukifoka unasikia “aunty you don’t look cute when you are angry” au “my daddy will buy you another one”

Leo asubuhi hivi vi twins vimefanya kitu cha hatari sana nikawatisha kuwa leo nawachapeni,nikaagiza niletewe fimbo mbili kubwa.Kumbe watoto wa watu hawajawaji kuchapwa wala kutishiwa fimbo.Kale ka kike kananiambia “aunty ukiwachapa baba yangu atakuchapa na wewe maana baba kasema mama akituchapa atamchapa na yeye” nikamwambia mimi simuogopi baba yako na fimbo zikija nawachapa kaka zako.

Fimbo zimefika ile watoto wanaziona tu waliteteeka hadi kamoja kakajikojolea na kengine kakatapika kwa panic.Nilishangaa sana maana mie wa kwngu keshakula sana mikwqju.Sasa nikajiuliza hata shule havichapwi hadi vitetemeke vile!

Ikabidi niache mkwara nianze kuvibembeleza na kutupa fimbo.Kale kakike kalivyoona nimetupq fimbo kakanimbia “usingenisikiliza baba yangu angekumaliza”

Huwezi kuamini hawa watoto eti kutishiwa fimbo tu wamelia zaidi ya masaa mawili.Na wanalia kwa kupokezana,huyu akinyamaza ukisema sasa wamenyamaza unashangaa mwengine kapokea .

Nimebembeleza nimechoka hadi na mim nikaingia chumbani kwangu kulia.Watoto hawa sijui baba yao uchumi ukiyumba itakuwaje coz wakitaka kitu lazima wapate la sivyo atalia siku nzima.Akitaka pizza kwa aman yako utahakikisha pizza imefika.Naona ajabu sbb mwanangu nikisema leo ni chai na kiporo cha ubwabwa kanakula.Mwanangu nikisema hata chai na ugali atakula with a smile on his face.Asubuhi ya kwanza the way vilitupelekesha ningekua na sukari ingepanda.Bodaboda walikua wanapishana getini kwetu coz kila tunachotumia sisi kwa breakfast walivikataa na kila kinacholetwa anakwambia sio hiyo ana favorite yake na lazima apate hiyo,unamrudisha boda ikija brand tofaut hali na hapo wako watatu na kila mmoja ana favorite yake.Ukisema uvikazie vitoto vya watu vitashinda njaa nafsi inakataa basi ni kuhangaika hadi kila mmoja apate anachotaka.

Hivi wazazi mnaodekeza watoto wenu faida ni ipi?

Mna upendo sana kushinda sisi wengine au?
Hahaha
 
🤣🤣🤣Wewe naona unatakq kuua urafiki na hao nduguzo wakitoka huko majuu wakute unawatazamisha kina junya solarmax

Nimeingia chumban kwa mwanangu nikakumbuka hii comment yako japo ni utani ila nikajisemea sometimes mama wa kambo wanaonewa😀.

Hivi imagine wewe na Lamomy ndo mngekua mawifi zangu hlf mnakuja mnakuta mwanangu nilokutwa nae ana TV ya Samsung room kwake halafu damu za kaka yenu zinaangalia Solarmax aka umiza macho si mngenila nyama nyie?😀😀

7A22115E-8D3B-4754-99F8-8773D264D362.jpeg
B714D15B-73CE-445F-9FF2-FC5F867BAE88.jpeg
Na hapo ukute nimenunua kwa upendo tena na hela zangu ila ndo hivyo ukiwa mama wa kambo lazima uonekane umependelea wa kwako😀
 
Kuna watu wana TV halafu wanaombea ziharibike ili wapate sababu ya kununua TV mpya kali zaidi.

Lakini zina wa disappoint haziharibiki 😂😂😂
😀😀😀
Mwishowe inabidi tu ufanye maamuzi magumu zitoke uingize kitu latest😀
 
😀😀😀
Mwishowe inabidi tu ufanye maamuzi magumu zitoke uingize kitu latest😀
Kuna ma TV ya zamani yanadumu sana mpaka unataka yaangalie Kibla tu yaanguke.

Kuna wakati nilinunua kitu Samsung, basi ile stand nikawa nimeiweka halafu haijakaa vizuri.

Nilikwenda kazini asubuhi, nikarudi nikakuta TV imeanguka chini, palikuwa na carpet zuri. Huwezi kuamini ile TV ilidunda poa tu na mpaka leo inafanya kazi haina tatizo hata moja. Hiyo ilikuwa miaka kama 11 iliyopita.

Mtu unataka kuitupa uweke mpya lakini unakosa sababu 🤣🤣🤣
 
Hao madogo wape manual activities na unapokuwa na muda unakuwa karibu kama kuchora, afundishe michezo tofauti ambayo hawaijui, asubuh wakiamka unafanya nao usafi, mpaka wazazi warudi wameshabadilika. Hao Kuna v trick vidogo vidogo.
 
