Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itabidi kila mtu alee watoto wake, hawa kwangu wangerudi kwao wamekonda ingebakia lawama tu..Aina za malezi siku hizi sijui ni aina na mfumo wa maisha gani jamii inajengewa.
Nilishangaa picha ulizoupload za TV zilikuwa na brand ya kuua macho,nikasema mmmh huyu ana mpango gani na kina junior?Kwa umri huu tuliofikia sio wa kutizama brand hazieleweki tufe macho bure ndugu yangu😀
Bidada unaendeleaje weekend hii na hao watoto?My week end is wacko.
Kuna watoto wazuri wa rafiki yangu watakaa na mimi mpaka katikati ya Nov. ila sijui nisemeje nisionekane wicked aunty ila wamekuja J nne na tayari niko super stressed na Nov. naiona mbali sana
Stress zilianzia kwa jinsi mtoto wangu hataki ku share Tv yake na wenzie sbb wenzie ni wadogo na vitu wanavyopenda kuangalia ni tofauti.
Nikatoa amri waangalie kwa kupokezana ila haikusaidia watoto coz bado hao madogo wageni mmoja wa kike wawili wa kiume.Vitu anavyopenda kuangalia wa kike hivi vijamaa viwili havipendi fulu kugombana.
Yaani ni mashitaka kila dakika.Huyu wa kwangu analalamika madogo wanaharibu vitu chumbani kwake na madogo wanalalamika kaka anawapiga na kuwafukuza chumbani kwake wasiangalie Tv.
Nikasema hizi stress zitaisha kila mtoto akiwa na tv chumbani kwake,nikatuma mtu akaninunulie Tv ndogo 4,zikaja zikafungwa kila mtu akafurahi nami nikasema nitapumua sasa ila nimejidanganya😃😃.eti baada ya kila mtu kupata Tv yake na interest ya kuangalia Tv ikaisha.Yaani madogo hawana muda na hizo Tv.Hela zangu zimepotea bure😭😭.
Hao wawili wa kiume ni mapacha wako very smart ila ni WATUNDU sana.Wamekaa siku mbili tu ila wameshaharibu vitu vingi halafu sasa vikiharibu kitu ukifoka unasikia “aunty you don’t look cute when you are angry” au “my daddy will buy you another one”
Leo asubuhi hivi vi twins vimefanya kitu cha hatari sana nikawatisha kuwa leo nawachapeni,nikaagiza niletewe fimbo mbili kubwa.Kumbe watoto wa watu hawajawaji kuchapwa wala kutishiwa fimbo.Kale ka kike kananiambia “aunty ukiwachapa baba yangu atakuchapa na wewe maana baba kasema mama akituchapa atamchapa na yeye” nikamwambia mimi simuogopi baba yako na fimbo zikija nawachapa kaka zako.
Fimbo zimefika ile watoto wanaziona tu waliteteeka hadi kamoja kakajikojolea na kengine kakatapika kwa panic.Nilishangaa sana maana mie wa kwngu keshakula sana mikwqju.Sasa nikajiuliza hata shule havichapwi hadi vitetemeke vile!
Ikabidi niache mkwara nianze kuvibembeleza na kutupa fimbo.Kale kakike kalivyoona nimetupq fimbo kakanimbia “usingenisikiliza baba yangu angekumaliza”
Huwezi kuamini hawa watoto eti kutishiwa fimbo tu wamelia zaidi ya masaa mawili.Na wanalia kwa kupokezana,huyu akinyamaza ukisema sasa wamenyamaza unashangaa mwengine kapokea .
Nimebembeleza nimechoka hadi na mim nikaingia chumbani kwangu kulia.Watoto hawa sijui baba yao uchumi ukiyumba itakuwaje coz wakitaka kitu lazima wapate la sivyo atalia siku nzima.Akitaka pizza kwa aman yako utahakikisha pizza imefika.Naona ajabu sbb mwanangu nikisema leo ni chai na kiporo cha ubwabwa kanakula.Mwanangu nikisema hata chai na ugali atakula with a smile on his face.Asubuhi ya kwanza the way vilitupelekesha ningekua na sukari ingepanda.Bodaboda walikua wanapishana getini kwetu coz kila tunachotumia sisi kwa breakfast walivikataa na kila kinacholetwa anakwambia sio hiyo ana favorite yake na lazima apate hiyo,unamrudisha boda ikija brand tofaut hali na hapo wako watatu na kila mmoja ana favorite yake.Ukisema uvikazie vitoto vya watu vitashinda njaa nafsi inakataa basi ni kuhangaika hadi kila mmoja apate anachotaka.
Hivi wazazi mnaodekeza watoto wenu faida ni ipi?
Mna upendo sana kushinda sisi wengine au?
Unaweza kuwasaidia hata kwa mwezi mmoja, na watabaki na kichwani kuwa aunt Pridah hataki hiki au kile.Huko kwao ndo wamelelewa kimayai mkuu.
Halafu mi naona haisaidii kutumia nguvu kustrress wabadilike hlf baada ya wiki chache wanarudi kwao kudekezwa tena.
Wangekua wamehamia kwangu moja kwa moja lazima ningewabadilisha
Ila nahisi naanza kuzoea sarakasi zao😀😀Itabidi kila mtu alee watoto wake, hawa kwangu wangerudi kwao wamekonda ingebakia lawama tu..
Hela za LG 4 kwa mkupuo natolea wapi mtumishi?😀Nilishangaa picha ulizoupload za TV zilikuwa na brand ya kuua macho,nikasema mmmh huyu ana mpango gani na kina junior?
