My week end is super crazy

My week end is super crazy

Afadhali imekupa uzoefu mpya na kujifunza mambo mapya hasa namna bora ya kumlea kijana awe tayari kuishi mazingira tofauti tofauti.
Kabisa.
Tena bora siku hizi anatoka hata kucheza nje😀
Zamani ilikua ni ndani tu.
Kipindi cha likizo alikua mpweke.
Siku ya kwanza katoka nje jirani alinipigia eti mmesahau kufunga geti fulani katoroka 😀😀 namuona huku nje😀
 
Ujue unaweza kumchukulia poa huyo dogo alivyoumia kuona matunda mengi yanatupwa hadi kukushauri usome hicho kitabu ila ameonesha kuwa na kitu kikubwa ambacho hata watu wazima wengi hawana.

Sio kawaida kwa mtoto wa umri huo kuonea huruma pesa.Kuna watu wazima wanatupa chakula,wanatumia vitu vibaya hasa vikiwa vingi ndani hata hawajali sbb vikiishwa vinaletwa vingine .
Hao madogo hao nimewapenda.
Hongea kwa baba na mama

Alinifanya nitafakari mambo mengi sana. Tukamwambia, sio mara zote tunakua na pesa, ndio maana tunanunua vitu vya kutosha mwezi mzima. Tukamuuliza, ukitoka shule ukafika nyumbani ukaambiwa chakula kimeisha hatujanunua itakuaje? Akasema si Dada atawapigia simu bodaboda akanunue vitu? Tukamwambia bodaboda anataka pesa, na kama hatuna wakati huo itakuaje? Akasema, mbona kila siku hua kuna pesa kwenye pochi ya Mama? Tukamwambia zina matumizi mengine.

Ila cha ajabu, ukirudi na vitu nyumbani anavyokupokea atasema thank you Daddy for us buying stuffs, kumbe kichwani hua ana maswali yake.

Ana maswali mengi sana kuliko Dada yake mkubwa.
 
Wala usijali sana yawezekana nina ma tv mengi ila na wewe una kitu hata nikiuza hizo tv zote siwezi kukipata.

Pia maisha ni furaha.
Kuwa na ma tv mengi haimaanishi mtu ana furaha.
Kama una furaha ushayapatia maisha.
Aaah Pridah acha kunipanga basi🤣🤣🤣🤣
 
Alinifanya nitafakari mambo mengi sana. Tukamwambia, sio mara zote tunakua na pesa, ndio maana tunanunua vitu vya kutosha mwezi mzima. Tukamuuliza, ukitoka shule ukafika nyumbani ukaambiwa chakula kimeisha hatujanunua itakuaje? Akasema si Dada atawapigia simu bodaboda akanunue vitu? Tukamwambia bodaboda anataka pesa, na kama hatuna wakati huo itakuaje? Akasema, mbona kila siku hua kuna pesa kwenye pochi ya Mama? Tukamwambia zina matumizi mengine.

Ila cha ajabu, ukirudi na vitu nyumbani anavyokupokea atasema thank you Daddy for us buying stuffs, kumbe kichwani hua ana maswali yake.

Ana maswali mengi sana kuliko Dada yake mkubwa.
Huyo hela yake itatoka baada ya kufanyiwa uhakiki wa kutosha.
 
My week end is wacko.

Kuna watoto wazuri wa rafiki yangu watakaa na mimi mpaka katikati ya Nov. ila sijui nisemeje nisionekane wicked aunty ila wamekuja J nne na tayari niko super stressed na Nov. naiona mbali sana

Stress zilianzia kwa jinsi mtoto wangu hataki ku share Tv yake na wenzie sbb wenzie ni wadogo na vitu wanavyopenda kuangalia ni tofauti.

Nikatoa amri waangalie kwa kupokezana ila haikusaidia watoto coz bado hao madogo wageni mmoja wa kike wawili wa kiume.Vitu anavyopenda kuangalia wa kike hivi vijamaa viwili havipendi fulu kugombana.

Yaani ni mashitaka kila dakika.Huyu wa kwangu analalamika madogo wanaharibu vitu chumbani kwake na madogo wanalalamika kaka anawapiga na kuwafukuza chumbani kwake wasiangalie Tv.

Nikasema hizi stress zitaisha kila mtoto akiwa na tv chumbani kwake,nikatuma mtu akaninunulie Tv ndogo 4,zikaja zikafungwa kila mtu akafurahi nami nikasema nitapumua sasa ila nimejidanganya😃😃.eti baada ya kila mtu kupata Tv yake na interest ya kuangalia Tv ikaisha.Yaani madogo hawana muda na hizo Tv.Hela zangu zimepotea bure😭😭.

