Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Then u simply concluded hakuna Mungu na ibada sio muhimu?
Nope sijasema hakuna Mungu. Anaweza akawepo, ila mpaka sasa hatujampata. Na hawa Mungu wote wanaohubiriwa hawapo.

Kwahyo kama hatujampata kwanini tuamini?
Atheism is not the beleif that there is no god.
Atheism is the lack of beleif in god.
Elewa tofauti hapo.

Ibaada ina umuhimu wake kwa waumini, ila kwangu mimi sasa haina umuhimu
 
Dah umeniharibia siku. Sikutegemea kusoma uzi wa kipumbavu kama huu. Miaka 24 ni mdogo na ubaya zaidi bado unaishi kwenu. Unajisikiaje unavyoona mama yako ananung'unika kwama hamfuati maelekezo yake? Wengi wetu huku town hatuendi kanisani ila tukifika nyumbani ili kumfurahisha mama ile siku ya ibada unabeba na biblia kabisa. Baada ya ibada lazima umsubiri asalimiane na watu wake kisha mrudi wote nyumbani. Mama akikunung'unikia ni mwanzo wa kujitafutia matatizo yasiyo ya lazima. Uache upumbavu wewe. Kama hutaki usumbufu hama hapo kajitegemee.
Nimekuelewa
 
Nope sijasema hakuna Mungu. Anaweza akawepo, ila mpaka sasa hatujampata. Na hawa Mungu wote wanaohubiriwa hawapo.

Kwahyo kama hatujampata kwanini tuamini?
Atheism is not the beleif that there is no god.
Atheism is the lack of beleif in god.
Elewa tofauti hapo.

Ibaada ina umuhimu wake kwa waumini, ila kwangu mimi sasa haina umuhimu
Mungu anasikia ilo
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Kwahiyo humu ndo kanisani kwako
 
Kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa andiko lako, umedhihirisha:

1. Ni jinsi gani huna nidhamu kwa Mama.
2. Ni jinsi gani huna midhamu kwa Mungu.
3. Ni jinsi gani unakwenda kuharibikiwa.
4. Jinsi gani una kiburi.

Note : Mama hana haki ya kululazimisha wewe kwenda Kanisan, ila huyu Mama anakupenda sana na anacholazimisha kina maana.
 
Nope sijasema hakuna Mungu. Anaweza akawepo, ila mpaka sasa hatujampata. Na hawa Mungu wote wanaohubiriwa hawapo.

Kwahyo kama hatujampata kwanini tuamini?
Atheism is not the beleif that there is no god.
Atheism is the lack of beleif in god.
Elewa tofauti hapo.

Ibaada ina umuhimu wake kwa waumini, ila kwangu mimi sasa haina umuhimu
Kama una note book andika nitayakumbuka yote nilio sema wakat nimechelew
 
Mi naomba nikuulize swali unijibu..
Je kitu ambacho hakipo kinaweza tengeneza kitu ambacho kipo na kinaonekana?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Nope sijasema hakuna Mungu. Anaweza akawepo, ila mpaka sasa hatujampata. Na hawa Mungu wote wanaohubiriwa hawapo.

Kwahyo kama hatujampata kwanini tuamini?
Atheism is not the beleif that there is no god.
Atheism is the lack of beleif in god.
Elewa tofauti hapo.

Ibaada ina umuhimu wake kwa waumini, ila kwangu mimi sasa haina umuhimu
Skia fany yaish
 
Mtii Mama Binti
Kakuweka vizuri maisha yanaenda hadi leo unauliza Mungu ni nani/hakuna Mungu

Maisha safari ndefu utajionea
Ila heri useme Mungu yupo na usimkute kuliko useme hayupo na uje umkute
Kama yupo actually itakuwa kosa lake kutojiweka wazi....hebu fikiria, Mungu angekuwepo tungekuwa tunabishana hivi juu ya uwepo wake?
Mbona hatubishani hivi juu ya uwepo wa Trump au Putin?

Au mumgu wenu amejificha makusudi?
 
Mungu ni neno
 
Mungu hutafutwa kwa maomb na kunyenyekea
 
SAFII SANAA[emoji23][emoji23][emoji23].

Kataa kabisa, usikubali wakulazimishe mambo usiyoyataka,
Hao wazazi waambie serikali haina dini, hivyo hata raia wana haki ya kuishi kulingana na wanachokiamin bila kubugudhiwa na mtu yeyote yule, na wakiendelea kukushurutisha wafungulie page za Kitabu cha sheria na katiba ya nchi wajionee[emoji23][emoji23].

Wakishindwa kukuelewa hapo basi waambie Dini isingekuwepo wangeabudu nini?[emoji23] huyo Mungu wanaempigia makelele makanisani waambie wakuoneshe ni wapi alisema ktk biblia wakutane makanisan? Na je ni kanisa lipi? Na dhehebu lipi? Na siku ipi? Wakikujibu maswali haya kwa mujibu wa biblia, basi kubaliana nao, lkn kwakuwa wao wenyewe pamoja na wachungaji wao hawana uwezo wa kujibu maswali haya, basi achana nao, usifuate ushauri wao.

Ni bora mkosane lkn si kukuforce uamini kitu usichotaka, mimi pia muhanga wa hili tatizo, walitaka mpka kunitenga lkn sikujari, nilikaza fuvu, siwezi kumuabudu Mungu aliyeletwa na watu weupe kwa manyanyaso na mauwaji ya watu weusi, kwanza imani yenyewe yakibaguzi.

KAZA FUVU HAKUNA KURUDI NYUMA
Dah mimi kwa hali hii nayoina nitarusha taulo nirudi nyuma..Maana kama mama anapata msononeko na mawazo kisa sijaenda kanisani, sio sawa.
Wacha nijiumize tu kumfurahisha, Maisha haya mafupi.
 
Back
Top Bottom