Alinifanya nitafakari mambo mengi sana. Tukamwambia, sio mara zote tunakua na pesa, ndio maana tunanunua vitu vya kutosha mwezi mzima. Tukamuuliza, ukitoka shule ukafika nyumbani ukaambiwa chakula kimeisha hatujanunua itakuaje? Akasema si Dada atawapigia simu bodaboda akanunue vitu? Tukamwambia bodaboda anataka pesa, na kama hatuna wakati huo itakuaje? Akasema, mbona kila siku hua kuna pesa kwenye pochi ya Mama? Tukamwambia zina matumizi mengine.

Ila cha ajabu, ukirudi na vitu nyumbani anavyokupokea atasema thank you Daddy for us buying stuffs, kumbe kichwani hua ana maswali yake.

Ana maswali mengi sana kuliko Dada yake mkubwa.
Wanatakiwa walale njaa siku moja
 
🤣🤣🤣Wewe naona unatakq kuua urafiki na hao nduguzo wakitoka huko majuu wakute unawatazamisha kina junya solarmax
Nimeingia chumban kwa mwanangu nikakumbuka hii comment yako japo ni utani ila nikajisemea sometimes mama wa kambo wanaonewa😀.

Hivi imagine wewe na Lamomy ndo mngekua mawifi zangu hlf mnakuja mnakuta mwanangu nilokutwa nae ana TV ya Samsung room kwake halafu damu za kaka yenu zinaangalia Solarmax aka umiza macho si mngenila nyama nyie?😀😀

View attachment 3109640View attachment 3109647Na hapo ukute nimenunua kwa upendo tena na hela zangu ila ndo hivyo ukiwa mama wa kambo lazima uonekane umependelea wa kwako😀
🤣🤣🤣🤣Yaani ningehakikisha hiyo Sumsung ya mwanao naimwagia super glue sehemu yeyote yenye upenyo kabla sijaondoka hapo kwako....tena gud enough your boy kanirahishia hapo alivyotupatupa vitu nimeiona super glue
 
Kuna ma TV ya zamani yanadumu sana mpaka unataka yaangalie Kibla tu yaanguke.

Kuna wakati nilinunua kitu Samsung, basi ile stand nikawa nimeiweka halafu haijakaa vizuri.

Nilikwenda kazini asubuhi, nikarudi nikakuta TV imeanguka chini, palikuwa na carpet zuri. Huwezi kuamini ile TV ilidunda poa tu na mpaka leo inafanya kazi haina tatizo hata moja. Hiyo ilikuwa miaka kama 11 iliyopita.

Mtu unataka kuitupa uweke mpya lakini unakosa sababu 🤣🤣🤣
😀😀😀

Naona ulivyoiona hapo chini ulijua ndo kwisha habari yake kumbe yenyewe inakwambia mimi na wewe hadi kifo kitutenganishe😀😀😀
 
😀😀😀

Naona ulivyoiona hapo chini ulijua ndo kwisha habari yake kumbe yenyewe inakwambia mimi na wewe hadi kifo kitutenganishe😀😀😀
Yani mpaka leo ipo chumba cha wageni huwa naiangalia nasema "Wewe Mkorea una roho ngumu sana" 😂😂😂
 
Kuna ma TV ya zamani yanadumu sana mpaka unataka yaangalie Kibla tu yaanguke.

Kuna wakati nilinunua kitu Samsung, basi ile stand nikawa nimeiweka halafu haijakaa vizuri.

Nilikwenda kazini asubuhi, nikarudi nikakuta TV imeanguka chini, palikuwa na carpet zuri. Huwezi kuamini ile TV ilidunda poa tu na mpaka leo inafanya kazi haina tatizo hata moja. Hiyo ilikuwa miaka kama 11 iliyopita.

Mtu unataka kuitupa uweke mpya lakini unakosa sababu 🤣🤣🤣
Dah umenikumbusha home tuliwahi kuwa na HITACHI ya chogo jamani ile ni roho ya paka ilibidi tu i phase out japo haina tatizo...ipo hadi leo
 
Dah umenikumbusha home tuliwahi kuwa na HITACHI ya chogo jamani ile ni roho ya paka ilibidi tu i phase out japo haina tatizo...ipo hadi leo
Hizo TV za HITACHI ya chogo za zamani zinadumu sana. Kuna moja nakumbuka ilikuwepo home tuliangalia Olympics za 1988 mpaka miaka ya 2000s ilikuwepo. Ina kimeza chake fulani kina matairi hivi 😂😂😂.
 
Back
Top Bottom