Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Ni halali yake kukushinikiza uende kusali atakako.
Unaishi kwake Kwa nini usifuate Sheria zake?
Wewe unaona swala la kusali linatakiwa liwe shurti? Yani sheria?
Yani ulazimishwe kusali? Ulazimishwe kutoa sadaka? Ulazimishwe kusikiliza mahubiri?
Hata kama huyaamini?

Em weka hisia pembeni za uzazi na utii...fikiria philosophically au basi ukishindwa hata theologically imekaaje?
 
You're such a moron
 
Ipo siku utamkumbuka mama yako kiburi cha uzima kisikudanganye . Nakumbuka sana baba yangu alikuwa akinisisitiza sana kusali nikiwa ingali kijana mdogo...
 
Mwenyezi Mungu akujalie akili ya kuona mbali. Kwa aina ya maisha unayotaka kuishi, utakuwa ni mwanamke wa hovyo kupindukia.

Maana sifa mojawapo ya mke mwema, ni ucja Mungu wake.
Hiyo ni 'imani' yako.
Yani ulivyosema hivyo ni kama vile wanaoenda kanisani hawatendi dhambi vile.

Let me tell you, mimi siendi kanisani lakini kwa maisha ninayoishi naweza kuwa wa kwanza kwenda mbinguni...(Kama ipo)
 
Mi natamani sana nipate mdada mwenye akili kama huyu, mwenye uwezo wa kutafakari.

Umenifurahisha sana, una akili na nzuri zaidi ni hiyo avatar ya mirabel, watu wanaongalia animation movies wana akili nyingi
Weeeh Mirabel hakua na akili chafu kama huyu.
 
Hata Hapa hakuna atakaywkuelewa dear.Hapa watamsapoti mama yako.
Mimi bana niko kama wewe niliachaga kuamini dini looong time ila hakuna anayejua sbb huko kwenye kujifanua mlokole ndiko ninakopatia ugali na mfuta ya gari.Ukinikuta anga zangu halafu mtu akuambie mie ni atheist lazima ubishe.
Pole ila usimueleze mama yako ukweli sababu hatakaa akuamini.Just play along.Barikiwa,😁
 
When purpose is not known abuse is inevitable.
Nimeanza na uwe msemo maana sasa nimegundua tatizo lako. Hujui umuhimu wa kanisa ndio maana huoni umuhimu wa kwenda. Uko sahihi sana.
Pole sana kwa sababu tatizo lako ni gumu kueleweka na utashutumiwa na wengi. Hata mimi mwanzo nalikulaumu lakini ni hakika unapaswa kuelemishwa na sio kulazimishwa.

Kama ningekuwa na namna basi ningechukuwa muda nikulisha ufahamu ili nafsi yako izaliwe katika roho na kupata uponyaji wa nafsi. Upo gizani tu pindi ukipata mwanga hakika utakuwa bora sana
 
Mleta mada hujitambui, yawezekena unatumia ngada au unasumbuliwa na ujuaji wa kijinga au usomi uchwara. Wewe mtu mzima gani unaishi kwenu, alafu unaambiwa na mzazi wako ufuate taratibu za mji wake unashupaza shingo. Au unataka wakati wanapoenda kanisani ubaki unamtafuna housegirl. Hapo Mzee akitangulia mbele za haki na wewe utatanguliza tumbo lako kudai urithi wakati sasa hivi unasema wewe ni mtu mzima hupangiwi Wala kulazimishwa. Kuwa na adabu kwa baba yako, na wewe utafanyiwa upuuzi km huu na watoto wako. Wazazi wako ni Mungu wa pili wanakuongoza kwa mema. Acha ujuaji na usera wa kijinga. Umeniudhi sana km Mzazi.
 
Asante, Nimegundua Athiest wengi ni critical thinkers maana hawana institution au dini yoyote inayowasaidia kufikiria...Ninashangaa hapa hata watu hawafikirii nje ya box. Yani wanafikiria ndani ya box la dini zao tu.
ila ajabu ningesema mimi naamini uislam mama analazimisha niende kanisani. Ungeona wanavyojaa kunitetea.
Hapa ishu ni mimi kuwa athiest ndio maana wananipinga.

Yani hizi dini zimefunga sana akili za watu.
 
Pamoja na kwamba siungi mkono kutokusali; ila kwa ulivyo andika tu, you are so bright na unahitaji kuelekezwa kwa hoja za nguvu na sio kwa mazoea. Pamoja na kutowiwa kwenda kanisani nakushauri Usome; kama ulisha soma Biblia jaribu kusoma Vitabu vya Dini tofauti.
Hii inaweza kukusaidia kwani bottom line; Mungu yupo, siku ya mwisho ipo, ambapo watu watahukumiwa kutoa haki kwa walioikosa hapa duniani ILA namna gani ya kumjua Mungu sahihi wa kumfuata ndio kazi hapo......SOMA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…