My week end is super crazy

Watazoea na wataacha kutapika.

Mpaka ifike november nyumba itakuwa haitamaniki.
Ngojea nione nitajaribu polepole.

Hlf vikiongea na mama yao wanasema wanampenda aunty hawataki kurudi nyumbani😁 kirohon nasema mtoto hata akukasirishe vipi ni ngumu kumchukia.Hata havijui kama vinanipa stress masikin na ninataman waondoke nipumur😁
 
Acha kulea watoto kimayai hao ma auncle ni damu yako huo mwezi mmoja unatosha kuwabadili mentality zao!

Wafundishe kitu tofauti kumbuka MTOTO UNAVYOMLEA...
Huko kwao ndo wamelelewa kimayai mkuu.
Halafu mi naona haisaidii kutumia nguvu kustrress wabadilike hlf baada ya wiki chache wanarudi kwao kudekezwa tena.

Wangekua wamehamia kwangu moja kwa moja lazima ningewabadilisha
 
Siwezi kuwarudisha hadi wazazi wao warudi,wamesafiri nje ya Tz na mimi mwenyewe ndo nilisema waletwe kwangu coz navipenda ila nimejua hawa inabidi mapenz ya mbalimbal,wakichukuliwa sitarudia tena kuvichukua
.
Pole sana. Hawa watakuwa watoto ambao wazazi wanalea kwa ule mfumo mpya wa 'gentle parent' mtoto haambiwi hapana, hafokewi, hachapwi.

Mtoto wangu wa kwanza tulilea kitaliban kama mimi nilivyokuzwa so far so good, mwanangu wa pili wamepishana miaka 5 nikasema hebu nifanye hiyo gentle parenting eh, heheheee..ananitoa jasho akianza kulia mtaa mzima unajua, na hapo sijatandika. Hizo tantrum sio za dunia hii. Mwanangu wa 3 sasa huyu sirudii kosa tunafanya vyote. Kuna namna nikimkata jicho anajua sichezi lakini huyu wa pili ananibully mpaka sasa 😂😂
 
Huo upuuzi kwangu hapana, mzazi wao angewatafutia kwa kwenda mapemaa
 
Pole na hongera mkuu.


Halafu nahisi wakishadekezeka kuwakazia inakua ngumu
..

Yaani wewe ndo umenielewa hasa hapo kwenye kilio.Ni kama wanalia kukukomoa,😁 .
Mimi nikipata mtoto sitafanya kosa la kudekeza.

Pole kwa kuwa bullied na sec
born.😁 na wanavyojiamin sasa hata umtishie haisaidii.
 
Huo upuuzi kwangu hapana, mzazi wao angewatafutia kwa kwenda mapemaa
Nakuelewa dear ila wazazi wao wako nje na mim ndo nilijitolea kukaa nao mpaka warudi
 
Asante sana dear, bado napoa😂😂
 
Binafsi huwa sioni furaha ya kudekeza mtoto..
Ile ongea yao ya kimideko hasa likiwa la kiume huwa nakereka sana..

Napenda sana mtoto awe rafiki sio kuact kule kudekadeka hata huwezi kwenda nae mahali maana atakutia aibu.
 
Huo sasa mtihani, mpka warudi umepungua kilo.
Acha tu ndugu.
Nimetoka kupiga patrol vyumban kwao sasa hivi vimelala so peacefullly hadi nafsi inanisuta jinsi navisema huku JF😀.
Vinavutia sana vi min monster vyangu😀
 
Binafsi huwa sioni furaha ya kudekeza mtoto..
Ile ongea yao ya kimideko hasa likiwa la kiume huwa nakereka sana..

Napenda sana mtoto awe rafiki sio kuact kule kudekadeka hata huwezi kwenda nae mahali maana atakutia aibu.
Kabisa mkuu.
Inatia hasira.
Sema kuna wazazi wanaona kama ndo upendo eti
 
Wewe ni winga wa kariakoo na ukome kupiga picha za TV kwenye maduka ya watu
 
Pole Sana..yani Naelewa unachopitia sasa Mimi nashauli pia kuhusu suala la wazazi humu ndani tuzoeshe watoto wetu kwenda Shule kwa usafiri wa kawaida
Mimi ilishanikututa siku moja sitasahau na Siwezi msimulia mtu Anaenijua ni kwamba toka Mwanangu kazaliwa Alikuwa hajawahi
kupanda Dala dala mpaka Amefika Darasa la Tano
sasa Siku moja nikasema ngoja niende nae tu tupande Dala dala nilikuwa naenda kumnunulia vitu vya Shule Aisee ile tumepanda tukakuta nafasi zimejaa msongamano..jasho..kukanyagwa Aisee Alipiga kelele Dala dala nzima wananishangaa tu Sababu Alikuwa Anadai Ashuke mbona niliona Aibu Mimi toka hapo Asubuhi Alikuwa Anapelekwa na gari Shule Saa ya kuludi ni Dala dala na Nilimwambia kabisa Akae Akijua Labda tu Mvua Inyeshe Nahisi hichi kituko kuna hata wazazi kilishawatokea ila ni Aibu kusimulia kabisa.
 
Mwisho wa siku ndo wanakuomba kitu unawaambia hauna, Wanajiongeza halafu mnakuja kulalamika watoto wanalawtiwa sana sikuhizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…