Hao wawili wa kiume ni mapacha wako very smart ila ni WATUNDU sana.Wamekaa siku mbili tu ila wameshaharibu vitu vingi halafu sasa vikiharibu kitu ukifoka unasikia “aunty you don’t look cute when you are angry” au “my daddy will buy you another one”

Leo asubuhi hivi vi twins vimefanya kitu cha hatari sana nikawatisha kuwa leo nawachapeni,nikaagiza niletewe fimbo mbili kubwa.Kumbe watoto wa watu hawajawaji kuchapwa wala kutishiwa fimbo.Kale ka kike kananiambia “aunty ukiwachapa baba yangu atakuchapa na wewe maana baba kasema mama akituchapa atamchapa na yeye” nikamwambia mimi simuogopi baba yako na fimbo zikija nawachapa kaka zako.

Fimbo zimefika ile watoto wanaziona tu waliteteeka hadi kamoja kakajikojolea na kengine kakatapika kwa panic.Nilishangaa sana maana mie wa kwngu keshakula sana mikwqju.Sasa nikajiuliza hata shule havichapwi hadi vitetemeke vile!

Ikabidi niache mkwara nianze kuvibembeleza na kutupa fimbo.Kale kakike kalivyoona nimetupq fimbo kakanimbia “usingenisikiliza baba yangu angekumaliza”

Huwezi kuamini hawa watoto eti kutishiwa fimbo tu wamelia zaidi ya masaa mawili.Na wanalia kwa kupokezana,huyu akinyamaza ukisema sasa wamenyamaza unashangaa mwengine kapokea .

Nimebembeleza nimechoka hadi na mim nikaingia chumbani kwangu kulia.Watoto hawa sijui baba yao uchumi ukiyumba itakuwaje coz wakitaka kitu lazima wapate la sivyo atalia siku nzima.Akitaka pizza kwa aman yako utahakikisha pizza imefika.Naona ajabu sbb mwanangu nikisema leo ni chai na kiporo cha ubwabwa kanakula.Mwanangu nikisema hata chai na ugali atakula with a smile on his face.Asubuhi ya kwanza the way vilitupelekesha ningekua na sukari ingepanda.Bodaboda walikua wanapishana getini kwetu coz kila tunachotumia sisi kwa breakfast walivikataa na kila kinacholetwa anakwambia sio hiyo ana favorite yake na lazima apate hiyo,unamrudisha boda ikija brand tofaut hali na hapo wako watatu na kila mmoja ana favorite yake.Ukisema uvikazie vitoto vya watu vitashinda njaa nafsi inakataa basi ni kuhangaika hadi kila mmoja apate anachotaka.

Hivi wazazi mnaodekeza watoto wenu faida ni ipi?

Mna upendo sana kushinda sisi wengine au?
What is week end? Hebu tafsiri kwa kiswahili ili nielewe.
 
Watu wananunua TV kama unavyonunua chumvi.
Halafu huwezi amini zilivyofungwa tu na interest ya kuangalia cartoon imeisha.
Nahisi ile kugombania remote na kupigana pigana ni starehe kwao
 
Halafu huwezi amini zilivyofungwa tu na interest ya kuangalia cartoon imeisha.
Nahisi ile kugombania remote na kupigana pigana ni starehe kwao
Ndo hivyo.

Kuna dogo alikuwa analilia sana game kila ikitoka lazima apate, tena apate mapema kabla ya wenzake.

Lakini akishaipata anacheza hata wiki haifiki anaitupa pembeni kashaisahau.

Anashughulika na mambo mengine.

Lakini asipopata sasa, huo muziki wake 😂😂😂
 
Hela za LG 4 kwa mkupuo natolea wapi mtumishi?😀

Kina Junior acha wapambane na solarmax macho yao bado hayajaona mengi hayawezi kuharibika.

Mimi na wewe tushaona mengi haya macho tukizembea kidogo tu tunaanza kuona ukungu😀😀
🤣🤣🤣Wewe naona unatakq kuua urafiki na hao nduguzo wakitoka huko majuu wakute unawatazamisha kina junya solarmax
 
Ndo hivyo.

Kuna dogo alikuwa analikia sana game kila ikitoka lazima apate, tena apate mapema kabla ya wenzake.

Lakini akishaipata anacheza hata wiki haifuki anaitupa pembeni kashaisahau.

Anashughulika na mambo mengine.

Lakini asipopata sasa, huo muziki wake 😂😂😂
😀😀😀
Ila watoto wana visa jamani😀
Nimempigia picha huyo dogo nimejikuta nacheka😀

Ila pamoja na hekaheka zao zote huwa wanaburudisha sana.

Wana uwezo wa kukukera mpaka ukatamani kumtupa dirishani hlf ndani ya dakika akakufanya utabasamu na usahau yote😀
 
Back
Top Bottom