Wanatuletea mizigo kwenye jamii yetu ya baadaeMy week end is wacko.
Kuna watoto wazuri wa rafiki yangu watakaa na mimi mpaka katikati ya Nov. ila sijui nisemeje nisionekane wicked aunty ila wamekuja J nne na tayari niko super stressed na Nov. naiona mbali sana
Stress zilianzia kwa jinsi mtoto wangu hataki ku share Tv yake na wenzie sbb wenzie ni wadogo na vitu wanavyopenda kuangalia ni tofauti.
Nikatoa amri waangalie kwa kupokezana ila haikusaidia watoto coz bado hao madogo wageni mmoja wa kike wawili wa kiume.Vitu anavyopenda kuangalia wa kike hivi vijamaa viwili havipendi fulu kugombana.
Yaani ni mashitaka kila dakika.Huyu wa kwangu analalamika madogo wanaharibu vitu chumbani kwake na madogo wanalalamika kaka anawapiga na kuwafukuza chumbani kwake wasiangalie Tv.
Nikasema hizi stress zitaisha kila mtoto akiwa na tv chumbani kwake,nikatuma mtu akaninunulie Tv ndogo 4,zikaja zikafungwa kila mtu akafurahi nami nikasema nitapumua sasa ila nimejidanganya😃😃.eti baada ya kila mtu kupata Tv yake na interest ya kuangalia Tv ikaisha.Yaani madogo hawana muda na hizo Tv.Hela zangu zimepotea bure😭😭.
Hao wawili wa kiume ni mapacha wako very smart ila ni WATUNDU sana.Wamekaa siku mbili tu ila wameshaharibu vitu vingi halafu sasa vikiharibu kitu ukifoka unasikia “aunty you don’t look cute when you are angry” au “my daddy will buy you another one”
Leo asubuhi hivi vi twins vimefanya kitu cha hatari sana nikawatisha kuwa leo nawachapeni,nikaagiza niletewe fimbo mbili kubwa.Kumbe watoto wa watu hawajawaji kuchapwa wala kutishiwa fimbo.Kale ka kike kananiambia “aunty ukiwachapa baba yangu atakuchapa na wewe maana baba kasema mama akituchapa atamchapa na yeye” nikamwambia mimi simuogopi baba yako na fimbo zikija nawachapa kaka zako.
Fimbo zimefika ile watoto wanaziona tu waliteteeka hadi kamoja kakajikojolea na kengine kakatapika kwa panic.Nilishangaa sana maana mie wa kwngu keshakula sana mikwqju.Sasa nikajiuliza hata shule havichapwi hadi vitetemeke vile!
Ikabidi niache mkwara nianze kuvibembeleza na kutupa fimbo.Kale kakike kalivyoona nimetupq fimbo kakanimbia “usingenisikiliza baba yangu angekumaliza”
Huwezi kuamini hawa watoto eti kutishiwa fimbo tu wamelia zaidi ya masaa mawili.Na wanalia kwa kupokezana,huyu akinyamaza ukisema sasa wamenyamaza unashangaa mwengine kapokea .
Nimebembeleza nimechoka hadi na mim nikaingia chumbani kwangu kulia.Watoto hawa sijui baba yao uchumi ukiyumba itakuwaje coz wakitaka kitu lazima wapate la sivyo atalia siku nzima.Akitaka pizza kwa aman yako utahakikisha pizza imefika.Naona ajabu sbb mwanangu nikisema leo ni chai na kiporo cha ubwabwa kanakula.Mwanangu nikisema hata chai na ugali atakula with a smile on his face.Asubuhi ya kwanza the way vilitupelekesha ningekua na sukari ingepanda.Bodaboda walikua wanapishana getini kwetu coz kila tunachotumia sisi kwa breakfast walivikataa na kila kinacholetwa anakwambia sio hiyo ana favorite yake na lazima apate hiyo,unamrudisha boda ikija brand tofaut hali na hapo wako watatu na kila mmoja ana favorite yake.Ukisema uvikazie vitoto vya watu vitashinda njaa nafsi inakataa basi ni kuhangaika hadi kila mmoja apate anachotaka.
Hivi wazazi mnaodekeza watoto wenu faida ni ipi?
Mna upendo sana kushinda sisi wengine au?
Nashukuru kwa namna fulani nimeanza kuwazoea.Bidada unaendeleaje weekend hii na hao watoto?
Siku nyingine usikubali kirahisirahisi kulea watoto wa kisasa.
Pole sana.Nashukuru kwa namna fulani nimeanza kuwazoea.
Nimewakazania sana naona sasa wanaanza kuelewa hapana na hakuna.
Shida kubwa imebaki kwenye utundu.
Hawa nahisi utundu wao ni wa kuzaliwa sio wa kudekezwa.
Kabisa aisee,sitachukua tena watoto kama siwajui vizuri
Pole sana.
Ila mimi nimefikia stage natamani sana watoto, hususan wadogo kabisa wale ambao mtu anaweza kuwalea vizuri yeye mwenyewe.
Ila tatizo siku hizi hata ukiwalea vizuri utotoni wakifika kwenye u teenager wanakubadilikia 😂😂😂
Hahaaaa.Teenager mbali sana kaka, kwanza vina tambua haki zao na ipeo mkubwa sana wa mambo.
Mfano vijamaa vyangu vinapenda sana vipikiwe chips, Sasa tukakubaliana kwamba, wakila chips mchana, usiku wale chakula kingine.
Siku hiyo taarifa inatolewa, vinasema but that is not fair, how can you make a decision for us? You should have called a meeting...wakati huo vitoto hata miaka 10 havijafikisha.