Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nitafanya hivyo.Wanyooshe wakiwa kwako wajue namna ya kuishi bila vurugu.
Hakika hili ni jambo jema sana kuwa na malezi ya pamoja, sio kila mzazi anavutia kwakeUmeongea vyema sana mkuu.
Ila pia naamini iko haja wazazi tupate mafunzo ya malezi maana wengine wanachukulia utoto kama ugonjwa.
Wengine wakiwa na vihela kidogo wanaona sifa kulea watoto kwa style ya what the kid wants the kid gets.
Wengi hawajui mtoto ni kama empty card na vile vitu vinavyoingizwa humo mwanzoni iwe vizuri au vibaya vikishaingia humo ni vigumu kuvifuta na wengi hawajui kuwa watoto sio wajinga.Ni binadamu wanaojifunza kwa kujaribu jaribu.Akigusa moto akiungua hatakaa tena maishan mwake aguse moto.
Akikataa kula ugali ataangalia nini kitatokea.Akiambiwa ukila utakua na nguvu kama baba na usipokula nakuchapa atakula na akikataa akichapwa kweli atajua hapa nikikataa ni viboko ila kakataa ugali anataka chips huyoo mbio unaagiza apikiwe chips siku nyingine ukimkatalia atasumbia sana sbb anajua nikikataa uwezekano wa kupata ninachotaka upo.
Na wazazi tunatakiwa wote tuwe na msimamo,baba akisema hapana na mama ni hapana.Sio baba kasema leo hawa wafue nguo zao akitoka mama unawaonea huruma unawasaidia.Au mama kasema hakuna hela wakienda kwa baba wanapewa.
Nimekupata mkuu na asante kwa kunikosoa na kunipa miongozo ya vile nilipaswa kufanya🙏🏼🙏🏼Kosa lako la kwanza,hukuuliza hawa watoto wanapendelea nini kwao hizi taarifa unapata Kwa wazazi wake.
Pili ulifanya kosa sana kununua hizo tv kwakua zinawndeleza ubinafsi Kwa mtoto wako na hao wageni,ilitakiwa uwakalishe na kuwaelimisha suala la umoja and team work,wapeleke nje wakakate majani ya bustani mkiwa wote,osha vyombo nao as team.
Tatu,unaingia gharama bila kua mbunifu as long as unawaridhisha wote,all this are wrong and hata mwanao atakua na tabia ya Umimi and mother only.
Change unavyomlea mwanao mtoe nje acheze na wenzie aweze soma mazingira tofauti.
🙏🙏🙏Wafanye kuwa rafiki zako, usikubali kuwapa kila wanachokitaka hata kama una uwezo nacho.
Kila mtoto ana kitu anachopenda kukifanya au kujifunza. Wafundishe kazi za mikono, nyumbani kama kuna maua wafundishe kumwagilia hapa utawapata watoto wengi sababu wanapenda kucheza na maji.
Kama kuna gari wafundishe kuosha, na unawapa ahadi wakiosha vizuri utawapeleka sehemu X. Sandals,nguo na sleepers zao waambie wazioshe wenyewe hata kama hazitotakata waache wacheze hapo kwa kazi hiyo. Watoto wakiwa wawili au zaidi hupenda kushindana na kila mmoja anataka afanye vizuri zaidi ya mwenzake.
Hapo safi mkuuNitafanya hivyo.
Nashangaa wa kwangu nilikua naweza kuchapa(siku hizi tunaongea tu) ila wa watu nashindwa.
Nimeongea na mwl. Wa sunday school awape mafunzo ya ziada vile mtoto wa Yesu anapaswa kuwa.
Asante sana Mkuu Ameshazoea kabisa Mungu ni Mwema.🙏🏼🙏🏼 Asante mkuu.
Itakua mlivyoshuka watu waliwafanya mada.
Pole ila sio kosa lake masikini kwake ilikua vitu vigeni ila hongera kumfanya azoee sbb hatujui kesho yetu itakuaje.
Mimi wa kwangu keshazoea kupanda daladala.Hata mimi napandaga hasa nikiwa na mwanangu na nimemfundisha hadi kugombea siti😀Huwa namwambia we wa kiume gangamara tupate siti😀😀 na katapambana tutapata kweli siti na akija mtu mzima bila kumwambia atasimama na kumpisha na ninakua nimemlipia kukaa kama mtu mzima na kuna siku tulipanda nikamwambia sina hela ya kukulipia ukae kwa hiyo utasimama mpaka tufike na huwa hapendi kubebwa.
wa kwangu pia yuko la 5 kama wa kwako ila kwa upande wangu naona bado ni mdogo kutumia daladala akiwa peke yake kwenda shule.Mimi wa kwangu atatumia daladala kwendea shule akifika form one ila kwa sasa naona ni hatari sana
😁😁😁sawa dada padri,ila ni LG tena sio Solarmax?au unaniagizia yangu mpya?Worry out.
Andaa ukuta wa kukaa 75," LG .TV yako