My week end is super crazy

Kwa umri huu tuliofikia sio wa kutizama brand hazieleweki tufe macho bure ndugu yanguπŸ˜€
Nilishangaa picha ulizoupload za TV zilikuwa na brand ya kuua macho,nikasema mmmh huyu ana mpango gani na kina junior?
 
Bidada unaendeleaje weekend hii na hao watoto?

Siku nyingine usikubali kirahisirahisi kulea watoto wa kisasa.
 
Huko kwao ndo wamelelewa kimayai mkuu.
Halafu mi naona haisaidii kutumia nguvu kustrress wabadilike hlf baada ya wiki chache wanarudi kwao kudekezwa tena.

Wangekua wamehamia kwangu moja kwa moja lazima ningewabadilisha
Unaweza kuwasaidia hata kwa mwezi mmoja, na watabaki na kichwani kuwa aunt Pridah hataki hiki au kile.
 
Itabidi kila mtu alee watoto wake, hawa kwangu wangerudi kwao wamekonda ingebakia lawama tu..
Ila nahisi naanza kuzoea sarakasi zaoπŸ˜€πŸ˜€
Nawamiss ule muda wako shule na mimi niko kwa mishe.

Pamoja na yote wakiondoka naamini ndo nitakondaπŸ˜€πŸ˜€
 
Nilishangaa picha ulizoupload za TV zilikuwa na brand ya kuua macho,nikasema mmmh huyu ana mpango gani na kina junior?
Hela za LG 4 kwa mkupuo natolea wapi mtumishi?πŸ˜€

Kina Junior acha wapambane na solarmax macho yao bado hayajaona mengi hayawezi kuharibika.

Mimi na wewe tushaona mengi haya macho tukizembea kidogo tu tunaanza kuona ukunguπŸ˜€πŸ˜€
 
Wanatuletea mizigo kwenye jamii yetu ya baadae
 
Bidada unaendeleaje weekend hii na hao watoto?

Siku nyingine usikubali kirahisirahisi kulea watoto wa kisasa.
Nashukuru kwa namna fulani nimeanza kuwazoea.
Nimewakazania sana naona sasa wanaanza kuelewa hapana na hakuna.
Shida kubwa imebaki kwenye utundu.
Hawa nahisi utundu wao ni wa kuzaliwa sio wa kudekezwa.

Kabisa aisee,sitachukua tena watoto kama siwajui vizuri
 
Pole sana.

Ila mimi nimefikia stage natamani sana watoto, hususan wadogo kabisa wale ambao mtu anaweza kuwalea vizuri yeye mwenyewe.


Ila tatizo siku hizi hata ukiwalea vizuri utotoni wakifika kwenye u teenager wanakubadilikia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Zamani ndio mtoto alikua wa jamii, Kwa Sasa ulezi umekua mgumu sana.

Wangu nawapenda sana, na wao wanalijua hilo, lakini pia wanazingatia kwamba wakikosea kipigo chake utafikiri wamevunja chungu chenye mboga ya familia.

Pole sana Kwa heka heka. Lakini huyo wako pia ukipata nafasi, mfanye achanganyike na wengine kidogo, itamsaidia sana.
 
Unaweza kuwasaidia hata kwa mwezi mmoja, na watabaki na kichwani kuwa aunt Pridah hataki hiki au kile.
Tumeshaanza kuelewana dear.
Mpaka siku wanaondoka mimi na wao wote tutakua tumebadilika.
Hata mimi kupitia wao najifunza vitu
 

Teenager mbali sana kaka, kwanza vina tambua haki zao na ipeo mkubwa sana wa mambo.

Mfano vijamaa vyangu vinapenda sana vipikiwe chips, Sasa tukakubaliana kwamba, wakila chips mchana, usiku wale chakula kingine.

Siku hiyo taarifa inatolewa, vinasema but that is not fair, how can you make a decision for us? You should have called a meeting...wakati huo vitoto hata miaka 10 havijafikisha.
 
Hahaaaa.

Unawaambia tu "shukuruni nyie si watoto wa baba yangu, mngekuwa watoto wake hilo suala hata msingelifikiria".

Tatizo wakimtafuta babu kumuuliza (kama yupo bado) naye wanamkuta kalainiiiika uzeeni siyo yule wa kipindi kileπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…